Hakuna sababu ya bunge la bajeti 2012

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
Nimeona niishauri serikali ya CCM iweze kusitisha maandalizi ya bunge la bajeti 2012/13 na sababu yangu kubwa ni kuona bajeti ya 2011/12 hadi sasa haijatekelezwa. Siyo halmashauri wala serikali kuu;ofisi zote hazipokei pesa na hazifanyi kazi, naiomba serikali sasa ipeleke pesa za maendeleo na pia isimamie bajeti ambayo hadi sasa imevurugwa kuliko kuitisha bunge litakalotumia pesa tena. Kama serikali imeshindwa kazi ni vizuri kuomba msaada wa kitaalam hata nchi jirani kama siyo kuitisha uchaguzi kabla ya 2015. Nionavyo yatatufika mabaya kuliko ya serikali ya mzee RUKSA
 
Halafu baada ya hapo ushangae pesa walizokuwa wameanza kullipana wabunge (posho ya laki 2) zilipitishwa na chombo/bunge lipi
 
Halafu baada ya hapo ushangae pesa walizokuwa wameanza kullipana wabunge (posho ya laki 2) zilipitishwa na chombo/bunge lipi

posho ni matusi makubwa ambayo serikali ya CCM imewahi kuturushia watanzania lazima tujitambue na tuiambie serikali hatutaki hili ama fanyeni lile: serikali zote lazima zitende matakwa ya wananchi wake na wananchi wakipaza sauti zinatenda. Tusiwe walalamikaji tu mitaani na kuishia kusifia kinafiki kisa tupewe madaraka
 
Ukitaka ona serikali ya CCM ikipinduliwa na wabunge wake ni hapo itakapotangaza kusitisha vikao vya Bunge kwa sababu zozote zile.
 
Kwanza wabunge wenyewe ni mzigo tu kwa serikali, hawana wafanyalo.
 
Back
Top Bottom