Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara Duniani

Mimi ugomvi wangu ni kwa waandishi wa habari wa hapa Tanzania. Kila mara tunaona wakifanya
mahojiano na viongozi wakuu wa serikali kuhusu miaka 50 ya "UHURU WA TANZANIA BARA". Hivi ni
kwanini huwa hawaulizi haya maswali rahisi lakini very tricky. Hivi hawa waandishi wetu (minus wa TBC1
na Radio Taifa hawa ni ma-vuvuzela wa watawala) huwa hawaoni waandishi wa nje wanavyojiandaa
wanapofanya mahojiano? Badala ya waaindishi wetu kuongoza mahojiano unakuta muhojiwa ndiyo
ana-dictate mahojiano.

Now wonder Mkapa aliwaita MAKANJANJA, the guy was extremly right!
 
Nimejaribu kuangali kupitia umoja wa mataifa kama kuna nchi hii inayo jiandaa kuazimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara.Nimejiuliza maswali mengi mojawapo kwanini nchi inakataa kuwa member wa UN kwa mda wote huu tangia ijipatie uhuru wake?
Kwa kufatilia zaidi ikanibidi ni ingie Google lakini huko pia sikupata web address ata home page ya hii nchi ya Tanzania Bara.
Nimekuja shangaa kuona kwamba Tanzania Bara inatambulia na FIFA lakini UN haitambui duh hapo ni kawaza tena.Kurudi tena Google nikitaka kuangalia nchi ya Zanzibar wakanipa kila kitu yaani home page imejaa taharifa zote za Zanzibar mfano muundo wa serikali,ramani,wizara etc.
Je Tanzania Bara ni nchi au siyo nchi na iko bara gani kwani hamna taarifa zinazoionesha kama hili taifa lina ishi hapa Duniani.Mwenye kujua anishulishe kwa njia zozote zile.

Labda kabla sijachangia nisaidie uhalalali wa kuwepo kwa nchi Duniani kunategema maamuzi ya ndani au ni lazima iwe Registered na UNO?
 
Binafsi nawashangaa sana hawa viongozi wa serikali wanapotosha watu kila siku na maneno yao yanayotaja tanzania bara.huku ni kupotosha jamii kabisa,kwa nini wanaogopa kusema tanganyika.

Kila siku matangazo yao yanataja uhuru wa tanzania bara,tanzania bara ipi?wamewaimbisha wasanii nyimbo eti ya uhuru wa tanzania bara,mi nashangaa sana kwa nini nchi inakosa viongozi wazalendo kiasi hiki.na bado eti wanahimiza uzalendo.....

Kama viongozi wa nchi wanaogopa na kukataza kutumia jina la nchi yao,ni nani atakaye litumia?sijui kwenye hizo sherehe hao wa britons watakao hudhuria hizo sherehe nao wataelezwa kuwa ni za tanzania bara au tanganyika,
 
Mkuu Averos,nchi kuitwa huru lazima itamburike kimatifa pamoja na umoja wa mataifa. Pia kuna vitu ambavyo vinaifanya nchi hiyo kuwa a legitimate and sovereign nation-state.

Moja wapo ni Serikali na Dora,wananchi, territory etc, Je Tanzania Bara inavyo vigezo hivyo? Kama vipo mbona haitambuliki ata hapa nchini kuliko Zanzibar inayotamburika kuwa ni nchi ata hapa Tanzania?

Nchi lazima iwe na kiongozi mfano raisi au mfalme,malikia na waziri mkuu kulingana na taratibu zao,je Tanzania Bara inatumia uongozi hupi?TUJULISHE HAYO MKUU.
 
Mimi nadhanani kuna haja ya somo la uraia lifundishwe siyo tu shuleni , nafkiri hata barabarani, makanisani, misikitini , kwenye baa na kote kwenye mikusanyiko ya watu. Hivi Wakati Tanganyika inaungana na Zanzibar kulikuwa na Tanzania?

Chemsha ubongo wako . Nimeamini sasa kweli humu JF kuna watu si raia wa nchi hii. ukiamua kusema Tanzania bara , sema pia Tanzania visiwani na ukiamua kusema Zanzibar, kumbuka pia kulikuwa na Tanganyika. Ila kwa kuwa hakuna serikali 3 ndiyo maana mmezoea kuita Tanzania bara na Zanzibar. Upo hapo?

Huwezi kupata Tanzania bara kokote ukishatoka nje ya mipaka ya nchi yetu, bali utapata Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama hujaelewa basi. Tatizo humu mmekalia majungu, chuki binafsi, roho mbaya. Jifunzeni historia ya nchi yenu mbona vitini vinavyoelezea historia ya Tanzania viko vingi?

Hii inshu bado kiini macho,nani amekuambia kuna tanzania visiwani na km ipo rais wake ni nani?
au rais wa hiyo unayoiita taznzania visiwani ndo rais wa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar?

Jaribu kufikirisha ubongo wako hata kwa dk 2 kabla haujatuhumu GT,na maana hoja za humu ni nzito na kwa taarifa yako vyombo vya habari ambavyo vinatangaza maadhimisho ya uhuru wa tanzania bara ni vya serikali na ccm na maswaiba wao ambao wanaficha ukweli,baadhi ya redio mfano magic fm inatangaza maadhimisho ya uhuru wa tanganyika na sio tanzania bara,hawataki kupulekeshwa hawa jamaa
 
we angali hata hizi wizara...mfano wizara ya mambo ya nje ni wizara ya JMT na haipo zanziba na pia wizara kadha wa kadha ni za JMT lakin wizara kama ya elimu ipo huku bara na zenji ipo zikijulikana kama wizara za SMZ, wizara ya kilimo iko zenji na huku bara ipo....sasa kama ndo hivyo hizi wizara zilizoko huku bara ni wizara za serikali IPI? hizi wizara za kilimo,elimu nK...
 
Mimi napata tabu ktk issue hii, kwa mfano wazanzibari hawaoni tabu kujitambulisha kama wazanzibari na pia vingozi wao wako hivo hivo.

Cha kushangaza nyinyi wenzetu Watanganyka hili jina hamlitaki na ndio maana viongozi wenu pia hawalipendi kulitumia hili jina musimlaumu Nyerere, na ikiwa wananchi wa watanganyika watakaza buti ktk suali hili basi Tanganyika itarudi kama zamani.

Sisi huku Zanzibar tunawapigia debe sana mupate serikali yenu lakini mwisho tunaonekana walalamishi, wabaguzi etc....!
 
Ni kweli kabisa hii nchi haipo lakini hawa waandishi wa habari ambao tunawategema wajuze umma nao wanakuwa vipofu kwa kusema uhuru wa Tanzania bara au Tanzania, but tukumbuke Tanzania iliundwa mwaka 1964 na haikuwahi kutawaliwa, kwa hiyo sio rahisi kuwa na uhuru, tanzania bara ni nchi ambay haipo kabisa.
 
hamna nchi a tza bara bali kuna watu wa tza bara yaani uko tunedako wote tutakuwa tanganyikeni
 
Siku zote mwenye jibu/majibu mazuri kwa maswali haya ni mch Christopher Mtikila ila tu niwaambie kuwa hiyo nchi haipo duniani ila ipo upande wa Tanganyika kwa muda ikisubiri Tanganyika itakaporudi. wakati wmingine ukiwauliza wazanzibar watakwambia Tanzania bara ndo nchi inayowatawala na wengine huenda mbele zaidi eti wanataka uhuru nao.
 
Hujasoma majibu yangu ya mwanzo. Soma juu kwanza upate niliyosema juu.
Unaanza matusi, character assassination, wewe sio muungwana. Ngoja nikuache maana siko style ya kwako. Wewe sio kundi langu.

asanteh kwa kumpuuza..
 
mimi sina tatizo na uhuru wa tanzania bara kwani mtoto akizaliwa akaitwa koku baada ya miaka minne akabatizwa na kuitwa anna haizuu kuendelea kusherekea birthday yake kisa kapata jina jipya...tatzo kwangu ni kwamba mbona zanzibar iko vilevile..
 
Tusiwalaumu waandishi wa habari,upotoshaji umeanzishwa na wana siasa. Hakuna nchi inaitwa Tanzania bara wala Tanzania visiwani. Kuna Tanganyika na Zanzibar. Na tarehe 9 December tutahadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom