Hakuna mwanamke fisadi?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Tangu vita dhidi ya Ufisadi ianze hapa Afrika mashariki, sijasikia mwanamke yeyote aliyetajwa kuwa FISADI.

Hii inanifanya nifikiri kuwa huenda wanawake ni watu waaminifu sana wakipewa uongozi wa juu katika nchi.

Labda wanawake ni waaminifu sana kutunza dhamana ya madaraka wanayokabidhiwa.

Au mnasemaje wanajamii?
 
Msemo huu umewahi kuusikia: kila mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanamke. Ufisadi unaweza kuwa mafanikio kwa fisadi. Je hao mafisadi wote ni sr bachelors?

Zile dhahabu za Lyatonga zilikuwa za nani? Yule mwanamke aliyewahi kunywa mihela ya NBC miaka hiyoo akiitwa Simbaulanga umemsahau? Labda kwa sababu hawajapewa nafasi ndio maana huwezi kuwaona kama ni mafisadi kiasi gani.

La mwisho,ufisadi hasa ni nini?
 
Kuna ukweli fulani katika jambo hili.

Wanawake si mafisadi kama ambavyo wanaume wako!

Malila hapo juu amewataja wanawake wawili tu, tena nao ni wa zamaani kwelikweli

enzi zileeee za Mwinyi! Sikatai kwamba wao si mafisadi, hasa kwa kuzingatia tafsiri

adhimu ya ufisadi, lakini kwa dhana hii ya sasa hivi ya ufujaji wa mabilioni bila

huruma, wanawake kidogo wako mbali , na hata wale wanaotinga mahakamani, ni

kwa kuhusishwa, na si moja kwa moja!

Hata gari yako ukitaka iuzike vizuri, ifanyie marketing kwa kuwaambia wateja kwamba

ilikuwa inaendeshwa na mwanamke, wala haitakaa!

Imani yangu mimi kwa hawa watu ni kwamba wapewe nafasi kubwa za kiuongozi,

maana hata kama watafanya ufisadi, hautokuwa sawia na ule unaofanywa na

mijaibaba:kutakuwa na chembe ya huruma kidogo.

Ndo hivyo.
 
wanawake wanaweza kuwa mafisadi kwa kuuma na kupuliza kama panya...

mfano mama yetu wa bunge a afrika aliyelazimishwa kujiuzulu...

ufisadi wa akina baba ni wa kubugia kila kitu kwa haraka haraka mpaka mwenye mali kustuka...mfano mzee wa viji-cent
 
Tangu vita dhidi ya Ufisadi ianze hapa Afrika mashariki, sijasikia mwanamke yeyote aliyetajwa kuwa FISADI.

Hii inanifanya nifikiri kuwa huenda wanawake ni watu waaminifu sana wakipewa uongozi wa juu katika nchi.

Labda wanawake ni waaminifu sana kutunza dhamana ya madaraka wanayokabidhiwa.
Au mnasemaje wanajamii?

Lakini usisahu, takribabani kwa kila mwanaume, nyuma yake kuna mwanamke!
 
wanawake wanaweza kuwa mafisadi kwa kuuma na kupuliza kama panya...

mfano mama yetu wa bunge a afrika aliyelazimishwa kujiuzulu...

ufisadi wa akina baba ni wa kubugia kila kitu kwa haraka haraka mpaka mwenye mali kustuka...mfano mzee wa viji-cent

Nyie mnasahau tu, Anna wa ANBEM? kwanza ndiye aliye mfundisha mr clean ufisadi! Make mama aliiba weee mijengo, sijui fursa kwa nani kaiba weee hadi kamwambia mzee tukwapue kabisa na mgodi wa kustaafia.

Zile anuani za ujasiliamali wa magogoni si ni za bibie?
Nasikia na Shadya naye kaanza kufanya vitu vyake huko Zenji, na wa mama mafisadi, tena wakubwa tu!
 
Mama Kejo kama sijakosea jina lake; ni yule wa ofisi ya mwanasheria mkuu. Hata mama Meghji alikuwa anahusishwa na ufisadi.

Ila wanawake ni nafuu kuliko wanaume. Ndio maana mwaka 2015 mimi na mama Migiro.
 
Ijulikane pia most of the high positions are occupied by men. And ufisadi in those high positions are more publicized then those done in lower posts. Pia like others have said some women might be encouraging their men to commit ufisadi just so they can live a luxurious life. Lakini pia there are some women who have been blessed with high positions na wakafanya ufisadi kama Mongela, kuna Zakia na pia mama "clean". hawavumi lakini wamo.
 
Lakini usisahu, takribabani kwa kila mwanaume, nyuma yake kuna mwanamke!

NONO,
MSEMO huo hauhalalishi kuwa wanawake wanahusika moja kwa moja katika ufisadi.

Mbona hatusikii tuhuma za moja kwa moja?
Bado kuna jambo la kufikiria hapa.
 
NONO,
MSEMO huo hauhalalishi kuwa wanawake wanahusika moja kwa moja katika ufisadi.

Mbona hatusikii tuhuma za moja kwa moja?
Bado kuna jambo la kufikiria hapa.

Mkuu umeshaambiwa kuwa Mama Mongela ametajwa na amelitia hasara Taifa, unataka wengine zaidi? Unamkumbuka yule dada liyefikishwa mahakamani kwa wizi wa fedha za EPA, au yule aliyehongwa kwenye kashafa ya IPTL. Wapo, usidhani kama wao nido wasafi kuliko wanaumwe. Kuna wengi tu, hata wezi kama S.M Simbaulanga. Hakuna cha kufikiri wapo wengi tu, nenda mawizarani ukasikie mambo utajua.
 
BONGO,
Nimekupata mkuu.
Kumbe ufisadi hauna jinsia.
Tujitahidi sisi wana JF tusiangukie katika huo ufisadi.
 
wanawake si mafisadi ila wanachechemiza ufisadi
angalia matokeo ya ufisadi ya walio wengi utakuta wameinvest kwa nyumba ndogoz na kadhalika........

maoni tu
 
Fisadi wa kwanza alikuwa mwanamke,ni yule wa pale Bustanini.

Tafsiri ya ufisadi kwa sasa inatumika vibaya.
 
Mke wa marehemu Balali pia anahusishwa sana ku-engineer wizi wa pesa za EPA akiwa connect ndugu zake akina Maregesi Law Associates (kama sikosei).
 
kwa hiyo mnapendekeza mfumo JIKE uchukue nafasi katika madaraka nchini Tanzania?
au kuna maana nyingine zaidi ya hiyo?
 
Back
Top Bottom