Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

nd. Kibai. Tatizo kubwa la social security zetu ni LOW INTEREST RATES. Haiwezekani nikatwe 1,000 leo halafu nipewe 1,001 baada ya miaka 30. Ndio maana watu wanataka wapewe chao. Vinginevyo viwango vikaribiane na COMMERCIAL & COMPOUNDED RATES. Kwa mfumo wa sasa mfanyakazi anapoteza kwa 'kuwekewa' akiba. Na hapo ndipo mrija ulipo.

kaka it depends na mfuko..huku pspf na lapf ndo kuna formular nzuri kuliko nssf...mtu aliyekuwa amefanya kazi kwa miaka 30 atalipwa michango yake tu na hiyo minor interest akiwa nssf...ila under pspf/lapf kuna kitu huwa kinaitwa time value of money huwa kinazingatiwa wakati wa kukotoa mafao...shilingi 1000 ya mwaka juzi sio ya mwaka huu....tumuulize huyo jamaa hapo juu aliesema kapata hundi ya kustaafu ya nssf ijumaa kapata kiasi gani,na kafanya kwa muda gani na alistaafu kwa mshahara gani then nikokotoe nikwambie ilikuwa apate kiasi gani kama angekuwepo huku pspf/lapf...
 
Kwa wasiojua NSSF ni cassino ya serikali ya JK. hakuna investment pale ni gambling kwenda mbele
 
WADAU WAENDELEE KUSUBIRI HADI LINI NSSF KUANZA KUENDESHWA KWA MFUMO WA SASA WA SOKO HURIA NA SERIKALI KUJIWEKA KANDO KAMA MRATIBU WA KILA KITU MLE BILA RIDHAA YA WADAU??

Kwa kuwa nchi yetu inafuata mfumo wa SOKO HURIA, hii inamaana kwamba taasisi zote ikiwemo NSSF nayo sharti iendeshe shughuli zake zote kwa kufuata taratibu zote zilizomo ndani ya mfumo huo ulioafikiwa na serikali yetu kwa hiari baada ya kuondokana na sera ya Ujamaa na Kujitegemea.

Mpaka hapo, mfumo huu wa soko huria unaielekeza NSSF kwamba kila mwanachama mmoja mmoja au kwa vikundi vyao, wanao UHURU WA KUJIUNGA NA KUJITOA wakati wowote ule. Vile vile soko huria inakataza ukiritimba wowote wa kusema mtu atalipwa tu pindi atakapofikisha umri wa kustaafu.

Ndio, tukiendelea mbele zaidi, mfumo huo huo wa soko huria vile vile unadai kwamba washikadau kuwekewa taarifa zote hadharani peupe kwa ajili ya wao wenyewe kujiamulia kile wakipendacho au wasichokipenda taasisi ya NSSF kufanya kwa kutumia jina lao na fedha zao za makato kwenye ujira wao.

Mpaka hapo, swali ni kwamba je wafanyakazi wa nchi hii wanataarifa kiasi gani juu ya watu au taasisi mbalimbali zinazokopa au KUJINEEMESHA TU hizo fedha zao?

Taarifa tayari zipo kwamba zipo baadhi ya taasisi zinazojimegea fedha NSSF kuendeshea kampeni za kisiasa kila baada ya miaka mitano; je hilo nalo wafanyakazi wanaliafiki kwa fedha zao??

Bodi ya NSSF ijitathmini kiundani vilivyo na kujiridhisha wenyewe kama kweli wangependelea taasisi hii muhimu kwa mustakabali wa wafanyakazi wa taifa hili litaendelea kuendeshwa kwa kufuata sera za Ujamaa na Kujitegemea (mfumo wa serikali kufanya maamuzi yote na uratibu kwa niaba ya washikadau) katika zama hizi za soko huria au nao wako mbioni kujitahidi kutokuachwa nyuma na wakati.

Hakika, NSSF huria inayoendeshwa kwa mtindo wa soko huria kwa kila kitu na wafanyakazi wake wote tangu ngazi za ufagizi hadi ukurugenzi nao kupatikana ki-ushindani badala ya uteuzi inawezekana.
 
Basi kama ni hivyo iwe ni hiari kwa mfanyakazi kujiunga na mifuko hiyo maana kujiunga tunalazimishwa na hata kustaafia kwa mwajiri yule yule iwe lazima ili upate mafao? What kind of colonialism is this??

TUMBIRI (PhD, University of Hull - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Kutokana ugumu wa maisha na kukosa ajira wanachama wengi tunateseka kwa kukosa jinsi ya kuishi. Makampuni yanatupunguza, NGO zinakufa na kadhalika sasa tunachotaka ni kushinikiza kutoa hela ndani ya mwezi mmoja hivi technologia kwenu inamaanisha nini? Kama wakati wa mwalimu miezi sita na leo wakati wa dhaifu miezi sita? Hamna computer, internet au nini tatizo lenu wiziwizi tu, hizi ni taarifa za awali kabla ya sheria yenu kandamizi tunaingia barabarani

NSSF ni DECI, ni muflisi kwa hiyo inahitaji muda kujipanga kukusanya hela ya kulipa
 
ALHAJI RAMADHANI DAU-Mkurugenzi mkuu wa NSSF. Naambiwa mwaka jana alichangia kampeni za CCM kwa kila mgombea ubunge nchi mzima kupewa 10 milioni. Makubwa haya.
 
Kabai tatizo sio kuweka akiba, tatizo la watu hapa ni kuwa, kuna watu wanataka kuastaafu kabla ya umri wa kisheria wa kustaafu ili wapate muda mzuri wa kufanya mambo binafsi na kufurahia maisha yao kabla hazijaja zile siku mbaya za uzeeni (ni mbaya kwa sababu kwa life style ya TZ, vichomi vinaanza mapema miaka ya 45 na unapofikia miaka 60, umeisha na unakuwa na uwezo mdogo sana wa kufurahiya maisha)/ Kumbuka kuwa maisha yako huyafurahii uzeeni! unayafurahiya ujananani!

Baadhi yetu tumataka kuondokana na utegemezi wa kutufanya watumwa wa waajiriwa wetu, kwa sheria hii inafanya watu sasa kama ataweka akiba yake ana kuamua kuwekeza akiwa na miaka 35 na akaacha kazi atalazimika kuziacha fedha zake kwa miaka 25!! this is not fair kwa inflation rate ya NCHI YETU!! lakini kwa wale walio na ndoto za kustaafia kazini hapa wamefika na hawana tatizo na hili.

Nilitegemea kabla ya kuandaa sheria hii waataalam wetu wangekuja na Data (takwimu) za ni watu wangapi na kwa namna gani waliochukua fedha yao mapema wameathirika kwa kushindwa kuzimanage, na wale walio staafu katika umri wa 55-60 wamefanya vizuri then wauconvise umma kuwa kuna umuhimu wa kuweka fedha yao mpaka ustaafu au vinginevyo. LKn hii mambo ya kutusaidia kufikiri na kutuamulia na kutupeleka kama mabwege haufai hata kidogo.
Ninaona kuwa mashirika haya ya kijamii wanataka kukamata hela ya watu wainvest walinde maslahi na mafao yao, waiushawishi umma kuwa hatujui kulinda future yetu!

Hivi mwenye kujua kuhusu PPF, maana ninavyo jua ili iningie kwenye pension scheme ni mpaka ucontribute kwa miezi 120 ambayo ni sawa na miaka 10. JE hii ina maama kuwa kwa sheria hii imeoverule hiki kigezo cha awali? na hata mashirika mengine kulikuwa na criteria ya kuingizwa kwenye pension scheme ambazo ndio unasubiri mpaka umri wa kustaafu!

Binafsi Hili ni pigo kwangu!

unaelekea pazuri tu na siyto mbaya humu ndani kaka tukawekana sawa, at least a different level of thinking. sasa kaka hii iko hivi, kuna kitun kinaitwa life styling! related to a person living on earth and namna ambayo anaweza manage risks zake. Ukiwa kijana mdogo it is believed kwamba unaweza kuwa na life expectance ndefu na kwahiyo you may engage actively kwenye risky business, lakini unapoanza 48 kwa tz kuelekea 50s ndipo sasa unaanza kukimbia kuwekeza kwenye maeneo risky, mfano hapa sasa ungeaza kununua treasury bills ama any risk free assets, ili ulinde fedha yako hata kama hupati faida kubwa, kwahiyo hata kama unataka kujiajiri, then that is a good saving vehicle, unaendelea kupiga kazi zako huku ukiendelea kuchangia kwenye mifuko hii na baadae unapata unafuu, hatusemi lazima mtu upate hasara kwenye biashara and this is not a negative thought of business lakini ni plan B incase sasa huko mbele huna kitu. Kama unaona hawa jamaa wanawekeza wenyewe then unasema okay, mimi sitaki ule mpango wa jumla unakwenda kwenye mpango wa akiba (Provident) unapata statement zako anytime u need them lakini hapa unabeba iunvestment risks mwenyewe that is the downside of it! mi nahisi we need ti open up financial consultancies kwa ajili ya watu binafsi. Na takwimu kaka zinaonyesha hata hii structure ya mafao ya sasa siyo nzuri sana watu wanachukua lumpsums kubwa halaf wana misuse tu, nunua dala dala thinking kwamba ni rahisi kumanage mtu baadae anaishiwa presure zinaanza and then anaenda, kwahiyo lets save jamani, miaka 10 ni lazima kwenye DB schemes, na its easy kufikisha kama hakuna shida watu wengi wana miaka zaidi ya 10 kazini so it is carefuly considered, nashauri tuunge mkono hili kwa NGUVU!
 
unaelekea pazuri tu na siyto mbaya humu ndani kaka tukawekana sawa, at least a different level of thinking. sasa kaka hii iko hivi, kuna kitun kinaitwa life styling! related to a person living on earth and namna ambayo anaweza manage risks zake. Ukiwa kijana mdogo it is believed kwamba unaweza kuwa na life expectance ndefu na kwahiyo you may engage actively kwenye risky business, lakini unapoanza 48 kwa tz kuelekea 50s ndipo sasa unaanza kukimbia kuwekeza kwenye maeneo risky, mfano hapa sasa ungeaza kununua treasury bills ama any risk free assets, ili ulinde fedha yako hata kama hupati faida kubwa, kwahiyo hata kama unataka kujiajiri, then that is a good saving vehicle, unaendelea kupiga kazi zako huku ukiendelea kuchangia kwenye mifuko hii na baadae unapata unafuu, hatusemi lazima mtu upate hasara kwenye biashara and this is not a negative thought of business lakini ni plan B incase sasa huko mbele huna kitu. Kama unaona hawa jamaa wanawekeza wenyewe then unasema okay, mimi sitaki ule mpango wa jumla unakwenda kwenye mpango wa akiba (Provident) unapata statement zako anytime u need them lakini hapa unabeba iunvestment risks mwenyewe that is the downside of it! mi nahisi we need ti open up financial consultancies kwa ajili ya watu binafsi. Na takwimu kaka zinaonyesha hata hii structure ya mafao ya sasa siyo nzuri sana watu wanachukua lumpsums kubwa halaf wana misuse tu, nunua dala dala thinking kwamba ni rahisi kumanage mtu baadae anaishiwa presure zinaanza and then anaenda, kwahiyo lets save jamani, miaka 10 ni lazima kwenye DB schemes, na its easy kufikisha kama hakuna shida watu wengi wana miaka zaidi ya 10 kazini so it is carefuly considered, nashauri tuunge mkono hili kwa NGUVU!

Kwa hali ya uchumi wa Tanzania, hilo la kulazimishwa kutochukua mafao yako unapoachana na mwajiri wako lipingwe na kupigwa vita na watu wote wenye akili nzuri. Mafao haya yana msaada na faida kwa baadhi ya mataifa ambayo yana uchumi mzuri lakini siyo Tanzania ambayo inflation ipo juu, currency depreciation haielezeki. Kama utachangia hela yako kwenye mifuko hii, ukaachishwa kazilabda ukiwa na umri wa miaka 35, ukawa huna kazi na ukaamua kujishughulisha na mambo yako ya kukuhakikishia mlo, hela yako uliyochangia huko NSSF ikalazimika kukaa huko kwa miaka 20, kama ilikuwa ni sh milioni 10, utakapoipata uwezo wake wa kununua bidhaa unaweza kuwa sawasawa na sh 100,000.

Wafanyakazi ni lazima waungane na walikatae hili kwa nguvu zote maana ni wizi wa wazi wa serikali dhidi ya wananchi kupitia mifuko hii. Serikali na uongozi wa mifuko hii wanajua kabisa wakipitisha sheria hiyo, itakuwa ni kama wafanyakazi wameipa mifuko hii pesa bila ya marejesho kwa wachangiaji. Wanafahamu kabisa kuwa sheria hiyo itawasaidia sana wao kupata pesa ya bure, na kile atakachopata mchangiaji, kwa walio wengi hakitazidi 10% ya kile alichochangia katika thamani. Huu ni wizi ambao unatakiwa kupigwa vita kwa kuungana kama wizi mwingine wowote. Kila mfanyakazi ni lazima atamke kuwa, 'kamwe sitakubali kuibiwa kwa mbinu ya kijinga namna hii'. Wanaiba hela ya PAYE, wameona haitoshi, sasa wanataka kuiba na michango ya wafanyakazi. Ama kweli mwizi huwa hatosheki, kila siku huzidi kupanga mbinu nyingi zaidi za kuiba.
 
Wana JF,

Kwa wale ambao ni WAFANYAKAZI tuhoji hili jambo kwa Serikali. Naamini kuna wafanyakazi ambao ni waandishi wa habari, jamani tusaidiane kujua ukweli wa jambo hili.

Nimefuatilia michango mingi hadi sasa , kuna mambo tunahitaji kujua/kuhoji:-
  1. Je, ni kweli sheria imeshapitishwa?
  2. Kama haijapitishwa, je huo mswaada utapelekwa bungeni lini au uko katika hatua gani?
  3. TUFANYE NINI KUZUIA kwa manufaa ya familia zetu?
 
hii sheria ikipita tuu ndio kifo cha CCM imewadia kwa sababu wamekula pesa zetu halafu wanataka kutupiga changa la macho.

Sisi tunaofanya kazi kampuni binafsi huwa tunahama kampuni moja kwenda nyingine kila siku huwezi subiri muda wa kustaafu kwa kuwa unaweza fanya kazi hat kampuni 20 mpaka kufikia muda wa kustaafu sasa itakua mbinde kuhusu zile kampuni ulizofanya kazi nyingine unakuata zimekufa na hazipo tena au kama zipo utakuta kumbukumbu zako hazipo sasa hebu angalia usumbufu ulipo hapo.

Hakuna mtu anaweza kukutengenezea maisha yako ya uzeeni hapa tanzania maisha yako utayatengeneza mwenyewe.

Nawaomba wabunge msithubutu kupitisha hili tafadhali,
 
Dah! Hii kali, ina maana hata wanaofanya kazi kwenye NGO nao itakuwa hivyo? Mbona hii ni kali ya mwaka. NGO inaanzishwa, baada ya miaka mitatu inaisha, wazungu wanasepa, mimi nina miaka 34, hadi nifike miaka 55-60 ni lini, na nitawatoa wapi wazungu wa kunijazia na kuthibitisha mafao yangu wakati shirika lilishakufa siku nyingi?
 
Ikipitishwa hii naacha kazi the next day. nani aliyewadanganya wote tumezaliwa kwa ajiri ya kuwafanyia wengine kazi maisha yetu yote? miaka sitini ni full life time, nichukue mafao yangu at age 60 ili inisaidie nini? Amani imewachosha hawa.
 
Ni kitu kizuri kama watafanya hivyo maana wengi wa vijana tunaohama hama kwenye ajira ukifika umri wa kustaafu hatuna kitu.
 
Wizi mwingine huo, hela ya mtu, mtu wa pili au tatu asiipangie majukumu. Hiki ni kifo kingine kwa wafanyakazi, afe na njaa au ashindwe kutibiwa kisa eti afike 60+ what if ugonjwa alionao utamuua, nani atumie hiyo fedha.

Hoja hapa nini kuhusu huu wizi? Serikali inataka iwe na uhakika wa kuzikopa sio??? HATUTAKI huo mpango. HATA mpango wenyewe wa mafao ni kwa kizamani sana, isiwe lazima kuweka hiyo mifuko pesa, iwe hiari ya mtu. Kama unaona unafaidika nao weka kama unaona unakitu kingine cha muhimu kufanya kama kununua kiwanja, uwekezaji , usafiri, biashara ni bora mtu akatumia fedha yake kama anavyotaka kuliko huu upuuzi.
 
kama ni kweli basi sisi tuliopo kwenye sekta binafsi ndo tuko hatarini zaidi ya kudhulumiwa mafao yetu, kwa waliowahi kufuatilia hela zao nssf nafikiri wanajua athari za hii kitu, makampuni binafsi mengine huwa hayadum kwa mda wote huo.so kampuni ikifa utapata wapi nyaraka za kukusibitishia malipo yako?
mfano ukienda nssf unapewa form ya kuonyesha namna malipo yalivyokuwa yanaiingizwa na mwajiri wako na ni lazima aijaze mwajiri wako, sa kama hayupo na kampuni ilishakufa itakuwaje?
HUU NI WIZI NA UDHULUMAJI SABABU MBAKA SASA WENGI HATULIDHIKI NA UENDESHWAJI WA HII MIFUKO HASA UKIZINGATIA WAO WANATUMIA PESA YAKO WANAPATA FAIDA ILA HAWAKUONGEZEI CHOCHOTE WEWE ULIYEWAPA MTAJI.
 
Huu ni wizi wa wazi wazi kabisa,ukifanya kazi miaka mitano kwenye sekta binafsi nakuwa umeongeza mtaji NSSF.
Sikubaliani na hili hata kidogo kuna ulazima wa watu kupigwa mawe hapa.
 
Back
Top Bottom