Hakuna klabu ya Sudan iliyowahi kuifunga Simba

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,604
20,336
Inawezekana kuna watu hawajajua bado kuwa hakuna hata klabu moja ya Sudan iliyowahi kupata ushindi kwa Simba. Kama nimekosea, aje mtu anisahihishe hapa. Hata mwaka ule El-Mereikh walipovunja pambano la CECAFA, walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 hadi dakika ya 89, na wakawapiga sana wachezaji wa Simba. Bahati nzuri Simba na El-Mereikh zikapangwa kucheza raundi ya kwanza klabu bingwa Africa, ambapo Simba ilishinda 1-0 Dar na ikashinda tena 1-0 Khartoum. El-Mereikh hawatamsahau Nteze John hata siku moja Timu ya El Hilal (ambayo ilijenga urafiki na Simba baada ya kuona Simba inawafunga mara kwa mara El-Mereikh watani wao), nayo pia imeshapigwa mara kadhaa na Simba. Kwa hiyo hii Al Ahly Shandy itakuwa klabu ya kwanza kuifunga Simba kama itafanya hivyo mjini Shandy, Sudan, jambo ambalo si rahisi hivi hivi.
 
unauhakika na unacho kinena?
 
unauhakika na unacho kinena?
Humu kuna watu wamejaa porojo zisizokuwa hata na msingi, na ukimuuliza umri wake unaweza kushangaa hata miaka 30 hajafikisha ndio maana anaongea pumba kwa jambo asilolijuwa.
 
Hadi sasa hakuna aliyeleta data zinazokinzana na hizo, zaidi ya kutukana kama wazee wa Yanga
 
Hapa hatufanyi mashindano ya umri mkuu, it is the matter of records...
Kwa style hii sishangai kwanini Yanga Afrika wamewapa timu wazee wa miaka 65+ badala ya kuchochea vijana wenye mwazo chanya.
Humu kuna watu wamejaa porojo zisizokuwa hata na msingi, na ukimuuliza umri wake unaweza kushangaa hata miaka 30 hajafikisha ndio maana anaongea pumba kwa jambo asilolijuwa.
 
Humu kuna watu wamejaa porojo zisizokuwa hata na msingi, na ukimuuliza umri wake unaweza kushangaa hata miaka 30 hajafikisha ndio maana anaongea pumba kwa jambo asilolijuwa.
we unalolijua ni lipi sasa kuhusiana na kilichoongelewa????
 
al-ahly shandy...
Dakika ya 66, 77 na 88.
Simba wakabadilishwa Pampers na kusubiri mikwaju ya penati.
Mtoa mada futa hii thread yako inatia aibu, coz watu walishaanza kusahau.
 
Humu kuna watu wamejaa porojo zisizokuwa hata na msingi, na ukimuuliza umri wake unaweza kushangaa hata miaka 30 hajafikisha ndio maana anaongea pumba kwa jambo asilolijuwa.

kwani kuijua historia laziam uwepo? wewe mbona unajua kuhusu vita ya dunia ulikuwepo ama ulishiriki?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom