Hakuna kiongozi mwenye busara na hekima ndani ya serikali yetu?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Bango lililoshikwa na waandamanaji limeandikwa kwa maandishi makubwa kabisa
KWA AMANI na wakati huo polisi wakitumia silaha kali kuzima haki ya wananchi kidemokrasia ni ushahidi wazi wa jinsi serikali ya Tanzania inavyokandamiza haki za raia wake.
Wimbo uliotawaliwa na hadaa za viongozi wetu kuwa Tanzania kisiwa cha amani nini maana yake yaliyojilia pale Arusha?

Kati ya waandamanaji na serikali nani amevuna amani pale Arusha?
Serikali kupitia vyombo vya dola ndiyo iliyovunja amani na inaendelea kuvunja amani.

ULIMWENGU UMESHUHUDIA HAYO YALIYOTOKEA ARUSHA NA NDIVYO SERIKALI INAVYOZIDI KUJICHAFUA KIMATAIFA

Naonja hata mtoto wa Mkulima alipoomba radhi kwa niaba ya serikali na CCM ilikuwa binafsi tokana na dhamiri yake safi mbele ya jamii
 
Ndugu yangu, siku zote na popote duniani panapotokea uvunjifu wa amani basi ni serikali iliyopo madarakani ndio chanzo na kamwe si upinzani. Lililotokea Arusha ndivyo ilivyokuwa Kenya, ndivyo ilivyotokea Ivory Coast n.k.
 
Back
Top Bottom