Hakuna kama cheka Tanzania

Freddy81

Member
Feb 3, 2009
99
3
NGumi%20k.c.jpg

Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro (Kushoto) akimtwisha konde mpinzani wake Japhet Kaseba kwenye pambano la raundi 12 kuwania mkanda huo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Ijumaa usiku.(Picha na Khalfan Said)



Juzi usiku alidhiilisha kuwa hana mpinzani nchini kwa sasa baada ya kufanikiwa kumpiga bondia Japhert Kaseba wa Dar es Salaam katika pambano kali la uzito bantam lilofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Hatahivyo, pambano hilo liliingia doa baada ya wapambe wa Kaseba kuingia ulingoni katika raundi ya tisa na hivyo kuanzisha vurugu zilizopelekea pambano hilo la raundi 12 kuvunjika katika raundi hiyo ya tisa.
Katika pambano hilo lililoanza saa 2:02 usiku baada ya kumalizika kwa mapambano ya utangulizi, Cheka alionekana mapema kupania kummaliza mpinzani wake baada ya kumshambulia mfululizo kwa makonde ambapo hata hivyo mengi yalikwepwa na Kaseba huku na yeye akijaribu kutupa makonde ya kushtukiza mwishoni mwa raundi hiyo ya kwanza.
Kuanzia raundi ya pili na kuendelea Cheka alimdhibiti vilivyo mpinzani wake, huku na yeye (Kaseba) akijaribu kumtupia makonde ya kushtukiza lakini pamoja na kujitahidi huko bado alishindwa kwenda sawa na nguvu za Cheka.
Kaseba alionekana kuishiwa nguvu kuanzia raundi ya saba ambapo alitumia zaidi kujilinda lakini katika raundi ya nane alidondoshwa chini mara mbili ambapo kuna wakati mwamuzi wa pambano hilo Anthony Rutta aliingilia kati kumuokoa.(NDO AKOME!!!!)
Huku raundi ya tisa ikienda ukiongoni na Cheka kuonekana kama angeibuka na ushindi wa 'Knocck Out' wapambe wa Kaseba walivamia ulingo na kumshambulia Cheka kitendo kilichopelekea pambano hilo kuvunjika.
Kufuatia hatua hiyo waandaaji wa pambano hilo huku wakitumia sheria zote za ngumi walimpa ushindi Cheka kutokana na ukweli kuwa mpaka pambano hilo linavunjika Cheka alikuwa akiongoza kwa pointi nyingi dhidi ya Kaseba.
Kufuatia vurugu hizo zilizodumu kwa dakika 20 Jeshi la Polisi lililazimika kumuondoa Cheka uwanjani kwa gari la polisi ili kukwepa kushambuliwa na wapambe wa Kaseba ambao walionekana kutoamini kipigo cha bondia wao.
Akizungumza mara baada ya pambano hilo, Cheka alisema hilo ni onyo kwa mabondia wengine wanaojitapa kuwa wana uwezo wa kucheza na yeye na kuwataka kujiandaa kikamilifu kabla ya kuomba kupigana naye.
 
Back
Top Bottom