Hakuna jipya baraza la mawaziri

Megawatt B

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
259
69
Ndugu zangu, wengi wetu tupo macho wazi kusubiri ni mabadiliko gani yatafanywa na mkulu, nawahakikishia hakuna jipya tusubiri mwaka 2015 panapo majaliwa. Watu makini hawapewi nafasi kwa kuwa hawapo bungeni na hata kama wapo bungeni si watu wakujipendekeza hivyo hawawezi kufikiriwa, mambo ni yaleyale. Mtu akichukuliwa msukule harudi, hata akionekana tena hujue ni zezeta huyo!
 
Mi nawahurumia sana watanzania wenzangu mnaotegemea jipya kutoka kwa jk na ccm yake! CCM jamani ilikufa na Mwalimu! iliyopo sasa hivi ni mzimu tuuondoe kwa kura basi!!wewe lala au hata chukua muda huu kuwafundisha wanao mambo kadhaa ya maana kuliko kusubiri jipya toka kwa ccm ya jk!!!!!!!!!!
 
ngoja tuusikilizie huu usanii....binafsi naamini kabisa kwa ccm hii ya jk hakuna chochote zaidi ya mipangilio na usanii km kawaida yake,MUDA NI HAKIMU MZURI...tusubiri tuone
 
Nafikir kwa sasa thread zetu zilenge katika namna ya kuikomboa TZ kutoka ktk mikono ya hawa wezi(MAGAMBA) coz hata akifanya mabadiliko ni usanii mtupu hakuna jipya ndugu zangu
 
Tumechoshwa na hizi habari za baraza la mawaziri. Kama hamna issue ya maana nyamazeni.
 
Am back from exile,yanayotokea Tanzania katika utendaji mbovu na kutowajibika kwa serikali suruhu yake sio baraza jipya bali serikali na mifumo mipya ndo tiba.
 
Huwezi kutegemea baraza jipya wakati unafahamu ni urafiki binafsi. Baada ya kuteua marafiki wa mwanzo sasa hivi msanii wetu hana list mpya.
 
Back
Top Bottom