Hakuna hata kidogo!

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
438
65
Mwarabu mwenye duka alimwambia kijana anayemsaidia kuuza duka.
"usimwambie mtu kuwa hakuna kitu hapa dukani, kama hakuna mwambie kimekwisha leo lakini tutaleta vingine muda si mrefu.
Siku moja walikwenda watu, wakawa wanauliza kwa sauti ya chini, kijana akajibu kwa sauti "hakuna hata kidogo!"
Wale watu walipoondoka Mwarabu akamfokea sana yule kijana kwamba "nilikuambia usimwambie mtu hakuna kitu. kwani walikuwa wanauliza nini?"
"Walikuwa wanauliza kama mvua zinanyesha eneo hili ndio nikasema HAKUNA HATA KIDOGO".
 
Back
Top Bottom