Hakuna hasara kwa kuhifadhi samaki walionaswa

paesulta

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
227
29
Date::10/26/2009
Magufuli: Hakuna hasara kwa kuhifadhi samaki walionaswa
Na Festo Polea

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli amesema kuwa hakuna hasara yoyote badala yake hilo ni somo kwa wavuvi haramu na kwamba sekta ya mifugo inastahili kupongezwa kutokana na ushindi huo.

Waziri Magufuli aliitoa kauli hiyo jana mara baada ya kufungua mkutano wa Chama cha Wenyeviwanda vya Kusindika Samaki (TIFPA) uliokuwa ukijadili jinsi ya kuendeleza sekta ya mifugo na kuondokana na matatizo yanayoikumba sekta hiyo na wenye viwanda vya kusindika samaki kwa ujumla.

Mahakama iliagiza kuuzwa kwa samaki wote waliokutwa kwenye meli iliyokuwa ikifanya uvuvi isivyo halali kwenye ukanda wa kiuchumi wa pwani ya Tanzania. Mahakama ilitoa amri hiyo baada ya upande wa mashtaka kuomba amri hiyo kwa hoja kwamba mgao wa umeme utasababisha ubora wa kitoweo hicho kupungua.

Hadi wakati mahakama inatoa amri hiyo, tayari gharama za kuhifadhi samaki hao ambao ni tani 296 kwenye kiwanda cha Bahari Foods, Mwenge jijini Dar es salaam zilishafikia Sh6.6 bilioni ambazo ni zaidi ya thamani ya samaki hao aina ya jodari.

“Waandishi wa habari mnaripoti kuwa ni hasara... hiyo si hasara kwa kuwa samaki hao wakiuzwa fedha itakwenda serikalini, na kwa kuwa kesi haijaisha meli yao iliyokamatwa bado tunayo na kwa kufuata sheria ya mwaka 2007, haki itapatikana kwa kuwa gharama ya kutafuta haki ni kubwa hivyo kesi ikikamilika mtaona kuwa hakuna hasara kwa serikali,’’ alisema Magufuli.

“Unajua ukimshika mhalifu lazima umpeleke kwenye vyombo vya sheria na hapo ndipo sehemu ya kutafuta haki na haki inapotafutwa... lazima kuwe na gharama; mimi naona ni ushindi na wananchi walipaswa kutushangilia na kutusifu badala ya kudhani hakuna kilichotendeka.’’

Meli hiyo ya Tawaliq 1 ilikamatwa Machi 8 na kikosi maalumu cha doria katika Bahari ya Hindi na ilikutwa ikiwa na raia 37 wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi huo haramu.
 
Back
Top Bottom