Hakuna dawa ziponyazo kwa ugonjwa wa CCM

Emashilla

Senior Member
May 24, 2012
138
26
NAPE UNATUPELEKA WAPI? NI HUZUNI KUDAI WANAOHAMA CCM NI SAWA NA VINYAGO!

Dalili ya maradhi ndani ya CCM ni mbaya kuliko miaka yote iliyopita. Na sasa imebainika, "Hakuna dawa yoyote ya kuisaidia CCM, Bali adhabu yake ni kuing'oa madarakani" katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Siku si nyingi aliwaita kero ndani ya chama, na magamba, na mizigo, na oil chafu, na sasa asema ni "Vinyago." Operesheni mabadiliko ya CHADEMA inayoshika kasi nchi nzima kwa sasa na kuendelea hadi kieleweke, yampa homa Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM.

Jana akiwa huko kusini mwa Tanzania katika juhudi zake za kujaribu kuzuia "hama hama" ya CCM na alipoona hali ni ngumu akaleta usemi mpya, yaani "Vinyago" na kusisitiza,

"Wanaohamia vyama vya upinzani ni vinyago. Hakuna chama cha upinzani ambacho hakikuanzishwa na wanachama kutoka CCM."

Aliongeza, "Sasa! kinyago ukichonge mwenyewe kikuogopeshe?"Nape Nnauye waombe radhi watanzania na viongozi wa upinzani nchini Tanzania , hasa CHADEMA maana umewaudhi wapenda haki na mabadiliko ya kweli.
 
Hata mtu akiwa mahututi icu kama hakuna dawa ya kumponyesha unaweza kutumia busara ya kumpa dawa ya kumwahisha ili kumuondolea maumivu.
Dawa ya ccm ipo.
 
Back
Top Bottom