Hakuna cha Kamera, wala ushirikina - Polisi

Hili kundi la mafisadi limekusudia kisasi hasa kwa spika na wabunge walio kinyume nao.
 
Kuna kitu ambacho Sitta hakijui, wengine wanakijua ama vinginevyo amemua kusalimu amri, watu wanajua kuwa kuna mtu aliingia bungeni ila haikuwa usiku, ilikuwa mchana na alizunguka zunguka humo ndani akiwa na mtumishi wa Bunge, na alizungukia hadi kiti cha Spika na picha zipo zimetiwa kibindoni.

Kwa hakika huu ni usanii mwingine, ulizeni waliokuwa kwenye kikao cha wabunge wa CCM ama kikao fulani hivi. Kwa uzembe tunaambiwa hata Kamera za ulinzi zilikuwa ziii, kuna watu walirekodi wakitaraji kupiga dili.

Wale watu mle ndani walikaa muda mrefu sana kulingana na kanda hizo. hapa kuna something, na hata mtumishi wa Bunge aliyehusika analindwa maana alichofanya inasemekana ni kinyume cha sheria.



Ohoo, hii Bongo land Bwana.
hao jamaa wenye hizo picha si watumwagie hapa ili tuwaumbue mafisi-adi?
 
naamini sasa watu sasa wamerudi kwenye drawing board.
kila upande ukingojea move ya mwengine.
naamini hakuna cha mahakamani wala nini
kwani jamaa watakodoleana macho tu.

dr. mwakyembe alisema tume yake inazo taarifa
amabazo wamebanisha sasa na katika hili kila upande
unahisi huenda wenzao wanalo la zaidi lakini wamebanisha
tu. matokeo yake? kimyaaaaaaaa
 
Mhnnnnnnnnnnn........ninaguna na majibu yaliotolewa kea mujibu wa uchunguzi wa Mkemia Mkuu kwani simuelewi.

Hii inaelekea kumsema Spika wa Bunge aliongopa.........je tunaweza kupata ukweli Spika aliposema kamera zilinasa watu wawili kuwa ndani ya ukumbi wa Bunge alitoa wapi taarifa hii?

Na je, Mkemia Mkuu alipelekewa samples atafute sumu au athibitishe uchawi na urozi?

KUNA JAMBO LINAFICHWA KWA NIA YA KUSAFISHANA HAPA.........!!!!!!!!!

Na nasema Spika ajiangalie kukolimbwa na yeye baada ya muda si mrefu......nina wasi wasi!!!!
 
Sasa kivumbi kutimuka. This time ni zamu ya SIX maana jamaa wa Vijisenti aliahidi kumburuza mahakamani. Mmmh wote ni wanasheria, na kama serikali kupitia Polisi, Mkemia Mkuu na Usalama wa Fisadi wanaficha ukweli hapa ndo tutaona UTAMU wa Mlenda from Tabora na Mchele(wali) from Bariadi. Sisi yetu macho kuangalia mafahali 2 wakitoana ngeo. JK this time una kazi kuhakikisha amani haivunjwi maana naanza kunusa harufu ya Mafisadi ku-face hasira za waziwazi kutoka kwa wananchi. Na unatambua wakichukia basi chochote kitakachokuwa mbele yao ni halali yao. Kaa chonjo bro maana naanza kuona zile style za Sungusungu, fimbo na mtu. Na tusipoangalia hata silaha za jadi zaweza tumika vilevile dhidi ya FISADIZ maana hawana fimbo za moto mlizonazo. Jaribu kuwasaidia kuwa kuwafungia Segerea.
 
Sasa kivumbi kutimuka. This time ni zamu ya SIX maana jamaa wa Vijisenti aliahidi kumburuza mahakamani. Mmmh wote ni wanasheria, na kama serikali kupitia Polisi, Mkemia Mkuu na Usalama wa Fisadi wanaficha ukweli hapa ndo tutaona UTAMU wa Mlenda from Tabora na Mchele(wali) from Bariadi. Sisi yetu macho kuangalia mafahali 2 wakitoana ngeo. JK this time una kazi kuhakikisha amani haivunjwi maana naanza kunusa harufu ya Mafisadi ku-face hasira za waziwazi kutoka kwa wananchi. Na unatambua wakichukia basi chochote kitakachokuwa mbele yao ni halali yao. Kaa chonjo bro maana naanza kuona zile style za Sungusungu, fimbo na mtu. Na tusipoangalia hata silaha za jadi zaweza tumika vilevile dhidi ya FISADIZ maana hawana fimbo za moto mlizonazo. Jaribu kuwasaidia kuwa kuwafungia Segerea.

Hapa ndipo utamu ulipo, ndio maana nilisema hii ni starter.

Anna Makinda kafunga mjadala kwa kutumia maamuzi ya Bunge kuwa Sitta hajasema bungeni kuhusu ushirikina. Je, maamuzi ya mhimili mmoja wa dola, bunge na yanaweza kuhojiwa na mhimili mwingine, mahakama?

Lakini Chenge ana mwanya mkali zaidi, kauli za masuala ya ushirikina Spika Sitta aliitoa kwa magazeti siku chache kabla ya kutoa kauli rasmi bungeni.

Kwa hiyo kauli hii aliitoa nje ya bunge haihusiani na azimio la jana la bunge, Chenge akimbilie mahakamani tu kwa kuchafuliwa jina.

Lakini akifika mahakamani Sitta ataanika ukweli ambao umesemwa kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge na Tume ya Utumishi ya Bunge ambayo haijasemwa kwenye taarifa ya mkemia mkuu wala Taarifa ya polisi kwamba: "Chenge na mtumishi wa Bunge waliingia bungeni na kuzunguka bila taratibu. Walionekekana wakifanya vitendo visivyojulikana kwenye viti ikiwemo cha Spika". Kwa hiyo itakuwa ngoma droo, wote chenge na Sitta ni wasanii wa kutupwa, ndio utamaduni wa chama cha mafisadi. Kulindana na kuogopana! Ndio maana narudia tena, chakula ni Kiwira, Richmond, Meremeta, desert ni EPA lakini hatutashiba mpaka mwaka mwaka 2010

Asha

Asha
 
Siwapendi na siwataki wote, Sitta, Chenge, Makinda, ushirikina na kauli ya kutaka kutulazimisha kuwa mjadala umefungwa. kama wamefunga, wafunge wao Bungeni, kwa nini wawalazimishe na wartu wengine kuufunga mjadala?
 
Mkanda upo na picha ya chenge inaonekana wazi na nini alikifanya kipo wazi. Ila kilichopelekwa kwa mkemia ni majivu na mchanganyiko wa madawa ya kienyeji ambapo sio rahisi kuwa sumu ila kwa imani. Sitta aliuona mkanda na maafisa wa ulinzi wa bunge.

Polisi wameona mkanda hii nimepata live kutoka kwa baadhi ya maofisa wa polisi wenye vyeo vya juu dodoma. Polisi hawataki kusema kwamba au kutamka jina la chenge kwani Sitta aliuona mkanda na anayo kopi ila hataki kuliambia bunge kwamba aliyeyeko kwenye mkanda ni Chenge. Polisi na ofisi ya bunge imetupiana nani wa kumfunga paka kengele. mwishowe wameamua kutulisha garasha.
 
Wanamaombi kutinga bungeni wiki ijayo

2008-07-13 22:26:42
Na Simon Mhina

Kamati ya Umoja wa Makanisa ya Kikristo nchini, imemuandikia barua Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, ikimuomba awaruhusu waende Dodoma kulizunguka Bunge kwa ajili ya maombi na kusisitiza kwamba hawaamini taarifa iliyotolewa na Polisi kwamba unga uliopatikana ndani ya jengo hilo haukuwa na uchawi.

Kadhalika, Kamati hiyo imewashauri mawaziri na wabunge wenye hirizi kuzisalimisha kwao kabla ya kuanza maombi kwani wanaweza kuumbuka.

Pia Kamati hiyo imesema hatua ya Naibu Spika kufunga mjadala kuhusu `unga wa uchawi` haiwakatishi tamaa kufanya maombi hayo.

Kamati hiyo imesema taarifa ya polisi imewachanganya na sio sahihi kwa sababu dola haiamini mambo ya uchawi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamti hiyo, Askofu Isack Kalenge alisema uchunguzi huo wa Polisi, Mkemia Mkuu, Bunge na Usalama wa Taifa ni batili kwa kuwa vyombo hivyo ambavyo viko chini ya serikali, havina uwezo wa kutambua uchawi.

Askofu Kalenge, ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Pentekoste International, alisema wanaamini kuwa bado uchawi upo bungeni na wabunge wengi wanateswa na nguvu hizo za giza.

``Uchawi ni jambo la kiroho, haliwezi kupimwa kwa kamera wala uchunguzi wa Mkemia Mkuu, tunaamini tatizo la uchawi bungeni halijapatiwa ufumbuzi, tunakwenda Dodoma kulimaliza tatizo hilo ili lisitokee tena,``alisema.

Akizungumza katika mkutano huo, Mchungaji Wilbert Ngowi alisema kamati hiyo haiwezi kufumbia macho taarifa hizo, kwa vile zimeliaibisha Taifa.

``Umefika wakati sasa kanisa liseme yale ambayo lilikuwa linayafumbia macho na lifanye mambo ambayo yalikuwa hayafanyiki, japokuwa hatua hii inaweza kutafsiriwa kwamba tunachanganya dini na siasa, lakini si vibaya.

Kuanzia sasa tumeamua kuchanganya dini na siasa kwa sababu maandiko matakatifu yanasema kufanya hivyo sio dhambi,``alisema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji Christopher Mtikila alisema iwapo watapata ushirikiano wa Spika wataenda bungeni wiki ijayo.

Akifafanua, kiongozi huyo alisema wamemuomba Spika awape kibali cha kuingia bungeni kuwaombea wabunge na `kuharibu` nguvu za giza zilizojaa humo.

Mchungaji Mtikila alisema kabla hawajatia mguu Dodoma, wanawataka Wabunge, mawaziri na yoyote ambaye anatembea na hirizi aisalimishe kabla hawajaanza maombi.

``Ni matarajio ya Kamati kwamba wabunge wazalendo, hususan wale ambao hawatembei na hirizi vibindoni, watafurahia kazi hii njema ya watumishi wa Mungu yenye lengo la kuwaponya,``alisema.

Kiongozi huyo alisema iwapo watakataliwa kufanya mambo hayo, watalizunguka jengo la Bunge hilo na kurusha `makombora ya sala` na kuahidi kwamba hakuna mwanga wala hirizi itakayosalimika.

Aliahidi kuwa wabunge na mawaziri, ambao ni wapenda uchawi, wataumbuka vibaya kutokana na sala hizo.

Alisema tayari waumini mbalimbali wameshaanza kufunga kwa ajili ya kujiandaa na sala hiyo.

Alisema hawatarajii upinzani kutoka kwa Bw. Sitta kwa sababu hivi karibuni Spika huyo alinukuliwa akiwataka viongozi wa dini, kuliombea Bunge kutokana na kuwa katika wakati mgumu.

``Sisi tumeamua kwenda kuliombea Bunge kama alivyosema, ila sisi tutaenda na mamlaka makubwa, ambayo yatasambaratisha kila roho chafu.

Sisi wenye macho ya kiroho tumejua kwamba pale ndani pametundikwa kila aina ya uchawi, lakini hakuna hata mmoja ambao utasalimika,``alisema.

Akizungumza na Nipashe jana, Spika wa Bunge, Bw. Samweli Sitta, alisema bado hajapokea barua hiyo.

Hata hivyo, Spika alikataa kuzungumza iwapo atawaruhusu kutekeleza azama yao hiyo mara atakapopata barua yao.

``Hilo unalouliza ni jambo jipya, lakini siwezi kulisemea kwa vile sijapata barua yenyewe. Ni vema ukaandika zaidi maoni ya hiyo kamati,`` alisema.
 
I knew kwamba watakanusha, lakini hii ni sababu ya political correctness. In the long run tutajua nani ni loser na nani anajua anachokifanya.
 
I knew this was crap! Nchi haiamini katika uchawi (at least ndivyo sheria zetu zinavyosema). Sasa Spika na kukurupuka kwake anasema mtu alikuwa anawanga! We need to be some steps ahead of these crazy ideas.
 
Huyu Ac nimemuogopa sasa si mchezo anajua kucheza dala kweli kweli. Amefunga la maradona sasa.

Mambo mengine tusiyachukulie ki mzaha tu! lazima mtu uingie ndani na ujue chanzo ni nini!

mimi mwenyewe sijui nani ataukamata usukani 2010, kwa taarifa yako hivi sasa kila mtu anafanya analoweza.
 
Basi watanzania, waandishi wameshaandika kuhusu hilo jambo wameuza magazeti, wameridhika, manake ilikuwa ni skendo, lakini kwa sasa, mwandishi wa kufuatilia kutuhabarisha mahali palipokuwa na tatizo, au utendaji wenye tatizo katika serikali yetu hatapatikana.
Mfano, kuna mtu alidanganya, kama kuna watendaji hawakufanya wajibu wao, au kuna polisi/wachunguzi walioonyesha utendaji mbovu, au kuna watu wameshawajibishwa, au wamepewa onyo, au kuna mtu kazi ya utawala imemshinda
Haya ndio mambo mimi nayotamani kuyasikia na kuyajua.
 
Back
Top Bottom