Hakuna cha Kamera, wala ushirikina - Polisi

hakuna jambo baya kuliko kufanya utafiti huku ukiwa na majiabu yako mfukoni


mara nyingi matokeo yakija kinyume na matarajio yako utajaribu kulazimisha na ikiwezekana kucheza na data


sasa hapa kuna watu wana majibu yao na si mengine ila chenge ndie alieonekana na alikuwa akitia sumu au kuroga kinyume na hypothesises hizo ni uongo na changa la macho

mie kama mtu ambae nimebahatika alau kidogo kupata kupitia skuli na kukaa na waliosoma nnaamini kila utafiti hufanyika kwa kuzingatia requrements zake na data zilizopatikana sasa ripoti iko hivo tuaminiane ndio ukweli ulivyo tusonge mbele
 
Ukweli ni kwamba hawa jamaa wa hili kundi wana nguvu sana, ni almost serikali ndani ya serikali yetu, muungwana naye pia inaonekana kuwa either wamemizdi nguvu au yuko nao, kwa sababu haiwezekani hata Waziri Mkuu akaogopa watu ndani ya serikali ambayo yeye ndiye kinara, sasa anamuogopa nani?

Maana sio siri tena among wakuu wa taifa kuwa uamuzi wake on Meremeta, haukuwa wa kwake, kwa sababu according to the data in the private anaongea maneno mazito sana dhidi ya mafisadi, sasa iweje akija public anakuwa bubu? Anamuogopa nani? Hatuwezi kusema kuwa anamuogopa Shein,

Sasa Pinda anamuogopa nani? Hata huu uamuzi wa polisi na unga wa vumbi, hauwezi kuwa umeamuliwa bila ya kumfahamisha mapema, ndio maana umechukua karibu mwezi mzima kuutoa maana yake ni kwamba walikuwa kwanza wana-touch base zote kwanza!


Je ni shilingi ngapi zimetumika kwa jaili y akutoa Ripoti hiyo na uchunguzi kwa ujumla?unaweza kukuta ni million 50.
 
Aaaaaaaya holaaa mmh!
Duh mbona kuna watu waliwaona wanaingia Bungeni kisha mmoja wao alisema walikuwa wanatafuta pa kukaa sasa Polisi nao wanasema hawajaona mtu kwenye CCTV ooh ulikuwa mzimu nini.
 
Nawashauri kuachana na mada hii, mtaumia vichwa bure. Tukubali tu yaishe. Tusonge mbele. Bao jingine hilo tena la kisigino.

Wa TZ tumezoea kudanganywa kila kukicha na tunakubali kila upuuzi.Twendelee hivyo hivyo siku zao wajajanja na mafisadi zinakuja. Mwisho wenyewe watashindwa na sisi wadanganyika tutashinda kwa JINA LA YEYE ALIYE JUU.AMEN
 
Akina Chief Matunge, Profesa MajiMarefu, Sheikh Yahya Hussein, Dr. Tamba, walishirikishwa? Wangeshirikishwa, tungepata majibu ambayo WENGI WETU tuliyatarajia!
 
Kama ni Mwungana mbona amekaa kimya? Hawa ni watendaji chini yake. Amewachukulia hatua gani. Usilaumu njama. Laumu inaction ya Mwungana. He is his own worst enemy.

He is part of the game if not Mwenyekiti wa kamati unategemea aseme nini?
 
All this is an insane, hivi wanatuona majuha? chiligati alivosema AC alikuwa akitafuta kiti cha kukaa. leo hii wanatuambia kamera haikuonyesha kitu???

Na tangu lini Polisi/mkemia akajua chunguza uchawi?
 
Kuna hawa jamaa wanaoitwa wataalam wa SSTL wako Mwananyamala, kazi yao kuuza vifaa vya security hasa CCTV cameras, Leo eti ni maanalyst ambao serikali inataka tuwaamini. Are they certified for that job????????

Only in TZ
 
kumbe uchawi kweli unafanya kazi...mimi nilikuwa siamini,mpaka leo!

Kwi! kwi! kwi! huu ni mkali mpaka serikali na bunge lake zimeingia mkenge?

Inabidi tuushindanishe na ule wa Pemba, Tanga au Sumbawanga ili tujue nani top.
 
Chenge ameonakana akicheka akicheka pembeni, kwani sasa hivi wakati wengine wote mmeshikilia magalasha/sa yeye kashikilia majembe kwenye karata zake... aamue tu acheze vipi.. nani awe wa kwanza kushtakiwa? Sitta, Magazeti, ...

Hawezi kumshtaki yeyote kwani anajipenda na anatambua wazi kuwa akimshtaki mzee six ataagiza yaliyofichwa yafichuliwe na yule Afisa wa bunge atakuwa shahidi.

Mungu iponye Tanzania ipo hatarini.
 
Tunasubiri HOJA BINAFSI toka kwa Mh. Chenge ya kumtaka Spika apime kauli na vitendo vyake Bungeni aone ni HATUA zipi achukue......
 
)

a. Hakuna Kamera iliyozimwa kuanzia mwaka 2006 (don't ask me walisema zilikuwa zimezimwa)
b. Kwenye mkanda uliodaiwa hakuna mtu aliyeonekana akifanya jambo lolote lile (mkanda mtupu?)
c. Vumbi lililoenda kuchunguzwa halikuwa na sumu yoyote inayotambulika.
d. Hakuna kitendo cha kishirikina.

Polisi wana uwezo gani wa kuchunguza mambo ya kishirikina?

Inabidi pia tufike mahala tukubaliane lengo la haya makamati kwenye nchi yetu huwa ni kuwasafisha watu fulani na wala sio kutafuta ukweli wa mambo, naogopa kusema kwamba hii ni pamoja na kamati ya "shujaa" wetu Mwakyembe!
 
Polisi wana uwezo gani wa kuchunguza mambo ya kishirikina?

Inabidi pia tufike mahala tukubaliane lengo la haya makamati kwenye nchi yetu huwa ni kuwasafisha watu fulani na wala sio kutafuta ukweli wa mambo, naogopa kusema kwamba hii ni pamoja na kamati ya "shujaa" wetu Mwakyembe!

Wadau nimeielewa sana taarifa ya polisi lakini katika kuielewa huko bado imenifanya niibue maswali yafuatayo
1. Taarifa ya kukiri kwamba chenge aliingia kutafuta kiti hadi mwenyewe akakiri nayo ya uongo?kwa mujibu wa polisi cctv kamera hata hilo tukio linalodaiwa halali la kutafuta kiti halikupigwa picha ilihali camera zilikuwa on?kama jibu ni ndiyo basi
2. Camera za bunge zina upendeleo katika kuchukua matukio
3. Maelezo ya sitta kwamba picha zilikuwa zimefifia yalikuwa na maana gani?kwa tafsiri yangu kama vile unavyoona negative sasa mbona taarifa haisemi hicho kilichokuwa kimefifia kilikuwa ni kitu gani?labda ni dust bin au kiti cha spika ili wadau waamini zaidi?
3. Kwa mantiki ya maelezo ya polisi sitta naye mwongo alikuwa akihisi tu hakupata wala fursa ya kuona huo mkanda kabla haujasafishwa na chiligati naye mwongo vilevile kwa taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa mhe.alkuwa kitafuta kiti cha kukaa.Kwani matukio yote haya hayakuonekana na mkanda ni mtupu kabisa
4.Toka lini polisi au mkemia mkuu akaweza kuchunguza ushirikina?Polisi katika ripoti yao wangeishia kusema tu kwamba hakukuwa na sumu kwani uwezo wao wa kiuchunguzi unaishia kwenye sumu na kemikali hilo la ushirikina wangelitolea conclusion nyingine kabisa.

Ama kweli this is tanzania
 
Hii ni moja ya hadithi za kuchekesha kweli. Yaani kama hadithi za sungura mjanja vile. Fisi unamkabidhi kondoo wako akulindie, then what do you expect. Kama kitendo cha kishirikina kilifanywa na mbunge wa CCM tena mwenye hadhi ya Chenge, basi tusitarajie kupata lolote la maana. Hizi ni kama story nyingine nyingi tu na visa kibao vinavyofanywa na viongozi wa CCM and they get away easily.
 
Kuna kitu ambacho Sitta hakijui, wengine wanakijua ama vinginevyo amemua kusalimu amri, watu wanajua kuwa kuna mtu aliingia bungeni ila haikuwa usiku, ilikuwa mchana na alizunguka zunguka humo ndani akiwa na mtumishi wa Bunge, na alizungukia hadi kiti cha Spika na picha zipo zimetiwa kibindoni.

Kwa hakika huu ni usanii mwingine, ulizeni waliokuwa kwenye kikao cha wabunge wa CCM ama kikao fulani hivi. Kwa uzembe tunaambiwa hata Kamera za ulinzi zilikuwa ziii, kuna watu walirekodi wakitaraji kupiga dili.

Wale watu mle ndani walikaa muda mrefu sana kulingana na kanda hizo. hapa kuna something, na hata mtumishi wa Bunge aliyehusika analindwa maana alichofanya inasemekana ni kinyume cha sheria.



Ohoo, hii Bongo land Bwana.
 
Tunashukuru angalau wametoa majibu

kuliko mtu akujibu utumbo bora asijibu maana kama ni mwanao unaweza kumng'oa meno. basi tu unajua mazingira yalivyo kwenye hili swala hatuwezi kuwatandika hawa majuha.
tulikuwa tunasubiri majibu ya uhakika siyo angalau jibu alimradi ni majibu. tulitaka majibu yaliokwenda shule, majibu kutoka kwa wasomi wanaoheshimu taaluma zao, watu wanaoheshimu kazi yao. lakini ndio hivyo mwanga na mchawi hawezi kuumbuana.
 
Back
Top Bottom