Hakuna 'Baraza Kivuli la Mawaziri' - Wassira

eti wasira anasema yeye anauzoefu na uongozi mbalimbali hata mbali ya Tanzania, anasema
ameanza kuwa mbunge akiwa na umri wa miaka 25 ambayo hakuna mbunge wa sasa,
akawa anatoa mfano wa serikali ya marekani kuwa huwa serikari tawala wanakuwa
na figure yao na wapinzani wanakuwa na figure yao mwisho wanakubaliana kwa figure
moja.
Inaonyesha wasirra sio progressive... ya nini kujisifia kufanya kazi hiyohiyo kwa miaka alfu lela u lela?

The old man is just passed his age, he should just step aside

Nani ana clip atuwekee??
 
Asubuhi hii nimeangalia tbc,kulikuwa na mjadala ulimuhusisha Mh Mbowe na Wassira!

Mbowe akatoa hoja kuwa serikali ya CCM ni dhaifu, ilishindwa kuangalia maswala muhumu wakati wa bajeti, hasa ya Nishati,na ya uchukuzi, ndio maana walitupiwa vitabu vyao.

Wassira akapandwa na jazba, akaanza kutukana kuwa mawaziri vivuli wote ni mbumbumbu na CHADEMA si wapenda amani na mengine mengi! Mbowe naye akachombeza!'Hii ndio serikali yetu na hawa ndio mawaziri tulio nao!
Hii imekuwa kawaida kwa wabunge/mawaziri wa ccm wanapokua na midaalo na Chadema kwani wanashindwa kujibu hoja za chadema na kupandwa na jazba na kuanza kung'akang'aka je hawajui ndio wanajimaliza kisiasa na kuwapa chadema uwanja wajutamba zaidi na hili ndio tunalolitaka
 
Basi sema wewe ni nini maana ya kivuli. Ninavyojua hata mimi kivuli ni kitu kisichokuwa halisi. Tena huwa hakiwezi kutokea mpaka kuwe na jua. Kwahiyo hapo CCM ndiyo jua halafu inamulika vivuli kama CHADEMA navyo vinatokea.
The Shadow Cabinet (also called the Shadow Front Bench or Shadow Ministry) is a senior group of opposition spokespeople in the Westminster system of government who together under the leadership of the Leader of the Opposition form an alternative cabinet to the government's, whose members shadow or mark each individual member of the government. Members of a shadow cabinet are often but not always appointed to a Cabinet post if and when their party gets into government. It is the Shadow Cabinet's responsibility to pass criticism on the current government and its respective legislation, as well as offering alternative policies.

In the United Kingdom and Canada the major opposition party and specifically its shadow cabinet is often called His or Her Majesty's Loyal Opposition.[SUP][1][/SUP] The adjective "loyal" is used because, while the role of the opposition is to oppose Her Majesty's Government, it does not dispute the sovereign's right to the throne and therefore the legitimacy of the government. However in other countries that use the Westminster system (for example, New Zealand), the opposition is known simply as The Parliamentary Opposition instead of shadow.

Some parliamentary parties, notably the British Labour Party and the Australian Labor Party, elect all the members of their shadow cabinets in a partyroom ballot, with the Leader of the Opposition then allocating portfolios to the Shadow Ministers. In other parliamentary parties, the membership and composition of the Shadow Cabinet is generally determined solely by the Leader of the Opposition.

In most countries, a member of the shadow cabinet is referred to as a Shadow Minister. In Canada, however, the term Opposition Critic is more usual.
 
Hii ni kuthibitisha kwamba magamba mmechoka kimwili na kiakili. Unachokiandika hapa hata hakieleweki, umekurupuka bila shaka toka usingizini kama anavyokurupuka wassira. Wasilianeni na magamba mwezako unayekubaliana naye ili mje na tafsiri sahihi.

Huyo halipwi na Nape, nafikiri ni bosi mwenyewe anayemlipa. Sijajua labda anatetea jengo la THT huyo, mwache atapetape.
 
nimemdharau sana Wasira leo...ana jazba za kipuuzi kweli na hana maana yoyote....Mbowe amemjibu kwa busara sana
 
Viongozi kama WASIRA hatufiki,Leo siyo mwaka wa 1965...ni tofauti mzee wangu sijui ulidhani umekaribishwa kwenye kipindi cha ENZI HIZO? kituko cha mwaka TBC1 mzee alipokuwa na mahojiano vs Mbowe iweje asitoe kashfa kwamba baraza la mawaziri wa mbowe ni feki.

Mbowe kwa ukomavu,kwa hekima,kwa utulivu ,huku amekula nne, alijibu kwa hoja kama kawaida.

kuna huu msemo mbowe aliutoa wakati mzee anaropoka....HII NDIYO AINA YA SERIKALI TULIONAYO NA NDO MAWAZIRI TULIONAO.

Kwa nn WASIRA UMEWAIBISHA MAWAZIRI WENZAKO NA SERIKALI KWA UJUMLA.???

PLSE MZEE NAKUSHAURI UNG'ATUKE SOON.Maana unaelekea kubaya .
 
wasira anaumia maana kwa % serikali inafanya kile kinachosemwa na upinzani...na huyu wasira ni mpuuzi tu yuko cc kwa sababu ya naa yake wala hana jipya
 
Nimeamka asubuhi late nakutana na Mbowe na Wassira TBC 1 jambo Tanzania. Sijajua hasa yaliyojiri ila nilichoona ni kuaniki kwa Mh Wassira!

Anasema CHADEMA ni chama cha ajabu cha upinzani maana kinakosoa kila kitu, hakijawahi kukubaliana na serikali hata siku moja. Anasema

Mbowe hana baraza la mawaziri (vivuli) coz they are so weak. Kwamba Mbowe hana serikali. Kwamba CHADEMA ni chama cha maandamano tuu

na hawataki amani. Nadhani alikuwa anakana kuwa bajeti ya serikali haijafumuliwa!

MAJIBU YA MBOWE
Mbowe kwa upole amesema anamheshimu Wassira na hivyo hataki kuingia kwenye malumbano naye. Kwamba wao wanapata muda mdogo mno bungeni, na hivyo wanautumia kuishauri serikali zaidi kuliko kuisifia. Wassira alipong'aka na kutaka kama vile kukasirika, Mbowe alisema 'Hawa
nido mawaziri wetu, hii ndio serikali yetu'?

Halafu akauliza kama wassira anasema mbowe hana mawaziri kwani sasa hivi tunaserikali?

Nawasilisha wakuu, aliyeona toka mwanzo atujuze yaliyojiri zaidi. Thank you

Japokuwa mimi si mshabiki wa chadema lakini leo Mh. Mbowe ameonesha uvumilivu na busara ya hali ya juu. Kama wabunge wote wa chadema watakuwa hivi, basi baadhi yetu ambao tunashuku kila kitu tutaanza kuamini ukomavu wa upinzani.
 
Basi sema wewe ni nini maana ya kivuli. Ninavyojua hata mimi kivuli ni kitu kisichokuwa halisi. Tena huwa hakiwezi kutokea mpaka kuwe na jua. Kwahiyo hapo CCM ndiyo jua halafu inamulika vivuli kama CHADEMA navyo vinatokea.
kwa sasa nikiifananisha ccm na mfalme juha nadhani nitakua sijakosea kutokana mambo wanavyoyapeleka sasa especialy Jk juha juha kweli ukitaka kuamini angalia utendaji wa baraza lake pamoja na viongozi mbali mbali aliowateua pia na utatuzi wa matatizo yanayojitokeza ktk serikali
 
Mbowe: 'hii ndio aina ya serikali tuliyonayo' hili jibu nimelipenda sana ni pia haina haja yakujibizana na mpumbavu kumpuuza ni azabu na tusi kubwa kwake
 
Hasira za wasira zinatuletea wananchi hasira,
kama alivyo wasira,viongozi wa ccm wanahasira na jazba,
Wasira hatufai kwa sababu ana hasira,

Na siku zote hasira hasara,Wisira punguza hasira,
Kiongozi mwelevu hana hasira,bali mpumbavu anakuwa na hasira,
Hasira hasara,viongozi tuache hasira,tuwe na hekima.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom