Hakimu mkazi au resident magistrate ni nani?

EPORA

Member
Apr 8, 2012
83
16
Habari wakuu! Naomba kujuzwa hivi hakimu mkazi manake nini hasa ni yule anaekaa karibu na mahakama au anaishi karibu na mahakama nielewesheni wataalamu wa lugha,nawasilisha!

=====

Mahakama nchini Tanzania ina vyombo vitatu: Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahakama Kuu za Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa Tanzania Bara. Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Mwanzo.

Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa Tanzania Bara ina:Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania(Mwenyekiti); Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania; Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu; na Wajumbe wawili walioteuliwa na Rais.

Mfumo wa sheria ya nchini Tanzania unaongozwa na Jaji Mkuu na Msajili wa Mahakama ya Rufaa kama Mtendaji Mkuu. Jaji Kiongozi(JK) akisaidiwa na msajili wa Mahakam Kuu, ndiye anayesimamia utawala wa Mahakama Kuu na Mahakama zilizo chini yake.

Mahakama Kuu imegawanyika katika Kanda, zinazosimamiwa na Mahakimu wafawidhi wakisaidiwa na Wasajili wa Wilaya. Katika ngazi za Wilaya na Mkoa, utawala uko chini ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mkoa na Wilaya. Mahakimi Wafawidhi wa Wilaya pia wanasimamia Mahakama za mwanzo katika wilaya zao zinazohusika.

Kutoka kwenye uchumi dhabiti kuelekea kwenye ufunuo wa soko huria nchini Tanzania, kumeifanya Mahakama ikabiliane na hukumu tata katika maeneo kama sheria ya ushirika, sheria ya kazi na ubunifu, sheria ya biashara, miamala ya biashara ya kimataifa, miamala ya ardhiuhalifu wa kimataifa, udanganyifu katika miamala ya fedha ya kimataifa na aina nyingine za uhalifu wa kiofisini. Haili hii inahitaji utaalamu na ubobezi zaidi, hasa katika sheria za biashara. Tanzania kama zilivyo mamlaka nyingine za sheria, imeshughulikia tatizo hili kwa kuamua kuanzisha kitengo cha biashara cha Mahakama Kuu kushughulikia kesi za Biashara ingawa ngazi ya sharti la ubobezi zaid halijafikiwa
 
tafuta magistrate act usome nenda government bookshop
kwa vile watanzania ni wa vivu wa kusoma hata kugooge imekushida acha
nikupe kiduchu. hakimu Mkazi kaainshwa ktk hiyo sheria ni nani
kwa Tanzania ni graduate wa LLB, ambae kafanya interview na kufaulu vema usahili wa kuwa hakimu mkazi
ataapishwa na jaji mkuu.
huyo anakuwa na uwezo wa kusikiliza mashauri ktk mahakama ya hakimu kazi
zamani ilikuwa ni mahakama za mikoa pekee ila kwa sasa hata mahakimu wakazi wanapelekwa ktk mahakama za wilaya ambako walikuwa district magistrate ambao zamani walikuwa na diploma
kwa hivo hakimu mkazi akipelekwa wilayani anaitwa district resident magistrate
jurisdiction zao ni kesi zote za jinai,madai nk ispokuwa mauaji,nk
mengineyo watakujuza wengine.
 
Lokissa umeeleza vizuri lakini mimi bado sijaelewa ni kwanini walipewa jina la hakimu mkazi hata kama wana sifa fulani za elimu?
 
Mahakama ndio inaitwa hivyo na sio hakimu. Ngoja waje weeleze sababu, 'Resident Magistrate Court"
 
Hakuna kitu kama mahakama ya mkoa kwenye mfumo wa sheria zetu. Mfumo wa mahakama unaanzia 1. Mahakama ya Mwanzo. 2. Mahakama ya Wilaya. 3.Mahakama ya Hakimu Mkazi. 4.Mahakama Kuu, na 4. Mahakama ya Rufaa.
kweli kabisa mkuu
 
Mahakimu wa Kisutu ndio Mahakimu wenye Kesi za Maana, na Escrow, ma EPA, Ma Richmond na watakatisha Fedha wote wanshtakiwa Kisutu!

Hakimu wa Kagera au Sumbawanga ataishia kusikiliza kesi za Imani za kishirikina na Migogoro ya Kijinga jinga
 
Hawa jamaa wana kihede hede.. Wanazikimbilia kesi alafu utasikia wanalalmika kuwa hawana uwezo wa kuzisikiliza.. If so kwa nini hizo kesi zisianzie mahakama kuu moja kwa moja ili mshitaki na mshitakiwa wapewe haki yao upesi? A law reform is needed here.
 
Mahakimu wa Kisutu ndio Mahakimu wenye Kesi za Maana, na Escrow, ma EPA, Ma Richmond na watakatisha Fedha wote wanshtakiwa Kisutu!

Hakimu wa Kagera au Sumbawanga ataishia kusikiliza kesi za Imani za kishirikina na Migogoro ya Kijinga jinga
Hata hawa mafaili yanapitia mikono yao tu ila hizo kesi nzito huwa zinatolewa maauzi na mahakama kuu.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mahakimu wa Kisutu ndio Mahakimu wenye Kesi za Maana, na Escrow, ma EPA, Ma Richmond na watakatisha Fedha wote wanshtakiwa Kisutu!

Hakimu wa Kagera au Sumbawanga ataishia kusikiliza kesi za Imani za kishirikina na Migogoro ya Kijinga jinga
Hahahahaaa! Weye mkuu acha fujo. Nami nahamia ku-Ndalisilama.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom