Hakika sasa nimeamini alichosema Dr. Slaa kuhusu Kikwete

NdasheneMbandu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
940
308
Wakuu,

Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 nilipata kuisikia kauli maarufu ya Dr. Slaa kuhusu madhara ambayo nchi hii ingepata endapo kikwete angechaguliwa mara nyingine tena. Dr. Slaa alisema kwamba kumchagua kikwete na CCM yake ni kukaribisha janga la kitaifa na wananchi watakuja kujutia uamuzi wao.

Leo hii, ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa, wananchi katika kila kona ya nchi wanalalamika ugumu wa maisha. Maisha yamekuwa magumu na kadri siku zinavyokwenda ndivyo bei za bidhaa zinavyozidi kupaa.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa wananchi, kikwete anaendelea na utekelezaji na nadhiri aliyojiwekea ya kuvunja na kuweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza Duniani kutembelea nchi nyingi kama si zote ndani ya kipindi cha miaka kumi tu ya uongozi.

Juzi tu baada ya kutoka Switzerland alikotoa kauli ya kusisitiza umuhimu wa misaada, alirudi nchini na baadaye kidogo aliekea Uingereza. Hivi ninavyopost thread hii, yupo Botswana eti kwenye sherehe ya chama tawala. Akiwa kwenye safari hizo, tumeshuhudia wagonjwa wakifa kwa kukosa matibabu kutokana na mgomo wa madaktari, wananchi Songea wanauawa na polisi na karaha mbalimbali lakini yeye kwa raha zake anaendelea na safari na matanuzi yake.

Kwa mwenendo huu, sina budi kuamini kuwa Kikwete ni janga la kitaifa.
 
Akiwa kwenye safari hizo, tumeshuhudia wagonjwa wakifa kwa kukosa matibabu kutokana na mgomo wa madaktari, wananchi Songea wanauawa na polisi na karaha mbalimbali lakini yeye kwa raha zake anaendelea na safari na matanuzi yake
NA kinachosikitisha zaidi ni kuwa hajatoa kauli yoyote juu ya lolote kati ya hayo!
dR sLAA is some kind of a prophet and a long awaited herald!
 
Na hapo hujaongezea kwamba baadhi ya wafanyikazi serikalini hawajalipwa mishahara. Kikwete's government is broke.
 
Hadi 2015, tutashuhudia mengi, na baadhi yetu tunamlinda kwa hayo anayofanya! hatutaki kusikia anakosolewa. Kama rais, anayo majukumu ya kuhakikisha watendaji wake wanatumikia wananchi na taifa kwa ujumla. Kwa Mhe rais, yeye anapokaa kimya kwenye inshu zinazohusu maisha ya wananchi ka hii ya juzi Songea anazidi kutudhihirishia kuwa bado anazile elements za kujiona hahusiki kama alivyokuwa waziri wa mambo ya nje.
 
Yani leo ukimwambia mtu ulimpigia nani kura atasema CDM yani wanaruka wote kimanga!

Tangu awali hili janga kubwa lisilo na tiba ni MUNGU pekee akanyoshe mkono na kutunusuru.

Ila wote walioipigia kura hawa mafisadi yani jela ndiyo ingekuwa halali yao flu!
Ni mawazo yako tu...kila mtu amemchagua Kikwete pamoja na wewe pia! ”Kikwete ni Chaguo la Mungu” ~ mapadre, maaskofu, wachungaji!!!
 
Hamkuwaelewa walisema hivyo wakimaanisha ni chaguo la Mungu kuiua CCM na Mwl Nyerere aliposema babo mdogo hakumaanisha udogo wa umri haiwezekani mtu wa miaka 50 kuwa ni mtoto ila alimaanisha kuwa ni galasha kama mama anapokuagiza nazi unaenda unaleta Zaidi ya dafu na angaliu hata dafu unaweza kunywa maji lakini yeye haliki.

Tuje kwa wananchi hivi wale wanaume huwa wanapenda kukaa kwenye vijiwe vya kahawa na kupanga vikosi vya Madrid, man u, arsenal na stars siwatofautishi na huyo walio mchagua
 
Alikuwa chaguo la Mungu miaka ileee... Kwa sasa ni chaguo la mafisadi na mashetani.
 
Maisha yenu watanzania yataendelea kuwa kitendawili hadi mtakapoacha ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa! Dhiki na mahangaiko mnayataka wenyewe! Hakuna sababu ya kuilaumu serikali bali wananchi mjilaumu wenyewe. Kumbukeni hiyo serikali haikuingia msituni na kutwaa madaraka! Mlipiga kura kwa ushabiki wenu wenyewe! Ugumu wa maisha unaoendelea kwa sasa ni kwa ridhaa yenu wenyewe! Hayo ndiyo matokeo ya rushwa ya chumvi na vikofia vya kijani. Poleni sana!! Bila mang'amuzi, safari bado ni ndefu!
 
Mleta nadhani hujui kabisa kwa nini Kikwete anasafiri, upunguani wako wa muono na uhaba wako wa kusafiri unakufanya uone kuwa safari ni matanuzi.

Hivi, wewe unajuwa isingekuwa hizi safari leo ungekuwa katika dhiki mara 10 zaidi?

Hivi haya ma gesi yanayovumbuliwaa kila kukicha, haya matalii yanayozidi kila kukicha, haya mahoteli mpaka imefikia kuwa Tanzania ndio imetowa hoteli bora duniani, unafikiri inakuja tu yenyewe? hata bajeti yetu, ingawa kikwete kapunguzi sana utegemezi wa bajeti kutoka nje, lakini still tunahitaji kujazilia, mpaka hapo mambo yatapokuwa mazuri.

Tafadhali kama hauna cha kusema bora ukae kimya.

Kila siku huwa nasema humu, hebu tuchambuwe mambo muhimu tuone ni Rais yupi aliefanya zaidi ya Kikwete? nakuhakikishia huna hata moja.

Si bora Kikwete anakwenda kikazi, Mkapa alienda kupunguza unene Switzerland akaiacha ofisi zaidi mwezi. Kuna hata mmoja alinyanyua sauti aksema kwii.

Nyinyi mnajulikana chuki zenu kwa Kikwete ni kwa nini. Lakini kwa utendaji bora na uchapa kazi, nawapa challenge, hakuna aliyemfikia hata robo. Tusiandikie mate na woino upo.

Barabara? KM ngapi kwa awamu zote? KM ngapi kwa Kikwete? amma zimeshajengwa au mikataba imesha sainiwa.

Mtarusha hili kama kawaida yenu.
 
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili,Hapo ndipo akili za wabongo zipime na kugundua kuwa walifanya makosa kumchagua kikwete na CCM yake iunde serikali ya nchi hii.Maisha ni magumu kila kona wa2 wanalalamika,hili liwe fundisho kwe2 2sifanye makosa tena 2015 kwani kosa sio kosa bali kurudia kosa ni kosa.
 
Hamkuwaelewa walisema hivyo wakimaanisha ni chaguo la Mungu kuiua CCM na Mwl Nyerere aliposema babo mdogo hakumaanisha udogo wa umri haiwezekani mtu wa miaka 50 kuwa ni mtoto ila alimaanisha kuwa ni galasha kama mama anapokuagiza nazi unaenda unaleta Zaidi ya dafu na angaliu hata dafu unaweza kunywa maji lakini yeye haliki.

Tuje kwa wananchi hivi wale wanaume huwa wanapenda kukaa kwenye vijiwe vya kahawa na kupanga vikosi vya Madrid, man u, arsenal na stars siwatofautishi na huyo walio mchagua
Nyerere alitoa hicho kisingizio kutokana na udini. Kwa wakati ule alitaka Mkatoliki mwenzake aongoze nchi, ikabidi atumie udikteta kumweka Mkapa.

Kikwete katufanyia mengi mazuri sana. Mkuu wetu halali, anaihangaikia nchi, anasafiri huku na kule kututafutia sisi wananchi maisha bora. Baba mwenye nyumba siku zote ni mwangaikaji, hawezi kukaa tu nyumbani! Lazima akatafute!!
 
Wakuu,
Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 nilipata kuisikia kauli maarufu ya Dr. Slaa kuhusu madhara ambayo nchi hii ingepata endapo kikwete angechaguliwa mara nyingine tena. Dr. Slaa alisema kwamba kumchagua kikwete na ccm yake ni kukaribisha janga la kitaifa na wananchi watakuja kujutia uamuzi wao.

Leo hii, ikiwa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa, wananchi katika kila kona ya nchi wanalalamika ugumu wa maisha. Maisha yamekuwa magumu na kadri siku zinavyokwenda ndivyo bei za bidhaa zinavyozidi kupaa. Wakati hali ikiwa hivyo kwa wananchi, kikwete anaendelea na utekelezaji na nadhiri aliyojiwekea ya kuvunja na kuweka rekodi ya kuwa rais wa kwanza Duniani kutembelea nchi nyingi kama si zote ndani ya kipindi cha miaka kumi tu ya uongozi. Juzi tu baada ya kutoka Switzland alikotoa kauli ya kusisitiza umuhimu wa misaada, alirudi nchini na baadaye kidogo aliekea Uingereza. Hivi ninavyopost thread hii, yupo Botswana eti kwenye sherehe ya chama tawala. Akiwa kwenye safari hizo, tumeshuhudia wagonjwa wakifa kwa kukosa matibabu kutokana na mgomo wa madaktari, wananchi Songea wanauawa na polisi na karaha mbalimbali lakini yeye kwa raha zake anaendelea na safari na matanuzi yake.

Kwa mwenendo huu, sina budi kuamini kuwa kikwete ni janga la kitaifa.

Unashauri nini sasa kwa wapiga kura waliopiga kura na watakaopiga kura mwaka 2015?.
 
Mleta nadhani hujui kabisa kwa nini Kikwete anasafiri, upunguani wako wa muono na uhaba wako wa kusafiri unakufanya uone kuwa safari ni matanuzi.

Hivi, wewe unajuwa isingekuwa hizi safari leo ungekuwa katika dhiki mara 10 zaidi?

Hivi haya ma gesi yanayovumbuliwaa kila kukicha, haya matalii yanayozidi kila kukicha, haya mahoteli mpaka imefikia kuwa Tanzania ndio imetowa hoteli bora duniani, unafikiri inakuja tu yenyewe? hata bajeti yetu, ingawa kikwete kapunguzi sana utegemezi wa bajeti kutoka nje, lakini still tunahitaji kujazilia, mpaka hapo mambo yatapokuwa mazuri.

Tafadhali kama hauna cha kusema bora ukae kimya.

Kila siku huwa nasema humu, hebu tuchambuwe mambo muhimu tuone ni Rais yupi aliefanya zaidi ya Kikwete? nakuhakikishia huna hata moja.

Si bora Kikwete anakwenda kikazi, Mkapa alienda kupunguza unene Switzerland akaiacha ofisi zaidi mwezi. Kuna hata mmoja alinyanyua sauti aksema kwii.

Nyinyi mnajulikana chuki zenu kwa Kikwete ni kwa nini. Lakini kwa utendaji bora na uchapa kazi, nawapa challenge, hakuna aliyemfikia hata robo. Tusiandikie mate na woino upo.

Barabara? KM ngapi kwa awamu zote? KM ngapi kwa Kikwete? amma zimeshajengwa au mikataba imesha sainiwa.

Mtarusha hili kama kawaida yenu.
Well said mkuu
 
Hii dunia ina watu na mijitu. Virushwa vidofodogo kweli vinapofusha. Hivi wewe umepewa nini kiasi cha kuwa kipofu kiasi hiki cha kushindwa kuona kitu obvious namna hii kuwa Jk ameshindwa si kidogo bali kabisa! Nakushauri iwapo huna hoja kabisa ni heri unyamaze kwani hata watoto wanaona ugumu wa maisha kwa sababu ya kushindwa kwake na kuendekeza kuombaomba badala ya kujenga strategy ya kuitoa nchi kwenye mashimo. Botswana atarudi na chakula cha watoto wako? Nadhani na wewe ni ****** mwenzie mnaothamini ngoma na visherehe visivyo na mashiko. Pole yako
N
 
Mleta nadhani hujui kabisa kwa nini Kikwete anasafiri, upunguani wako wa muono na uhaba wako wa kusafiri unakufanya uone kuwa safari ni matanuzi.

Hivi, wewe unajuwa isingekuwa hizi safari leo ungekuwa katika dhiki mara 10 zaidi?

Hivi haya ma gesi yanayovumbuliwaa kila kukicha, haya matalii yanayozidi kila kukicha, haya mahoteli mpaka imefikia kuwa Tanzania ndio imetowa hoteli bora duniani, unafikiri inakuja tu yenyewe? hata bajeti yetu, ingawa kikwete kapunguzi sana utegemezi wa bajeti kutoka nje, lakini still tunahitaji kujazilia, mpaka hapo mambo yatapokuwa mazuri.

Tafadhali kama hauna cha kusema bora ukae kimya.

Kila siku huwa nasema humu, hebu tuchambuwe mambo muhimu tuone ni Rais yupi aliefanya zaidi ya Kikwete? nakuhakikishia huna hata moja.

Si bora Kikwete anakwenda kikazi, Mkapa alienda kupunguza unene Switzerland akaiacha ofisi zaidi mwezi. Kuna hata mmoja alinyanyua sauti aksema kwii.

Nyinyi mnajulikana chuki zenu kwa Kikwete ni kwa nini. Lakini kwa utendaji bora na uchapa kazi, nawapa challenge, hakuna aliyemfikia hata robo. Tusiandikie mate na woino upo.

Barabara? KM ngapi kwa awamu zote? KM ngapi kwa Kikwete? amma zimeshajengwa au mikataba imesha sainiwa.

Mtarusha hili kama kawaida yenu.

Mkubwa, unajua watanzania tunachanganya siasa na hali halisi ya maisha.Heri umemwambia ukweli.
 
Back
Top Bottom