Haki za mwanachama

Maswi

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
932
211
Haki za MwanaChama CHADEMA
Kila mwanachama ana haki ya:-
5.2.1 Kuchagua viongozi wa Chama wa ngazi anayohusika kwa mujibu wa katiba.
5.2.2 Kuchaguliwa kuongoza na kuwakilisha Chama katika ngazi yoyote kwa kuzingatia
masharti yaliyowekwa ya sifa za uongozi.
5.2.3 Kushiriki vikao vya Chama vinavyomhusu na kutoa mawazo yake kwa uhuru kwa
kuzingatia taratibu za vikao.
5.2.4 Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za
kinidhamu kicham
a.
5.3 Wajibu wa Mwanachama CHADEMA
5.3.1 Kushiriki kikamilifu katika vikao vinavyomhusu na katika shughuli nyingine za Chama
kadri atakavyotakiwa
5.3.2 Kuchangia gharama za uendeshaji Chama kwa njia ya ada ya Uanachama ya kila mwaka
na kwa michango mingineyo inayoamriwa na vikao vya Chama.

5.3.3 Kutetea na kueneza Itikadi, falsafa na madhumuni ya Chama ndani ya jamii anamoishi.
5.3.4 Kushirikiana na wanachama na viongozi wengine wote katika kutekeleza sera na mipango
ya Chama.Kuwa tayari kupambana na namna yoyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na
ubaguzi.


5.3.5 Kuwa tayari kupambana na namna yoyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na
ubaguzi.

TAFAKARI
 
Ni kweli kabisa, tupambane kadri tuwezavyo kuwashinda Hawa Mashoga wa Uingereza/Ufipa
 
Back
Top Bottom