Haki ya Uraia - Nani anaweza kuninyang'anya Uraia?

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Learned brothers...
Kuna maswali mbalimbali ningependa kuyaweka hapa kwa kusudi la kuyajadili na kupata mwangaza zaidi kuhusu hili swala zima la uraia. Hii imetokana hasa na debate kubwa iliyokuja baada ya mbunge kupigwa chini na kamati kuu ya ccm kwa madai ya kutokuwa raia!

1. Je ni haki/lazima kwa kila mwanadamu kuwa na uraia wa nchi fulani?
Natumia neno haki kwa sababu Uraia unakupa privileges mbalimbali kama ulinzi, uwezo wa kusafiri kwenda nchi nyingine, uwezo wa kupiga kura, nk. Hivi vyote vinakuja kama haki yako wa kuwa raia wa nchi fulani.

Lakini nadhani neno 'lazima' nalo lina nasafi yake. Najua kuwa nchi nyingi haziwezi kukufutia uraia kama matokea yake yatakufanya uwe 'stateless'.
Kwa mfano: Uingereza - Section 4 of the British Nationality, Immigration and Asylum Act 2002http://en.wikipedia.org/wiki/Denaturalization#cite_note-10 gave power to the Home Secretary to ‘deprive a person of a citizenship status if the Secretary of State is satisfied that the person has done anything seriously prejudicial to the vital interests’ of the United Kingdom etc, except in the case where such might render the person stateless.
Najua pia hii sio kwa Uingereza pekee bali nchi nyinge nyingi.

2. Je nchi ikikunyang'anya uraia, si lazima uondoke hiyo nchi au upate kibali kipya cha kuishi hapo?

3. Je ni haki kwa serikali kukunyang'anya uraia kama huna uraia wa sehemu nyingine?

Sasa katika kujibu haya maswali...jaribu ku-reconcile yote na story ya Kambona.
Tukiangalia historia ya Kambona, tunaona kuwa mnapo aliporudi Tanzania mwaka 1992, serikali ilimnyang'anya passport kwa madai ya kutokuwa Mtanzania. Je, walipomnyang'anya passport si iliwabudu kumfukuza nchini pia? Na kama walimpa kibali cha kuishi Tanzania, hicho kibali kiliwekwa kwenye nini? Maana chombo cha kubeba kibali cha kuishi nchi nyingine yeyote ni passport na hiyo waliichukua.
Pia, kama ivyo, angeweza kwenda nchi gani bila kibali cha kusafiri au ingembudu kujiita mkimbizi? Je Kambona na yeye alikuwa stateless? Je sheria ya Uraia Tanzania inasemaje kuhusu hili?

source: Oscar Kambona - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Mkuu umeuliza maswali ya msingi sana, labda tusubili tuone kama wataalamu wa sheria wataweza kutufafanulia kwa undani zaidi maana hata mimi nilikuwa najiuliza swali hili.

Learned brothers...
Kuna maswali mbalimbali ningependa kuyaweka hapa kwa kusudi la kuyajadili na kupata mwangaza zaidi kuhusu hili swala zima la uraia. Hii imetokana hasa na debate kubwa iliyokuja baada ya mbunge kupigwa chini na kamati kuu ya ccm kwa madai ya kutokuwa raia!

1. Je ni haki/lazima kwa kila mwanadamu kuwa na uraia wa nchi fulani?
Natumia neno haki kwa sababu Uraia unakupa privileges mbalimbali kama ulinzi, uwezo wa kusafiri kwenda nchi nyingine, uwezo wa kupiga kura, nk. Hivi vyote vinakuja kama haki yako wa kuwa raia wa nchi fulani.

Lakini nadhani neno 'lazima' nalo lina nasafi yake. Najua kuwa nchi nyingi haziwezi kukufutia uraia kama matokea yake yatakufanya uwe 'stateless'.
Kwa mfano: Uingereza - Section 4 of the British Nationality, Immigration and Asylum Act 2002http://en.wikipedia.org/wiki/Denaturalization#cite_note-10 gave power to the Home Secretary to ‘deprive a person of a citizenship status if the Secretary of State is satisfied that the person has done anything seriously prejudicial to the vital interests' of the United Kingdom etc, except in the case where such might render the person stateless.
Najua pia hii sio kwa Uingereza pekee bali nchi nyinge nyingi.

2. Je nchi ikikunyang'anya uraia, si lazima uondoke hiyo nchi au upate kibali kipya cha kuishi hapo?

3. Je ni haki kwa serikali kukunyang'anya uraia kama huna uraia wa sehemu nyingine?

Sasa katika kujibu haya maswali...jaribu ku-reconcile yote na story ya Kambona.
Tukiangalia historia ya Kambona, tunaona kuwa mnapo aliporudi Tanzania mwaka 1992, serikali ilimnyang'anya passport kwa madai ya kutokuwa Mtanzania. Je, walipomnyang'anya passport si iliwabudu kumfukuza nchini pia? Na kama walimpa kibali cha kuishi Tanzania, hicho kibali kiliwekwa kwenye nini? Maana chombo cha kubeba kibali cha kuishi nchi nyingine yeyote ni passport na hiyo waliichukua.
Pia, kama ivyo, angeweza kwenda nchi gani bila kibali cha kusafiri au ingembudu kujiita mkimbizi? Je Kambona na yeye alikuwa stateless? Je sheria ya Uraia Tanzania inasemaje kuhusu hili?

source: Oscar Kambona - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Tanzania tuna uraia wa aina tatu, raia wa Kuzaliwa, kuandikishwa na kurithi. Ukiwa ni raia wa kuzaliwa kamwe huwezi kunyang'anywa uraia kwa Tanzania kwa mujibu wa sheria No.8 ya 1995 ya Uraia Tanzania. Watu wanaoweza nyang'anywa ni wale wenye uraia wa kununua. Kama hujawahi kuwa Mtanzania na Unaishi kwa mishemishe tu, huwa mara nyingi unatangazwa kama si raia wa Tanzania na wala hunyang'anywi na hii ndio inawahanga wengi kwa historia ya Tanzania. Na mwenye nguvu na kukunyang'anya uraia mara nyingi Kamishna wa Uhamiaji kupitia waziri wake, ambaye kwa sasa ni waziri wa mambo ya ndani
 
Ninachofahamu kuna uraia wa aina mbili,yaani wa kuzaliwa na wa kujiandikisha sasa huo Uraia wa wa kurithi ukoje?tafadhali nijuze?
 
Kuna baadhi ya makosa ukiyatenda raisi wa nchi ana uwezo kukufukuza nchini /depotation, ila sijui kama unakuwa si raia wa tanzania tena manake akimaliza mda wake unaruhusiwa kurudi.
 
Tanzania tuna uraia wa aina tatu, raia wa Kuzaliwa, kuandikishwa na kurithi. Ukiwa ni raia wa kuzaliwa kamwe huwezi kunyang'anywa uraia kwa Tanzania kwa mujibu wa sheria No.8 ya 1995 ya Uraia Tanzania. Watu wanaoweza nyang'anywa ni wale wenye uraia wa kununua. Kama hujawahi kuwa Mtanzania na Unaishi kwa mishemishe tu, huwa mara nyingi unatangazwa kama si raia wa Tanzania na wala hunyang'anywi na hii ndio inawahanga wengi kwa historia ya Tanzania. Na mwenye nguvu na kukunyang'anya uraia mara nyingi Kamishna wa Uhamiaji kupitia waziri wake, ambaye kwa sasa ni waziri wa mambo ya ndani

na wa kurithi inakuwaje?
 
Kuna baadhi ya makosa ukiyatenda raisi wa nchi ana uwezo kukufukuza nchini /depotation, ila sijui kama unakuwa si raia wa tanzania tena manake akimaliza mda wake unaruhusiwa kurudi.

fafanua zaidi. Hili ndilo walilomfanya Kambona?
 
Back
Top Bottom