Haki nisaidieni hapa! Huyu binti yangu..............

Jambo wote JF,
Msichoke kusoma! Nahitaji msaada!
Ndugu naombeni msaada wenu. Wakati fulani huko miaka ya nyuma, niliwahi kuoa mdada mmoja mkenya. Tuliishi kwa miaka 7. Katika ndoa yetu ambayo haikuwahi kuwa na baraka za Paroko tulibahatika kupata mabinti 2. Wa kwanza alizaliwa 1990 na wa pili 1995. Tulikorofishana naye 1996. Kipato changu hakikuwa kinatosha. Nilikuwa najilipia shule na wakati huo huo kuhudumia familia. aliondoka na kurudi kwao kwa madai hakuzoea shida. Wakati huo nilikuwa naishi Dar. Aliondoka na watoto wote. Yule wa kwanza alipofika darasa la 7 akaleta ukorofi (kwa madai ya mama yake) ikabidi niende kwao Nairobi na kwa kuongea na binti ilibidi niondoke naye na kumtafutia shule huku. Alipata shule na sasa yuko high school. Shida sasa! Huyu mdogo naye kamaliza 8, hakupata alama za kutosha kujiunga na form 1. Mama yake kanipigia simu kuwa mtoto hakufanya vizuri. Tukakubaliana atafute shule huko na mimi nitafute atakayefanikiwa basi aende shule. Taarifa hizi ni tangu 28th Dec 10. Nilihangaika kwa kweli, sijui yeye kama alikuwa anahangaika! Last week nikapata shule fulani ya kanisa katoliki. Nikamwambia, kwanza hakutaka aende lakini baada ya kuhimiza sana akasema hana muda wa kumpeleka. Ikabidi nikatize safari yangu na kwenda NRB kumchukua. Nikampeleka shuleni na kwa bahati akafanya vizuri. Wale masista wa pale wakanambia nikalipe ada na ikifika J2 nihakikishe nampeleka mtoto shule. Nilikiwa njiani nikamjulisha huyu mama kuwa mtoto anatakiwa shule jumapili. Akaanza oooh ni mapema sana na mimi nilikuwa na mipango ya shule, mara sijui huyu mtoto kakulia kwenye maadili ya kiislamu umempeleka shule ya kikristu. Nilikasirika na kukata simu. Binti alikubali kusoma pale. Kesho yake nikampigia simu kuwa naenda kulipa ada akanung'unika sana mwisho akanambia sawa nenda kalipe. Nikaenda kulipa shs 1,438,000/= acha mahitaji mengine. Kumbe huku nyuma akampigia simu mtoto aombe kwenda kuchukua baadhi ya vitu vyake. Kwa nia njema kabisa nikamkubalia. Kufika jioni akanipigia simu kuwa amepata shule huko kenya na ada ni shs 55,000/= kwa muhula. Kwanza niliduwaa halafu nikamuuliza zile ambazo nimeshalipa inakuwaje? Alichonambia hiyo itabidi iwe hasara. Nikamwambia kuwa hayo ni masihara. Nilimtaka ahakikishe kuwa leo Jumamosi tarehe 22/1/11 kuwa mtoto anakuwa hapa kwangu ili nimpeleke shule Kesho. Niandikapo ujumbe huu SIJAONA HATA ALAMA YA HUYU BINTI YANGU KUJA. Na mbaya zaidi hata simu zao hazipatikani.
Nifanyeje jamani,,, shida sio hasara ila ile munkari alokuwa naye ya kusoma hapa kwetu Tanzania na ndoto alizokuwa nazo kwa kipindi kifupi nilichokaa nacho ndo kinanitesa. Jamani nisaidieni ushauri.

NDUGU yangu nakupa pongezi kwa kujali watoto wa ko bila kujali jinsia.nakupa pole kwa hayo masaibu.Swali langu kubwa kwako je,mtot wa kwanza alishawahi kurudi kwa mama yake tangu umemchukua? haujawahi kutoa vitisho vyovyote kwa huyu mama kuhusu watoto kuwa hutawarudisha kwake? tatu wewe hujaoa?/ Ushauri...mtume mtoto wako i mean dadake akamchukue mdogo wake lazima atakuja nae,pili mpe na barua ulioipokea ktukota shuleni ya kujiunga na hiyi shule ili mama apate kuamini na risiti ya malipo.

Uchungu wa mtoto aujua mzazi yawezekana anaogopauna mpango wa kuwatorosha watoto wote. Tusimlaumu huyu mama bila kujua upande wa pili wa shilingi ni sawa na kuhukumu mtu bila kumsikiliza.naamini kilajambo lawezekana.

Kama pia kampatia shule nzuri huko NRB usisite we mlipie na kwa wale masista watakurudishia hela zako kama binti hatakuja.
 
:shock:pole Sana Mangi,

Hili ni gumu,natamani tungesikia na upande wa pili then tungeweza shauri zaidi.

Ushauri wangu: Tafuta namna ujue kama kweli mwanao amepata shule,kwakuwa simu haipatikani,nafikiri unajua wanapoishi,omba nguvu,ujasiri na ulinzi wa Mungu manake hao wa Kenya sio,kwanini asipatikane kwa simu,isije kuwa ana njama zake.....

Funga safari,kazungumze na mama watoto wako na tembelea shule ya mtoto na uzungumze nae,anaionaje shule na kama anafurahia,akisema hafurahii,muulize kama kuna shule anayofahamu ambayo angependa kusoma ambayo ni nzuri zaidi ya hiyo,nenda angalia na lipia ada mwenyewe bila kupitia kwa huyo mama,as ameshakufanya mradi wa hela.Mwambie ada ya mwanao nitalipa mengine kazi kwako,jukumu la kulea ni lenu sote.......kama shule aliyopelekwa na mama yake ni nzuri,mlipie ada,muache asome na mama alipie matumizi yaliyobaki,hawezi au hataki,mtoto aje Tanzania......

Nafikiri kwa namna hiyo utakuwa umemsaidia mwanao ambaye nafikiri ndo muhimu zaidi kutokana na tabia za huyo mama
Whatever decision you take,usimuumize mtoto,hastahili hayo,mwenye shida ni mama.Mungu akutangulie....Kutire Mbe!!!
 
Inawezekana ni kweli maana na bro wangu ameoa huko naona yaliyosemwa yote yana ukweli. Okay Tumshauri mwenzetu tuachane na Roho mbaya zao.
Unamfahamu mwanamke wa kikenya aliyebahatika kulazimisha ndoa na mtz? Kama hayajakukuta basi fanya utafiti bwana. Hawana mapenzi ya ngono Bali ya mali. Akishaolewa anawaunganisha ndugu na rafiki zake kuja tz kutafuta kazi na maslahi. Wengi hujifanya ni wajaluo wa tz, hufoji vyeti vya kuzaliwa na kuchukua Pasport za tz haraka.

Wapo wengi mno, serikali yetu inachekacheka tu
 
Pole sana Mkuu, huyo dada hamtakii mema mwanenu na anamtumia binti yenu ili kufaidika toka kwako kwa namna moja au nyingine, labda atakuja kukwambia anachokitaka toka kwako.
 
Pole mkuu. Nenda NRB mkayamalize maana kwa hatua hii cm itachelesha suluhu. Ukifika huko ajenda kuu iwe ni 1 tu-maisha bora ya binti yenu yasiathiriwe na tofauti zenu.
 
inapofikia issue ya mtoto kuzuiwa kupata elimu roho inaniuma saana tu hasira zimenipanda tayari natamani nikuchangie nauli ukamchukue mwanao asome. sasa hivi elimu ni kitu cha maana saaaana. dah pole mkuu ngoja hasira zishuke kwanza.

m
a
 
Wakenya Wana roho za kinyama sana, labda kutokana na maisha yao ya kikatili. Wengi sana wanaolewa tz ili wapate kupata ajira au maisha mazuri na siyo mapenzi. Nadhani alipoona mambo yako hayajatulia kwa wakati huo akaona siyo bahati yake. Inawezekana kitendo cha hali yako kuimarika sasa anataka kurejea. Amegundua akiachia watoto wote uwezekano wa kurudi haupo. Hebu jaribu kumwita aje na mtoto uone.

Pole pia

mtoa mada pole sana, vilevile huu ushauri wa Gurudumu jaribu kuutafakari just 4 a minute
 
kwani huyo dada ni muislamu kama ndio inaonesha mlikuwa mnatunishiana misuli ya kiutamaduni a.k.a. kidini, stori ya kumwaga ugali na mboga, kama mama amekubali hivyo muachie kwa gharama zake na ukubali hiyo hasara.
 
pole sana mtoa mada, ila jaribu kufuatilia ukweli halisi kwa kwenda kule nrb. Manake waweza kukaa huku na kuendelea kunung'unika na pia kumsababishia mtoto matatizo, kama shule ipo kule nrb basi lipia asome huko, na pia katika suala la kulea mtoto mwambie huyo aliyekuwa mkeo inabidi tofauti ziwekwe kando, na wote muwe na lengo moja tu la kumsaidia mtoto. Lakini nakuambia ukweli utajulikana tu kama anazuga au vipi?

Pili muombe Mungu akusaidie kutuliza hasira zako ili hili suala mlitatue kwa amani pande zote mbili na muafaka uwe ni wa kujenga maisha ya binti.
 
Pole sana mkuu
Nakuonea huruma kukutana na huyo mzazi mwenzio asiyethamini shule na pia asiyeona jitihada zako za hali na mali, jaribu kumtafuta ndugu yako yeyote wa kike mfunge safari akaongee nae.

Ujulishe uongozi wa shule juu ya delay ya mtoto, ukifanikiwa usifanye kosa la kuwaacha tena mpaka wamalize shule
akitaka kuwaona aje kuwasalimu kwako wakati wa likizo hata nauli mtumie.

Kila la heri
 
Duh!
Pole sana.
Mama anaogopa kuwaacha watoto wake wote mikononi mwako. Sijui kama mlivyogombana akaondoka na watoto ulikuwa ukiwahudumia,
ushauri;

kuwa mnyenyekevu na umsikilize anavyotaka juu ya elimu ya mtoto wenu maana hadi sasa ameshikilia madaraka, kama vipi muache mtoto asome kenya si unajua tena hii elimu yetu ya kibongobongo ilivyo.

Mwisho wahadithie uongozi wa shule maswahibu yaliyokukuta. Ikiwezekana urudushiwe nusu hasara. Au samehe sababu pesa inatafutwa na inawezekana thamani ya elimu atakayoipata huko ni kubwa kuliko hiyo millioni uliyoitoa.
 
Jambo wote JF,
Msichoke kusoma! Nahitaji msaada!
Ndugu naombeni msaada wenu. Wakati fulani huko miaka ya nyuma, niliwahi kuoa mdada mmoja mkenya. Tuliishi kwa miaka 7.

Katika ndoa yetu ambayo haikuwahi kuwa na baraka za Paroko tulibahatika kupata mabinti 2. Wa kwanza alizaliwa 1990 na wa pili 1995. Tulikorofishana naye 1996. Kipato changu hakikuwa kinatosha. Nilikuwa najilipia shule na wakati huo huo kuhudumia familia. aliondoka na kurudi kwao kwa madai hakuzoea shida. Wakati huo nilikuwa naishi Dar.

Aliondoka na watoto wote. Yule wa kwanza alipofika darasa la 7 akaleta ukorofi (kwa madai ya mama yake) ikabidi niende kwao Nairobi na kwa kuongea na binti ilibidi niondoke naye na kumtafutia shule huku. Alipata shule na sasa yuko high school. Shida sasa! Huyu mdogo naye kamaliza 8, hakupata alama za kutosha kujiunga na form 1. Mama yake kanipigia simu kuwa mtoto hakufanya vizuri. Tukakubaliana atafute shule huko na mimi nitafute atakayefanikiwa basi aende shule. Taarifa hizi ni tangu 28th Dec 10.

Nilihangaika kwa kweli, sijui yeye kama alikuwa anahangaika! Last week nikapata shule fulani ya kanisa katoliki. Nikamwambia, kwanza hakutaka aende lakini baada ya kuhimiza sana akasema hana muda wa kumpeleka. Ikabidi nikatize safari yangu na kwenda NRB kumchukua. Nikampeleka shuleni na kwa bahati akafanya vizuri. Wale masista wa pale wakanambia nikalipe ada na ikifika J2 nihakikishe nampeleka mtoto shule. Nilikiwa njiani nikamjulisha huyu mama kuwa mtoto anatakiwa shule jumapili.

Akaanza oooh ni mapema sana na mimi nilikuwa na mipango ya shule, mara sijui huyu mtoto kakulia kwenye maadili ya kiislamu umempeleka shule ya kikristu. Nilikasirika na kukata simu. Binti alikubali kusoma pale. Kesho yake nikampigia simu kuwa naenda kulipa ada akanung'unika sana mwisho akanambia sawa nenda kalipe. Nikaenda kulipa shs 1,438,000/= acha mahitaji mengine. Kumbe huku nyuma akampigia simu mtoto aombe kwenda kuchukua baadhi ya vitu vyake. Kwa nia njema kabisa nikamkubalia.

Kufika jioni akanipigia simu kuwa amepata shule huko kenya na ada ni shs 55,000/= kwa muhula. Kwanza niliduwaa halafu nikamuuliza zile ambazo nimeshalipa inakuwaje? Alichonambia hiyo itabidi iwe hasara. Nikamwambia kuwa hayo ni masihara. Nilimtaka ahakikishe kuwa leo Jumamosi tarehe 22/1/11 kuwa mtoto anakuwa hapa kwangu ili nimpeleke shule Kesho. Niandikapo ujumbe huu SIJAONA HATA ALAMA YA HUYU BINTI YANGU KUJA. Na mbaya zaidi hata simu zao hazipatikani.

Nifanyeje jamani,,, shida sio hasara ila ile munkari alokuwa naye ya kusoma hapa kwetu Tanzania na ndoto alizokuwa nazo kwa kipindi kifupi nilichokaa nacho ndo kinanitesa. Jamani nisaidieni ushauri.


kaka pole sana kimsingi hao watoto wako watakuja wenyewe, kama watataka kuishi bongo, katika umri wa miaka 18 waje kwa hiari yao, huwezi kuwalazisha kumbuka wana uraia wa mama kenya, na watanzania pia, najua hawataki bongo huku longolongo kibao pole
 
Wadau nashukuru sana kwa msaada wenu. Nilipoposti hii thread nilikuwa nimeongea pia na rafiki yangu tuliyesoma naye. Ni zaidi ya ndugu! Alifika Moshi akitokea Dar mida ya saa 3 usiku kwa ajili ya ushauri na kufanya maamuzi. Ilipofika saa 6 usiku tulikubaliana na kuamua.

Mimi, Rafiki yangu na wake zetu tuliamua kwenda NRB. Pia tuliongozana na binti yangu mkubwa ambaye anapajua anakoishi mama yake. Tuliondoka kwenye saa 8 usiku. Saa tano asubuhi tulikuwa nrb. Tulifika pale kwa bibiye mida ya saa 6 hivi na tulimkuta na huyo binti mdogo. Tulijadiliana kwa kina sana na ilielekea hakuwa amepata shule tayari. Ilibidi tumtumie binti yangu mkubwa aongee na huyo mdogo na kujua anachotaka.

Ikumbukwe kuwa katikati ya wiki iliyopita huyu mdogo alikuja Tanzania na alifanya mtihani wa majaribio na kufaulu vizuri. Majibu aliyotoa binti mdogo ni kuwa yeye anataka kusoma Tanzania na sio kenya. Alitoa sababu nyingi zikiwemo kuwa yeye amekuwa kaiishi na Bibi yake mzaa mama bila mapenzi ya baba na mama hivyo anataka akae na baba yake pia. Mama yake alishikwa na mshangao na kumuuliza Li (jina la mtoto ni Li) unanigeuka sasa?

Binti alimwambia nitakuwa nakuja kukusalimia kama dada ajavyo. Ilibidi aseme ukweli kuwa ni kwa msukumo wa wazazi wake ndo akalazimika kukataa Li kuja Tanzania eti atakosa watoto wote. Ilibidi tukubaliane twende hadi Wundanyi huko kwa bibi na babu yake Li tukiwa na mama yake Li na Li mwenyewe. Tulifika usiku sana. Tukasubiri hadi kukuche.

Saa 12 asubuhi hodi! Tukaanza majadiliano, haikufika saa 2 asubuhi tuakapata go ahead! Tukashukuru mara na kuja Tanzania leo leo. Kwa kuwa kila kitu kilikuwa tayari tulipitia Hospitali pale Mawenzi na kujaza medical report. Tukarudi kubadilisha nguo na kuelekea shule kule Same. Leo saa 10 jioni nilimkabidhi Li kwa Sister mkuu wa shule na ameanza kidato cha kwanza kwa furaha sana.

Nimeona sio vyema kutokuwajuza kilichojiri ndugu zangu wa JF.
Ninawashukuru sana kwa maoni, ushauri, nasaha na michango yenu. Mmekuwa wakarimu sana kwangu na kwa hilo sina budi kuwashukuru sana. Niwahakikishie wote kuwa hakuna mahala popote nimesema kuwa Li na dada yake hawatoenda kumjulia hali mama yao.

Huo ndio msimamo wetu na mke wangu. Dada yake Li huwa anaenda mara kwa mara akipata nafasi ama akiwa likizo. Mke wangu hana shida na hawa watoto hata kidogo. Ni hisia zangu kuwa ninahitajika sana kuhakikisha watoto wangu wanapata elimu bora na sio bora elimu.

Nashukuru kuwa wameelewa na wamekubaliana na sisi.
Nirudie tena kusema asante sana na Mungu awabariki sana.

Ndugu yenu
Eeka Mangi
 
Hongera sana mkuu,am very happy kwa kufanikiwa kutatua tatizo lako kwa njia ya maelewano na ex wife wako. Mungu amsaidie li asome kwa bidii na afaulu.
 
Back
Top Bottom