Haki na usawa tanzania

KAPONGO

JF-Expert Member
May 29, 2009
1,661
668

Kila ninapomaizi kuhusu mstakabali wa Tanzania, naona ukungu wa kiza katika mambo mengi kama Watanzania wenyewe hawajaamka na kuchukua hatua za maksudi za kuinusuru hatma na mustakabali wa nchi.

Chukulia mfano mdogo wa haki na wajibu wa msingi ya kila raia mwema katika nchi inayozingatia utawala wa demokrasia na sheria - wajibu wa kulipa kodi: Wigo wa ukusanyaji kodi unawabana zaidi wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi ambapo malipo ya Lipa Kadri unavyopata (PAYE) zinafilisi kipato chao cha kila mwisho wa mwezi, wakati hakuna jitihada madhubuti za kutanua wigo huo kwa sekta zisizo rasmi. Kinachokera zaidi na kusikitisha ni msamaha ya kodi ya mishahara na marupurupu ya Wabunge. Wao kwa kuwa ndo wameingizwa mjengoni kutunga sheria, huwa mstari wa mbele sana kupitisha sheria zenye maslahi yao. Kama kulipa kodi ni muhimu kwa nini wao wasiwe mfano kwa waliowachagua!! hivi sasa tumeambiwa kuwa mikopo ya mashangingi kwa waheshimiwa hao imeshatolewa- milioni 90!! lakini taarifa zinasema kiukweli anacholipia mbunge mwisho wa siku ni nusu tu ya fedha alizokopeshwa kwa maelezo kuwa nusu nyingine serikali inawalipia kwa kutambua mchango wao wa kusukuma maendeleo(sic!): Cha kujiuliza vipi madiwani ambao wapo karibu zaidi na wananchi nao hawanastahili hiyo?, watumishi wa sekta nyeti za umma je?.

Kwa sababu hiyo kuna umuhimu wa kuwa na mfumo wa check-and balance usiotoa mwanya kwa chombo kimoja cha dola kuamua kujinufaisha bila kwanza kupitiwa na kupitishwa na chombo kingine huru, ili tufike mahali tuone haki si tu ikizingatiwa bali tuone ikitendeka...ili matukio kama ya kupitisha mishahara minono bila kujali sekta nyingine za umma yasijitokeze tena..ama mahakama ichelee kutoa dhamana kwa mahakimu na majaji wanaokabiliwa na kesi kama za mauaji ambazo tumekuwa tukiambiwa kwa siku nyingi kuwa hazina dhamana lakini hivi sasa tunashuhudia waheshimiwa wakipewa dhamana wakati wengine wananyimwa.
 
Back
Top Bottom