jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,558
- 25,322
Swali langu tufanye nini na watu hawa ambao tunao ndani ya jumuiya zetu? Kama Sheria ya nchi na katiba zinawalinda na tunachosuta ni hisia ambazo haziwezi kuwafunga kutokana na kulindwa na sheria, vinginevyo badili sheria.
Binafsi nasikia kichefuchefu kabisa wayafanyayo, lakini wao ni binadamu wanaostahili haki zao. Nimewahi kufanya kazi pamoja nao nchi za nje, hasa lesbians, sijaona ubaya wao kwa jamii au kikazi. Ni watu wazuri kufanya nao kazi kuliko wengine ambao ni wasumbufu sana katika mambo ya kujamihiana kazini.
Lesbians wako safi kushirikiana nao unajisikia kama uko na mwanaume mwenzako, na hawataki kuguswa kwa mambo ya kipuzi na wanajisikia kama wako huru bila kuleta mtafaruku kwa watu. Wengi wao wanafanya kwenye nafasi nyeti zao, so wote waonyeshao hadharani.
Sikubaliani na mtindo wao ulio kinyume cha maumbile na mpango mzima wa Muumba wetu kushirikisha uumbaji. Lakini tufanyeje na watu hawa wakati sheria inawalinda?
Hizo sheria zitakuwa zimetungwa na ccm. tuipige chini, tuzifute hizo sheria ovo, tena tusiogopeshwe na ugumu wa kuitenda kazi hiyo.