Haka ndiko kabinti kangu...

HONGERA sana kwa ukaribu uliouweka na mwanao,
POLE kwa yote yaliyotokea kwa mwanao,
Ila mkeo hakutakiwa kuchukua hatua ya kumpiga mwanao ksb,
Hiyo hatua itamfanya aone kama kuna ukuta kati ya wazazi wake na yeye,
Jambo ambalo siyo zuri, Nadhani ukikaa na kumwelesha mkeo,
hatorudia tena kumnyamazisha mtoto pindi anapotaka kujua taarifa fulani,
au kutoa taarifa fulani.

Nina HASIRA na huyo fataki, mwaribifu wa watoto wetu,
Mfuate mwambie ushenzi anaoufanya unaufahamu,
na mpe tahadhari ya kumliport polisi pindi asipojirekebisha,
na ikiwezekana toa taarifa mpaka serikali za mtaa,
hii pia itasidia kuweza kumfatilia zaidi hata wazazi wengine,
na kumwonesha kuwa ushenzi na unyama wake umejulikana.

Huyo mtoto tafuteni muda wa kukaa naye, tumie lugha nyepesi inayoendana na umri wake,
atakayoweza kuielewa kuhusu mambo ya hatarishi kwake,
na kumwomba na kumsisitiza kuwa nyinyi wazaze wake ndiyo,
rafiki wake wa kwanza na wengine ndiyo wanafuatia, kila jambo lake,
nyie ndiyo muwe wa watu kwanza kulifahamu.

POLE SANA NDUGU YANGU, HATA SIJUI WALIMWENGU TUNAUTAKIA NINI HUU ULIMWENGU WETU.
HATARI KWA WATOTO WETU NI ZAIDI YA TUNAZOZIONA NA KUZISIKIA.
 
Na hawaeleweki kwa kweli ( ila sio wote). Yaan kuna wengine wameumbwa akili wakaziacha huko huko! Hawanaga uso wa haya wala aibu. Huruma kwao ni mwiko
Mwanaume mwenzenu huyo.............
Usijekuta hata rafiki/ndugu ya mtu hapa wa karibu..................
Mi hapa ndo huwa siwaelewagi viumbe wanaoitwa wanaume duniani.
 
hyo dawa yake mtego akimuita tu yan unamtia displine ya kutosha mpk aone noma
 
Kuna mdau hapa majuzi alikuwa anaulizia upatikanaji na umiliki wa bunduki, nadhani ungechek nae.
 
Niko njia natoka polisi kufungua RB Na. Mzn/RB/0001/2011 'SHAMBULIO LA AIBU' usiue ngoja tumkamate tumpeleke kituoni! hafai kwenye jamii yoyote.
 
Pole sana inasikitisha na kuudhi sana, wenzangu wameshachangia vya kutosha sina haja ya kusema mengi, ila usimruhusu huyo mbuzi akuharibie mwanao, hivi hajui uchungu wa mwana huyo eeeh, angefanyiwa mwanae angekubali, you must face him na uhakikishe unamuumbua mbele za watu, hakun ustaarabu hapo. Pole sana mkuu
 
Ni kweli unaweza kukuta hapo mtaani anayo tabia hiyo na siyo kwa mtoto wako peke yake bali ni watoto wengi hapo mtaani.

Mpongeze mtoto wako kwa ujasiri aliyoonyesha kukueleza ukweli na umpe moyo kwa kufanya hivyo kwani ameweza kujiepusha na mengi.

Ila huyo mzee lazima mumkabili na mumueleze ukweli. Ingefaa ukapata na wazee wawili watatu ambao wanao watoto na wao wakawauliza kama amewafanyia hivyo. MUSIMUWACHE HIVI HIVI TU WALA KUWEKA TAREHE YA KUMVIZIA FATAKI HUYO.

Tulikuwa na jirani yetu wa aina hiyo lakini yeye alikuwa anataka kuwaharibu vijana wa kiume. Siku moja mmoja akasema mbele ya wazee wake (kama huyo wako). Baada ya kufanya uchunguzi kumbe alishawaita vijana wengi pale mtaani na kutaka kuwafanyia uchafu huo.

Tuliamua kumfukuza mtaani hapo (enzi zile hakukuwa na kuripoti polisi).
 
hilo baba limenifanya nifyonze mwenyewe,mwondolee uvivu na umwambie aache tabia chafu la sivyo mchukulie hatua za kisheria
 
Yani aisee kitoto cha miaka tisa kinaweza kukujia na mimba ya nyangau mzee ati.
Sasa jamani tusiwatume hata dukani, dah.................

Ningekua na uwzo ningehamisha wanaume kwenye sayari nyingine...........
Wawe wanakuja huku kwa sababu maalumu tu.

Yaani ukiwahamisha wanaume wanawake wenzio watakushuhulikia. Kuna wanawake ambao hawawezi kupita siku mbili bila hiyo huduma!
 
Nimewahi kukutwa na mkasa unaofanana kidogo na wa binti yako. Nikiwa na umri wa 6-7 yrs niliishi nyumba ina fundi cherehani akifanyia kazi zake barazani. Alikuwa na mazoea ya kuniita ananiambia nimuangalie, nikiacha ananiambia tena, tena... Sikujua kwanini alifanya hivyo. Baadae tukahama pale, miaka ikasogea, nikawa binti ninaejitambua hapo ndipo nikagundua pamoja na kuambiwa 'nina sexy eyes' ndipo nikaja kukumbuka na kuelewa y fundi alikuwa ananilazimisha niwe namuangalia. Nikajua alini2mia kuifurahisha nafsi yake pasipo mimi kujua. Kwa kuwa sikuwahi kumwambia mtu yeyote sikuwa na wa kumlaumu, hvi sasa nina 28yrs, baba yangu amerudi kuishi kwenye makazi yale, 2my suprise nilipoenda kumsabahi baba yule fundi yupo na kazi yake nyumba ya jirani. The 1st day nimeambiwa na baba kuwa ndie yule fundi aliyekuwa kwenye nyumba yetu nilipata hasira, nikakumbuka aliyoyafanya nikatamani nikam2kane kumaliza hasira zangu ila nikajizuia, sijawahi kumsalimu hata nikimuona nakwazika sana. Nakushauri uongee na mtoto wako umueleze ukweli, kwani atakapopata akili ya kujua ubaya wa hilo jambo, na kukumbuka alikueleza na hukumpa msaada, atakuwa so disapointed on u.
 
Khaaaaaaaa!!Mizee mingine hovyo kweli!!Embu fanya ukaongee nae umwambie ukisikia tena hata amepokea salamu ya mtoto wako aandae polisi kabisa!!

Alafu hukuwahi kumkanya mtoto asiwe anafuatana na mtu yeyote hata jirani yenu bila ruhusa yako???Fanya uongee nae na umwambie kwanzia leo hata mtu akimtania kidogo tu akujulishe.Ukifanya mchezo utaletewe mjukuu bila kutarajia!!!
 
Yeeeeeeesu, nimeumia sana jamani nini iki? jamani kaka pls pls usimcheleweshe uyo mzee maana atatuaribia mtoto jamani, just go strait umpe onyo na hakika hatorudia tena. Pili naomba uongee na mama(mkeo) mwambie awe mpole na amwelekeze mtoto masuala mazima ya mapenzi yaani madhara na asiingie ndani sana ila amwelekeze yale muhimu na yakumkinga na adui `FATAKI"
NAPATA UCHUNGU sababu mimi ni mzazi na mtoto wa kike, pia wana jamii pia tuwe na tabia yakuwalinda watoto maana watoto ni wetu sote na si wa mmoja aliye mzaa.
Pls nenda kwa uyo FTK
 
Yani aisee kitoto cha miaka tisa kinaweza kukujia na mimba ya nyangau mzee ati.
Sasa jamani tusiwatume hata dukani, dah.................

Ningekua na uwzo ningehamisha wanaume kwenye sayari nyingine...........
Wawe wanakuja huku kwa sababu maalumu tu.
teh teh! Nimependa sana hii.
 
Inasikitisha sana jamani hii dunia imekuwa ya ajabu sana. Wazazi jamani inabidi kuvunja ukimya na kuanza kuongea na watoto wetu kuanzia wakiwa wadogo. Mtoto anatakiwa afundishwe sehemu zake za siri kuwa ni private kuanzia umri anapoanza kuongea,ajue kujihifadhi na kutomruhusu mtu kuzishika.
Hapa home tuna katoto ka kiume ana 3 na nusu hakubali hata mdogo wake wa two years amwone anapovua nguo na hakubali kushikwa na mtu zaidi ya muda anaoogeshwa tu. Amefundishwa kiasi kwamba mtu akimshika tu hata kwa utani basi anaripoti mara moja.

Wazazi tujitahid tuwalinde watoto wetu na hawa mabazazi. Pole sana mkuu.
 
Ni PM nije nikusaidie kuongea tena ki-utu uzima wala hakuna AK 47 wala mashine gun nitakuja nayo. Nakuna na Biiblia yangu. Maneno nitakayompa nafikiri presha itamuondoa.

Wahi haraka kabla mtoto hajaharibiwa Ikiwezekana hama kama ni nyumba ya kupanga, kama yako basi weka geti na makufuli ya SOLEX.
 
Ni PM nije nikusaidie kuongea tena ki-utu uzima wala hakuna AK 47 wala mashine gun nitakuja nayo. Nakuna na Biiblia yangu. Maneno nitakayompa nafikiri presha itamuondoa.

Wahi haraka kabla mtoto hajaharibiwa Ikiwezekana hama kama ni nyumba ya kupanga, kama yako basi weka geti na makufuli ya SOLEX.

kwenye red,pia nasi wazazi kuna wakati tunajisahau mtoto anacheza na kuzurura(zagaa)bila hata kutumwa utamkuta mtaa wa pili,
michezo ndo imenoga kwa mtu kama fataki inakuwa kwake rahisi kumrubuni tuwachunge watoto wetu jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom