Haka katabia kananikeraga sana.

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,044
1,999
Unakuta umeenda kwenye show ya msanii flan na mpenzi wako,cha kushangaza huyo mpz wako anajifanya anaenda kumtuza huyo msanii afu anamkatikia mauno as if wanajuana..inanikeraga sana hii tabia.
 
Na huwa wanawatunza hela zenye number za simu. Kama mwanamke wako mcharuko mwambie akupe wewe hiyo hela ukamtunze.
 
Acha kwenda naye manake kila ukienda naye utakuwa unaboreka tu.
 
Mi niliona concert ya Fally ile ya kwanza hadi nikakata tamaa yaani, ilibidi nibadili channel. Wanawake wanamkatikia alafu na yeye anawachezea kwa dharau sana... cha kushangaza wana watu wao pale pale, wengine unaona mtu wake anamkataza kupanda, jukwaani, anamvuta mkono ila Fally anamwita basi dada anamsukuma mtu wake na kumkimbilia fally! hadi huruma nakwambia...
 
Ni kweli!

Kuna show flani nilifanya Nairobi, kuna waifu wa mtu alijisahau akaomba denda kabisa yaani wakati nampatia kuna njemba ikaharibu show.
 
Mi niliona concert ya Fally ile ya kwanza hadi nikakata tamaa yaani, ilibidi nibadili channel. Wanawake wanamkatikia alafu na yeye anawachezea kwa dharau sana... cha kushangaza wana watu wao pale pale, wengine unaona mtu wake anamkataza kupanda, jukwaani, anamvuta mkono ila Fally anamwita basi dada anamsukuma mtu wake na kumkimbilia fally! hadi huruma nakwambia...

kuna watu hawajiheshimu kwakweli. Ni raha zao lakini huwa wananiudhi kweli, hawana staha hata kwa wenzi wao!!!
 
Kua mnakatikiana wenyewe makwenu ili wasidate na viuno vya wasanii. Sio watu hata kwenda na wenzenu disco hamwezi wakati mnajua fika wanapenda sana kukata mauno.
 
sasa kinachokufanya uende nae kwny show za waranii ni nini wakat unajua kabisa hupend tabia kama hzo
 
Mi huwa najiuliza sana kama wanadamu tunajitambua!Sijapata jibu kabisa!
 
Mi najitambua lakini siwezi kabisa kujizuia kupanda jukwaani na kukata hadi chini. Tena msanii akinipeti peti ndo mzuka unanipaisha.

Mi huwa najiuliza sana kama wanadamu tunajitambua!Sijapata jibu kabisa!
 
Wa kwangu nilishampa misimamo yangu na huwa hafanyi ujinga huo. Mueleze kwamba huipendi hiyo tabia, kama ni mke bora atakuelewa.
 
unakwenda nae wa nn?? mwache home akae na watoto,kama hamna watoo acha alale mwenyewe mpka utakaporudi.
Hio yaonyesha huna sauti kwako hadi huwezi mpa amri mwenzi wako ala!!!
 
Unakuta umeenda kwenye show ya msanii flan na mpenzi wako,cha kushangaza huyo mpz wako anajifanya anaenda kumtuza huyo msanii afu anamkatikia mauno as if wanajuana..inanikeraga sana hii tabia.

Labda wanajuana.
 
Unakuta umeenda kwenye show ya msanii flan na mpenzi wako,cha kushangaza huyo mpz wako anajifanya anaenda kumtuza huyo msanii afu anamkatikia mauno as if wanajuana..inanikeraga sana hii tabia.

Yaani kama vile wanaume wanavyo enda kuwatunza wacheza shoo kwa kuwawekea pesa kwenye boobs na kile kimfereji; wanankera sana!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom