Haji Ramadhan, maamuzi yako yanahitaji pongezi za dhati!!!

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Jana majira ya saa tatu unusu nikiwa najifanyia kazi zangu kwenye laptop, huku nikipitisha macho kwenye TV, ghafla nikaona kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV na kuongozwa Salama Jabir, kikianza na mhojiwa akiwa Haji Ramadhan.

Baada ya Mazungumzo ya muda fulani, Salama alimuuliza Haji kuwa kuna tetesi kuwa alipokuwa yupo kambini kwenye BSS, Mkewe Haji alipata mimba isiyo ya mumewe, Je hbr hizo zina ukweli? Haji alijibu kuwa habari hizo ni za kweli kuwa mkewe alishika mimba ya mwanaume mwingine yeye akiwa kambini Dar kwenye BSS, na hivi sasa amemsamehe mkewe na analea huyo mtoto asiye wake pamoja na watoto wake 2 wa kuzaa!

Sababu kubwa ya kumsamehe mkewe ni kuwa hakupenda watoto wake waje waishi maisha ya taabu bila mapenzi ya mama yao au kulelewa na mama mwingine. Kwa maana hiyo alikuwa tayari kusamehe yote kwa faida ya maisha ya baada ya wanawe.

Nini cha kujifunza?
Hatma ya ndoa ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe. Ni vyema kusameheana kwa makosa tunayofanyia ndani ya ndoa ili kunusuru maisha ya baadaye ya watoto wetu. Kama wanaume wote tungekuwa na huruma na upendo mwingi kama wa ndugu yangu Haji (Maana hata mimi HorsePower sijui kama nigeweza kusamehe, loh!), watoto wa mitaani wasingelikuwepo kabisa, maana isingekuwa taabu mtu kulea mtoto wa mwenzie, na pia kila baba angeweza kuwajibika kwa watoto wake.

Hongera sana Haji, umeonyesha ni namna gani umeweza kuwa baba unayetanguliza upendo wa familia mbele zaidi kuliko mambo mengine. Nashauri kwa kila mwenye MOYO wa AINA hii, aweze kusamehe kwa faida ya familia. Pia wadada msibwete na kuanza kuzaa hovyo nje mkijuwa kuwa mtasamehewa, acheni, mtakutana na akina HP watawapiga talaka bila hata kuangalia nyuma!

Swali kwa Wana JF?
Je, ungelikuwa wewe ndo umekutwa na haya, ungeweza kusamehe? Unaweza kuonyesha moyo wa kusamehe kwa mkeo kwa level hii?

***** Angalizo: Nimeandika haya hapa kwa kuwa Mhusika aliyazangumza wazi kwenye EATV jana. **********
 
Ataleta wa 2, then utamsamehe, wa 3 utamsamehe, na ataendelea kumegwa nje akiwa na uhakika kuwa hata ukijua hutaweza muacha, si unataka watoto wasiishi bila baba na mama.
That's bullshit, I'll never let my kids to be used as a leverage, I may forgive her for a humanity reason and only once ila I'll never let my kids used as a bid on that case.
I'm sorry if I'm gonna be harsh, but that's who I am mkuu HP.
 
HUYO UHAJI KAUPATIA WAPI?

Mwenye kujua dini ya ki islamu hawezi kukubali mke wake azini nje ya ndoa vipi huyo afikie hatua mpaa alee mimba sio yake, na aendelee kuishi na mke wake.

Mke wako akienda nje ya ndoa piga talaka tu, hakuna zaidi ya hilo...wanao samehe wake zao wakienda nje ya ndoa nashaka sana wana matatizo ya kiume.
 
Mkuu nafikiri anaamini kuwa mke akikosa na akaomba msamaha anamaanisha kuacha kabisa hizo tabia. So may be expectation zake ni kuwa kosa hilo halitarudiwa tena! Kwa akina sisi, daaaa ni ngumu kidogo kusamehe, kulea mimba na baadaye mtoto ambaye tayari ana babayake ambaye pia yuko hai!

Lakini imani ndivyo inavyofundisha, samehe saba mara sabini, Khaaa!
 
HUYO UHAJI KAUPATIA WAPI?

Mwenye kujua dini ya ki islamu hawezi kukubali mke wake azini nje ya ndoa vipi huyo afikie hatua mpaa alee mimba sio yake, na aendelee kuishi na mke wake.

Mke wako akienda nje ya ndoa piga talaka tu, hakuna zaidi ya hilo...wanao samehe wake zao wakienda nje ya ndoa nashaka sana wana matatizo ya kiume.

Fazaa nakubaliana na wewe dini ya Kiislam na dini zingine zote hazikubali mke/mume kuzini nje ya ndoa. Ishu ni kuwa, jamaa hakumruhusu mkewe, ila alipokuwa kambini ndo akamkuta mkewe kafanya hilo kosa, probably bahati mbaya. Kwa imani zinatufundisha kusamehe, akaamua kumsamehe mkewe kabisa na sasa anamlea na huyo mtoto wa mke wake.
 
Hakuna kumsamehe mke wako kama kavunja uaminifu huo unaitwa ujinga sio msamaha.

Hilo zee linafaa kuitwa jinga lolo Ramadhani sio Haji Ramadhani :biggrin1:
 
Hakuna kumsamehe mke wako kama kavunja uaminifu huo unaitwa ujinga sio msamaha.

Hilo zee linafaa kuitwa jinga lolo Ramadhani sio Haji Ramadhani :biggrin1:

Fazaa, hujawahi kumpenda mtu kiukweli nini? Mapenzi ni complex mkuu na ukimpenda mtu kiu-kweli unakuwa na moyo wa subra na kusamehe mkuu. Wako wengine huwa wanatishiwa hata kufa, au kunusurika kufa lakini still hurudi kwenye ndoa zao, au hao nao hujawahi kuwasikia? Mapenzi huwarudisha mdogo wangu!
 
Jana majira ya saa tatu unusu nikiwa najifanyia kazi zangu kwenye laptop, huku nikipitisha macho kwenye TV, ghafla nikaona kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV na kuongozwa Salama Jabir, kikianza na mhojiwa akiwa Haji Ramadhan.

wana "RUZINGA" hawajifichi
 
Huyo mwanamke anaweza kuzaa tena na jamaa huyohuyo maana wanajua kuna ***** lao litalea tena mtoto. Kama kaweza mara ya kwanza atashindwaje mara ya pili?
Na lazima jamaa atakuwa anawasiliana nae kujua hali ya mwanae. Jiulize kama huyo dada kanona jamaa atakuwa bado udenda haumtoki?
Ngumu kumeza kwa upande wangu.
 
daaah jamaa anamoyo wachuma nini? au inawezekana hata huyo haji anawatoto wanje. kwahiyo anajua siku ikijulikana nae asamehewe kirahisi.
 
Fazaa, hujawahi kumpenda mtu kiukweli nini? Mapenzi ni complex mkuu na ukimpenda mtu kiu-kweli unakuwa na moyo wa subra na kusamehe mkuu. Wako wengine huwa wanatishiwa hata kufa, au kunusurika kufa lakini still hurudi kwenye ndoa zao, au hao nao hujawahi kuwasikia? Mapenzi huwarudisha mdogo wangu!
Sijawahi kusika kupenda ni sehemu moja wenye kupendana huwa wanapendana na wanaheshimiana....Anaye toka nje ya ndoa anakasoro tu flani na mara nyingi sana sijawahi kusikia kikombe cha chai kikawa chai na chai ikawa kikombe.

DAWA YA MWANAMKE MZINIFU NI TEKE TU AENDE AKAZINI KWAO SIO KWENYE NYUMBA YA MME WAKE.

Huyo haji anatakiwa bakora ili ajue nini mana ya kuwa Rijal.
 
Back
Top Bottom