Haja ya kuwa na Machapisho ya Jamii Forum

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,718
457
Wana jamvi, nimekuwa nikisoma sana mabandiko humu ndani na wakati mwingine nami hubandika. Elimu iliyomo humu imetufaidia sana tunaoweza kuingia mtandaoni na wachache tukutanao katika vijiwe vya kahawa, mama muuza,kwenye mambo yetu yale, n.k. Kwa upande wangu naona kama eneo kubwa la watanzania halifikiwi na ujumbe/mchango mzito wa wana jamii forum. Ushauri wangu sasa, naomba tuwe na utaratibu wa kuandaa vijarida, machapisho au vitabu vitakavyo jumuisha michango yote ya mawazo juu ya mambo ya msingi katika uhai wa Taifa letu. Kwa mfano, tukitoa kitabu juu ya mchakato wa kupatikana kwa KATIBA MPYA kuonyesha ni jinsi gani wana jamvi wanavyoshiriki kwa dhati.
Naomba kuwasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom