Haitoshi! - Chenge jiuzulu na Ubunge!

tatizo ni la CCM ya leo, tumeingiliwa na Mafia ambao kazi yao ni Ufisadi tu, nothing else. Ufisadi ulikuwepo before but not to these levels whereby these guys feel untouchable. It is a gang of select people that needs to be weeded out. kusema CCM nzima ni wafisadi isnt true

Sasa mkuu tuchoreni mstari tujue ufisadi unaishia mipaka gani katika CCM. Na kama mafisadi na wasio mafisadi wanajulikana katika CCM, kinachoshindikana kuwatimua hao mafisadi ni nini hasa?
 
Chenge amechaguliwa ubunge na watu wa Bariadi kwa tiketi ya CCM.

Vyanzo viwili vinavyoweza kwa uhalali kumfanya Chenge aondoke kwenye Ubunge ni CCM (kwa kumvua uanachama au kumuomba ajiuzulu ubunge) na watu wa Bariadi (kwa kuandamana na kumtaka mbunge wao ajiuzulu)

Wengine tunachoweza kufanya ni kumtaka aelezee alivyozipata hizo hela na ikibidi uchunguzi wa rushwa ufanywe.

Habari ya kumtaka ajiuzulu ubunge Mtanzania wa kawaida sio mahali pake, hata kama wewe ni CCM na unataka Chenge ajiuzulu ubunge ili chama kisipakwe matope kwa ajili yake, watu wa kuwalalamikia sio Chenge bali ni uongozi wa CCM (ku lobby Chenge afukuzwe uanachama au kutakiwa ajiuzulu ubunge na uongozi chamani)

Tusiwe tunapiga kelele tu, unataka Chenge ajiuzulu ubunge wewe kama nani? Kma ni mna-Bariadi gete gete kwenuko sawa sawa kabisa, lakini kama siyo huna haki kumpigia kelele Chenge.
 
HEH...YABIZILE KINEHE?...Chenge...Chenge...kaiba mahela ya selekali...Balyadi...bagosha twite kinehe lulu ehaha.? Afanyiziwe maandamano kuanzia mipaka yote ya eneo ya kumfulusha ubunge...shenji gete.Ametufanya Wasukuma pumbafu...fisadi.yale machumvi yako na masukali na mavitenge....mabiya na manyama....kumbe ulikuwa umeiba?
 
sisi kama watanzania tunaweza kuishinikiza ccm kumvua umember chenge na hivyo kumuondolea haki ya kuwa mbunge.
pia tunaweza kuwakumbusha watu wa bariadi haki yao ya kuweza kumsinikiza mbunge wao kuachia ngazi iwapo hawamtaki.
sasa sie hapa kama JF tupo kumtaka JK amvue umember wa ccm chenge ili ubunge mvuke pia
 
a. Chenge alipochaguliwa kuwa Mbunge hakuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Bariadi. Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano - Hivyo kila raia wa Jamhuri hiyo ana haki ya kusema lolote juu ya uongozi wa Chenge na Ubunge wake.

b. Chenge anapoingia Bungeni hasubiri hadi hoja zinazohusu Bariadi Magharibi ndio atoe maoni, na anapokaa kutunga sheria hatungi sheria zinazohusu Bariadi Magharibi na kukaa pembeni zinapokuja sheria za Bariadi Mashariki. Sheria anazoshiriki kutunga ni za Jamhuri nzima - hivyo kila raia wa Jamhuri hiyo bado ana haki ya kutolea maoni uongozi na ubunge wake na kutotaka kuwa na mtunga sheria kama yeye.

c. Chenge ameongoza Idara ya Mwanasheria Mkuu kwa karibu miaka kumi na katika miaka hiyo ufisadi wa mikataba ulifikia kilele; ni kutokana na kujulikana kwake katika nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu (akiwa pia Mbunge ex officio) Chenge akaamua kwenda kugombea Ubunge na akaupata na kurudi Bungeni kama Mbunge wa Kuchaguliwa. Ni kutokana na kuchaguliwa kwake akaingizwa katika serikali kama Waziri. Maamuzi yake katika Uwaziri hayakuwaathiri watu wa Bariadi tu, na hakuna ushahidi kuwa fedha alizoficha Jersey na kwingineko ni za WanaBariadi tu. YOte yanalihusu Taifa.

NI kwa sababu hiyo basi, kama kweli amepima uzito wa tuhuma zinazomkabili na madai ambayo yameelekezwa kwake, ni wazi kuwa hatendei haki Jamhuri na Bunge letu kwa kuendelea kushika nafasi ya Ubunge na kama kweli yeye ni mwajibikaji basi wakati umefika wa yeye kuachia pia kiti cha Ubunge ili CCM iweze kumsimamisha mtu mwingine.

Vinginevyo endapo utakuja mjadala Bungeni ambao utakuwa unamgusa kimaslahi na akaamua kushikilia shilingi au kutumia nafasi yake ya parliamentary immunity kusema na kuzua mambo mengine ambayo asingeweza kuyafanya nje ya Bunge basi ni wazi ni hatari kwa demokrasia nzima ya Bunge.

Chenge ni lazima ajiuzulu pia Ubunge ili kuondoa kuonekana kwa aina yoyote kuwa suala dhidi yake ni dogo na linahusu Uwaziri tu. Kimsingi linamhusu yeye kama kiongozi wa Kitaifa.

CHENGE JIUZULU UBUNGE, UMELILETEA AIBU TAIFA!
 
Vyanzo viwili vinavyoweza kwa uhalali kumfanya Chenge aondoke kwenye Ubunge ni CCM (kwa kumvua uanachama au kumuomba ajiuzulu ubunge) na watu wa Bariadi (kwa kuandamana na kumtaka mbunge wao ajiuzulu)

Sasa usishangae watu wa Bariadi wakaandamana kumuunga mkono mbunge wao kama walivyofanya watu wa Monduli.

Unajua ambacho nimejifunza kutokana na mkutano wa juzi pale London ni kwamba pengine sisi hapa JF tunaona mambo kwa jicho tofauti sana na watanzania wengine. Yaani pale ilikuwa kama vile mambo Tanzania ni shwari kabisa; tena habari za akina Chenge hazikuonekana kama ni issue. Na kuna afisa moja wa serikali mkubwa sana alinifuata akaniambia hivi nyie mnaona mtu kuwa na $1m ni issue kweli, hiyo mbona ni pesa kidogo sana? So the question is, are we (JF) out of touch with the rest of Tanzanians?
 
Chenge ni lazima ajiuzulu pia Ubunge ili kuondoa kuonekana kwa aina yoyote kuwa suala dhidi yake ni dogo na linahusu Uwaziri tu. Kimsingi linamhusu yeye kama kiongozi wa Kitaifa.

The question is why only Chenge? Kuna watu kibao wamelipa taifa hasara za kutisha kupitia IPTL na kadhalika, mbona hatukusema hawa nao wajiuzulu ubunge wao? Vipi Lowasa na Richmond yake mbona tulimuacha na ubunge wake? Vipi Rostam mbona tunewakubalia CCM kuukalia ukweli wa mambo ambao ulikuwa uanikwe na Rostam? Mbona hatujasema spika aondoke kwa partiality yake bungeni?

Kujiuzulu Chengu ubunge ni wazo zuri sana, lakini tuache double standard. Isionekane kwamba wizi wa Chenge unazidi ule wa majambazi wengine serikalini. By the way, so far kilichomfanya Chenge ajiuzulu hatujaambiwa-kama ni hizo hela au hicho kidomokidomo chake cha kusema vijisenti!
 
Kitila, jibu jepesi why Chenge ni kuwa... look at the money. Kati ya wote uliowatolea mfano hakuna hata mmoja wao (hata Balali) ambaye ametajwa kuweka fedha yoyote nje ya nchi na hakuna hardcore evidence ya yeye kujilimbikizia fedha kiasi cha kuwekeza nyingine kwenye kisiwa cha Jersey. Only Chenge.

Lakini kuna sababu nyingine pia; Chenge amewatukana Watanzania kuliko mwingine kati yao. Si Lowassa, wala Balali waliothubutu kutrivialize walichofanya kama alivyofanya Chenge.

Lakini pia si kweli kuwa Lowassa na wengine hatukutaka wajiuzulu Ubunge. Makala zangu za Tanzania Daima na zile za Raia Mwema kote nilisema wazi kuwa CCM lazima iwawajibishe ikiwemo na kutaka wajiuzulu Ubunge na ikithibitika (kama kwa Chenge) kuwa makosa yao si ya kiutendaji tu (mismanagement) lakini pia ni ya kifisadi basi wavuliwe na uanachama.

Kwa upande wangu, katika hili sina double standard, I only have one standard and one standard only; madai ya kifisadi yakizidi juu yako, na ukaonekana kuna ushahidi wa wewe kutumia nafasi yako vibaya kujinufaisha, kujiuzulu nafasi yako tu haitoshi, lazima uwajibishwe pia na chama chako na kama ni mbunge lazima pia ujiuzulu.
 
Lakini pia si kweli kuwa Lowassa na wengine hatukutaka wajiuzulu Ubunge. Makala zangu za Tanzania Daima na zile za Raia Mwema kote nilisema wazi kuwa CCM lazima iwawajibishe ikiwemo na kutaka wajiuzulu Ubunge na ikithibitika (kama kwa Chenge) kuwa makosa yao si ya kiutendaji tu (mismanagement) lakini pia ni ya kifisadi basi wavuliwe na uanachama.
.
Yes I said and you said am Wrong?the sama M. M Mwanakiji who is also Lula wa Ndali.Kwanini usikubali yaishe kuliko kunifanya mie muongo na mzushi??
I love what you write and you have made me like to read more books and all Acts which are being used here in Tanzania.

Bada ya kusema hayo,Mzee Mwanakijiji hauoni kama hili ni bao lingine la kisigino??
 
Wewe unahitaji kufanyiwa uchunguzi wa akili. Kwani kama Mkjj ndiye Lila hiyo inasaidia vipi kujua jina halisi la Mkjj? Mbona yote bado ni pen names?

Kwi kwi kwi kwi ... yaani hapa imebidi nianze kucheka tu hapa!
 
Na yule aliyesema hata ikibidi watu kula nyasi ili ndege ya raisi inunuliwe, naye hakuwatukana Watanzania? Lipi ni tusi kubwa...kusema dola milion moja ni visenti au kumwambia mtu kula nyasi (sina nukuu kamili)? Hivi huyo waziri alijiuzulu wadhifa wake serikalini na ubunge aliokuwa nao?

Halafu mimi siamini kabisa kama Kikwete naye yuko safi ingawa ushahidi sina. Lakini kama yuko clueless kabisa na ufisadi unaondelea basi na yeye hastahili kuwa raisi. Ajiuzulu mara moja! Kama anajua kuhusu huo ufisadi na yeye kwa namna moja au nyingine anahusika nao halafu anaendelea kuwateua mafisadi ktk nyadhifa kubwa serikalini basi judgement yake ni mbovu na hilo pekee linatosha kwa yeye kubwaga manyanga chini. We just can't have a head of state whose judgement is grossly flawed. Let's have same standards for everyone.
 
Huyo mzee wa nyasi nimekuwa nampiga vita hapa kwa muda mrefu sana na alichokisema yeye ni offensive big tyme. Haya yote yanazidi kuonyesha kuwa Kikwete naye ni fisadi tu like everybody else kwenye government yake iliyojaa mafisadi.
 
Yes I said and you said am Wrong?the sama M. M Mwanakiji who is also Lula wa Ndali.Kwanini usikubali yaishe kuliko kunifanya mie muongo na mzushi??
I love what you write and you have made me like to read more books and all Acts which are being used here in Tanzania.

Bada ya kusema hayo,Mzee Mwanakijiji hauoni kama hili ni bao lingine la kisigino??

nadhani umefanya uvumbuzi wa mwaka...! Hakuna mahali nilipojaribu kukufanya uwe muongo na mzushi. Tafuta thread humu iliyoleta habari za kuanzishwa kwa gazeti la Raia Mwema. Labda utaelewa. Lakini umejipa jukumu ambalo ni la kujitekea to prove the obvious.
 
Na yule aliyesema hata ikibidi watu kula nyasi ili ndege ya raisi inunuliwe, naye hakuwatukana Watanzania? Lipi ni tusi kubwa...kusema dola milion moja ni visenti au kumwambia mtu kula nyasi (sina nukuu kamili)? Hivi huyo waziri alijiuzulu wadhifa wake serikalini na ubunge aliokuwa nao?

Halafu mimi siamini kabisa kama Kikwete naye yuko safi ingawa ushahidi sina. Lakini kama yuko clueless kabisa na ufisadi unaondelea basi na yeye hastahili kuwa raisi. Ajiuzulu mara moja! Kama anajua kuhusu huo ufisadi na yeye kwa namna moja au nyingine anahusika nao halafu anaendelea kuwateua mafisadi ktk nyadhifa kubwa serikalini basi judgement yake ni mbovu na hilo pekee linatosha kwa yeye kubwaga manyanga chini. We just can't have a head of state whose judgement is grossly flawed. Let's have same standards for everyone.

Nyani, kila mpiga ngoma hupiga aitakavyo; na ngoma hunoga zikipigwa zaidi ya moja. Sasa kama mtu akipiga ya chenge, na mwingine apige ya Mramba, na mwingine apige ya Lowassa hata ya Kikwete... kwanini mpiga ngoma atakiwe apige ngoma zote yeye wengine wabakie kucheza tu au kutikisa miguu? kama unayo ngoma na unataka kupiga piga... sidhani kama inaoondosha utamu wa ngoma anayopiga mwingine.
 
Huyo mzee wa nyasi nimekuwa nampiga vita hapa kwa muda mrefu sana na alichokisema yeye ni offensive big tyme. Haya yote yanazidi kuonyesha kuwa Kikwete naye ni fisadi tu like everybody else kwenye government yake iliyojaa mafisadi.

Yaani kwa stretch yoyote ile ya imagination huwezi ukalinganisha kuambiwa kula nyasi ili ndege ya mkubwa inunuliwe na Chenge kuita $ millioni moja vijisenti (halafu watu wanasahau kuwa aliongezea kuwa kila mtu ana viwango vyake-which is true). Huyu fisadi wa nyasi naye si bado mbunge? Naye ajiuzulu mara moja kwa kutukana humanity nzima!!
 
Nyani, kila mpiga ngoma hupiga aitakavyo; na ngoma hunoga zikipigwa zaidi ya moja. Sasa kama mtu akipiga ya chenge, na mwingine apige ya Mramba, na mwingine apige ya Lowassa hata ya Kikwete... kwanini mpiga ngoma atakiwe apige ngoma zote yeye wengine wabakie kucheza tu au kutikisa miguu? kama unayo ngoma na unataka kupiga piga... sidhani kama inaoondosha utamu wa ngoma anayopiga mwingine.

True that....

Mramba na wewe jiuzulu mara moja kwa kuutusi ubinadamu kwa kauli yako ya nyasi!!!
 
Yaani kwa stretch yoyote ile ya imagination huwezi ukalinganisha kuambiwa kula nyasi ili ndege ya mkubwa inunuliwe na Chenge kuita $ millioni moja vijisenti (halafu watu wanasahau kuwa aliongezea kuwa kila mtu ana viwango vyake-which is true). Huyu fisadi wa nyasi naye si bado mbunge? Naye ajiuzulu mara moja kwa kutukana humanity nzima!!

Taratibu tu wote watakuja kwenye same standard. So far nategemea Kikwete kuitisha kikao cha chama haraka sana na kufanya some house work. Ukiangalia trends kwenye viongozi wa ccm na wale wa kwenye serikali utaona jinsi ufisadi na dharau zilivyo part of their lives!
 
Na yule aliyesema hata ikibidi watu kula nyasi ili ndege ya raisi inunuliwe, naye hakuwatukana Watanzania? Lipi ni tusi kubwa...kusema dola milion moja ni visenti au kumwambia mtu kula nyasi (sina nukuu kamili)? Hivi huyo waziri alijiuzulu wadhifa wake serikalini na ubunge aliokuwa nao?

Na huyu Katibu wa kudumu,Mgonja anasubiri nini??
 
Huyo jamaa ajiuzulu ubunge au asijiuzulu sisi tunachotaka vijisenti vyetu virudi. Ila nawashauri watu wa jimbo lake waliomchagua sababu alikua na vijisenti wamkatae na wamzomee atakapokwenda kuongea nao, wasilete habari ya Monduli baada ya Lowassa kujiuzulu.
 
I beg to differ,

a. Chenge alipochaguliwa kuwa Mbunge hakuchaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Bariadi. Alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano - Hivyo kila raia wa Jamhuri hiyo ana haki ya kusema lolote juu ya uongozi wa Chenge na Ubunge wake.

Tatizo sio Chenge amechaguliwa katika bunge gani, tatizo kachaguliwa na nani? Constituency yake ni wapi? Kama Mbunge wa BAriadi anawajibika kwa watu wa Bariadi, kama Mbunge wa CCM anawajibika kwa CCM.Kwa hiyo kama kuna watu wa kuhimizwa wamuwajibishe Chenge ni watu wa bariadi na CCM.Sasa hivi kama mbunge wa Bariadi Chenge hawajibiki kwa mpiga kura siye wa Bariadi.Kama una beef naye unataka ajiuzulu ubunge ongea na watu wa Bariadi au shinikiza vikao husika vya CCM vimvue uanachama au kumshurutisha ajiuzulu vyeo vya kichama.Vinginevyo ukimwambia Chenge ajiuzulu ubunge wa Bariadi, akikuuliza ulinichagua wewe utamjibuje? Akikwambia una mandate ya chama nilichosimamia utamjibuje?

Sasa whats next? Akishajiuzulu ubunge tumwambie ajivue u board member Barricks Gold (mfano tu)wakati sisi sio hata shareholders wa Barrick Gold? Waache shareholder (CCM na watu wa Bariadi) waamue. Sisi tunaweza kuweka pressure kwenye corruption charges tu.Naona sasa tutataka mpaka kwa mkewe nako ajiuzulu kwa mtaji huu.Give CCM a chance to show how they stand, talk to them, not Chenge.

b. Chenge anapoingia Bungeni hasubiri hadi hoja zinazohusu Bariadi Magharibi ndio atoe maoni, na anapokaa kutunga sheria hatungi sheria zinazohusu Bariadi Magharibi na kukaa pembeni zinapokuja sheria za Bariadi Mashariki. Sheria anazoshiriki kutunga ni za Jamhuri nzima - hivyo kila raia wa Jamhuri hiyo bado ana haki ya kutolea maoni uongozi na ubunge wake na kutotaka kuwa na mtunga sheria kama yeye..

Kila raia ana haki ya kutoa maoni kuhusu kila kitu.Hiyo haimaanishi maoni hayo yana msingi.Kumwambia mtu ajiuzulu ni zaidi ya maoni, ni protest, ni lobbying.Unapomwambia mtu ajiuzulu -which is becoming a myopic trend here nowadays- you better be ready with facts and not only maoni.Kama wewe ukisema unataka Chenge ajiuzulu na wapiga kura wa Bariadi wakisema wanamtaka mbunge wao je, wewe utaonaje? Wewe utaonaje kama mbunge wako unayempenda (Mfano Slaa au Zitto) watu wa Bariadi wanakuja kumpigia kelele ajiuzulu, utaona hiyo fair?

c. Chenge ameongoza Idara ya Mwanasheria Mkuu kwa karibu miaka kumi na katika miaka hiyo ufisadi wa mikataba ulifikia kilele; ni kutokana na kujulikana kwake katika nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu (akiwa pia Mbunge ex officio) Chenge akaamua kwenda kugombea Ubunge na akaupata na kurudi Bungeni kama Mbunge wa Kuchaguliwa. Ni kutokana na kuchaguliwa kwake akaingizwa katika serikali kama Waziri. Maamuzi yake katika Uwaziri hayakuwaathiri watu wa Bariadi tu, na hakuna ushahidi kuwa fedha alizoficha Jersey na kwingineko ni za WanaBariadi tu. YOte yanalihusu Taifa.

Umesema vizuri, maamuzi yake kama Waziri hayakuwaathiri watu wa Bariadi tu, bali yaliathiri taifa zima.Ndiyo maana sikusema kitu kumtetea, to the contrary nili-champion call ya Chenge kujiuzulu uWaziri kwa sababu hapo nilikuwa katika constituency yake kama Mtanzania na yeye kama Waziri wa cabinet ya Tanzania, lakini hili la bariadi mimi kama sio mpiga kura wa Bariadi, na kama sio mwanachama wa CCM simo katika constituency yake na sina haki ya kumpigia kura ajiuzulu.

Ndiyo maana yule mpuuzi Alberto Gonzalez alikaa Justice Department miezi kibao overdue aki parrot "I serve at the pleasure of the president" kwa sababu alikuwa ni presidential appointee, who appoints/elects has the last say.Sasa Chenge akikwambia "I serve at the pleasure of the Bariadi people, who are behind me" utamwambia nini? Ndiyo maana nasema kama kuna mtu wa kumshawishi amtake Chenge ajiuzulu ubunge ni wanachi wa Bariadi na watu wa CCM.

NI kwa sababu hiyo basi, kama kweli amepima uzito wa tuhuma zinazomkabili na madai ambayo yameelekezwa kwake, ni wazi kuwa hatendei haki Jamhuri na Bunge letu kwa kuendelea kushika nafasi ya Ubunge na kama kweli yeye ni mwajibikaji basi wakati umefika wa yeye kuachia pia kiti cha Ubunge ili CCM iweze kumsimamisha mtu mwingine.

Kama bado unaamini kuna kupima kokote kwa aina hiyo kunakoendelea you are mistaken.The only thing Chenge anachopima ni "what can I get away with" na katika hili he can get away with being an MP if neither CCM nor the Bariadi people demands his resignation.Ndiyo maana nakwambia lobby with them, not Chenge.

Vinginevyo endapo utakuja mjadala Bungeni ambao utakuwa unamgusa kimaslahi na akaamua kushikilia shilingi au kutumia nafasi yake ya parliamentary immunity kusema na kuzua mambo mengine ambayo asingeweza kuyafanya nje ya Bunge basi ni wazi ni hatari kwa demokrasia nzima ya Bunge.

Indeed,

Lakini demokrasia hiyo hiyo ndiyo iliyowapa haki wananchi wa Bariadi kumchagua na wewe kumchagua mbunge wako.Kwa hiyo si vizuri wewe ambaye hukumchagua mbunge wa Bariadi huna mamlaka, humna moral argument, hauko katika constituency yake.Ongea na mabosi wake, watu wa BAriadi na CCM, na siyo kumtaka Chenge ajiuzulu, atakucheka tu na kukuambia unasumbuliwa na mvua na kukufanya the object of his arrogant ridicule.

Chenge ni lazima ajiuzulu pia Ubunge ili kuondoa kuonekana kwa aina yoyote kuwa suala dhidi yake ni dogo na linahusu Uwaziri tu. Kimsingi linamhusu yeye kama kiongozi wa Kitaifa.

Utaongea hivyo kama nani wakati huko katika constituency yake? Wakikwambia wanampenda BAriadi utasemaje?

CHENGE JIUZULU UBUNGE, UMELILETEA AIBU TAIFA!

Tafuta mwingine wa kumshtakia Chenge (CCM, bariadi voters) lakini si kumtaka Chenge mwenyewe ajiuzulu
 
Back
Top Bottom