Haitapita Muda Mrefu, Formula ya Kumuondoa Kikwete Madarakani itapatikana!

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Shida ni kuwa-mobilise wananchi watambue ya kwamba huyu jamaa nchi imemshinda.
Lakini kwa matukio yanayoendelea, na yanayowaathiri wananchi punde nchi italipuka.
Angalia mambo yafuatayo;
Mauaji yaliyotokea arusha
Mauaji yaliyotokea Nyamongo
Uvamizi wa ardhi unaotokea sehemu mbalimbali nchini
Suala la mgawo wa giza
Suala la serikali kuishiwa na kukopa kopa benki za ndani
Mishahara ya waalimu
Migomo vyuoni
Uchakachuaji kwenye Kilimo Kwanza
Ufisadi UDA,Meremeta,EPA n.k
Mgawanyiko ndani ya chama cha magamba (CCM)
Malipo duni kwa polisi na wanajeshi
Ukosefu wa ajira kwa vijana
Kuwagawanya watanzania kwa kutumia propaganda za UDINI
Uchakachuaji wa kura uliofanywa kwenye uchaguzi wa mwaka jana
Mfumuko wa bei usio dhibitiwa huku gharama za maisha zikipanda kila uchao
Matumizi mabaya ya fedha za wahisani


NB; kwa kifupi serikali dhaifu ya sasa imeshachukiza kila kundi lililopo ndani ya taifa ili, na watu wapo standby kusubiri Amri ya mwenye kujitolea kumfunga paka kengele.
 
Pengine ni wakati mzuri wa kutafakari nje ya boksi, je ni hatua sahihi? Shida na adha kama uhaba wa mafuta, mgao wa umeme, ni mambo ya kitambo tu, yanapita. Ila swala la ufisadi na ubadhirifu wa rasilimali zetu ni changamoto kubwa kwa Rais wetu. Naamini mheshimiwa Rais Kikwete ana macho anaona, ana masikio anasikia na ni mwerevu kwa kadri Mwenyezi Mungu alivyomjalia. Inshallah, panapo uzima mabadiliko tutayashuhudia na kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom