Haipendezi kukiita CCM chama cha magamba

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
JF imekuwa na members wengi wasioipenda CCM. Siku za karibuni zimeibuka kejeli mbaya dhidi ya chama hiki kinachoongoza dola na members wengi wa JF wametumbukia kwenye kejeli hii ambayo mimi naona sio uungwana.
Mbona wao CCM hawakebehi vyama vingine? I mean mbona wao hawaiti chadema majina ya kukebehi na ya mzaha?
Nashauri Mods walambishe BAN wote watakaokuwa wanakidhalilisha chama hiki badala yake tujadiliane kwa staha. Hata kama mimi nitajisahau nitakiita chama cha magamba na mimi nilambishwe BAN tu.
Naomba kutoa hoja
 
Jana sijui juzi kuna mbunge amesema CHAMA CHA MUNGU,tena bungeni sasa hiyo si KEJELI????na taarifa zake zikiripotiwa hapa watu watakuwa wanakejel????
 
kama sio chama cha magamba, hao wanaoyavua wameyatoa wapi? nawe unaogopa kulivua lako? vumilia tu mkuu ... kuvua gamba yataka moyo ... nape anayajua vizuri!
 
Jana sijui juzi kuna mbunge amesema CHAMA CHA MUNGU,tena bungeni sasa hiyo si KEJELI????na taarifa zake zikiripotiwa hapa watu watakuwa wanakejel????
Sitapingana na yeyote atakayesema baadhi ya wabunge wa ccm ni wehu. Huyo aliyesema CCM ni chama cha Mungu kama alimaanisha Mungu aliyeumba dunia basi laana i juu yake
 
Kwa sababu mapinduzi yalishafanyika siku nyingi,kilichopo sasa ni kujivua gamba na hii inajustify ccm kuwa chama cha magamba!
 
JF imekuwa na members wengi wasioipenda CCM. Siku za karibuni zimeibuka kejeli mbaya dhidi ya chama hiki kinachoongoza dola na members wengi wa JF wametumbukia kwenye kejeli hii ambayo mimi naona sio uungwana.
Mbona wao CCM hawakebehi vyama vingine? I mean mbona wao hawaiti chadema majina ya kukebehi na ya mzaha?
Nashauri Mods walambishe BAN wote watakaokuwa wanakidhalilisha chama hiki badala yake tujadiliane kwa staha. Hata kama mimi nitajisahau nitakiita chama cha magamba na mimi nilambishwe BAN tu.
Naomba kutoa hoja

CDM wao wanapendwa kuitwa MAGWANDA, sioni kosa kusema chama cha MAGAMBA.
 
JF imekuwa na members wengi wasioipenda CCM. Siku za karibuni zimeibuka kejeli mbaya dhidi ya chama hiki kinachoongoza dola na members wengi wa JF wametumbukia kwenye kejeli hii ambayo mimi naona sio uungwana.
Mbona wao CCM hawakebehi vyama vingine? I mean mbona wao hawaiti chadema majina ya kukebehi na ya mzaha?
Nashauri Mods walambishe BAN wote watakaokuwa wanakidhalilisha chama hiki badala yake tujadiliane kwa staha. Hata kama mimi nitajisahau nitakiita chama cha magamba na mimi nilambishwe BAN tu.
Naomba kutoa hoja
Kama ni wa kulambishwa Ban wa kwanza ni wewe halafu kadiri unavyotetea kisiitwe magamba ndivyo unavyo promote jina la magamba.
 
Ni sawa lakini naamini tuna imisuse hiyo falsafa. Hata kwenye vyama vingine kuna magamba pia kwaiyo si sahihi kukiita ccm chama cha magamba

Kwani hivyo vyama vingine navyo vimejinadi hadharani kwamba vinavua hayo magamba? CCM si wenyewe ndio wametangaza kuvua magamba? sasa tukiwaita wavua magamba tunakosea nini?
 
JF imekuwa na members wengi wasioipenda CCM. Siku za karibuni zimeibuka kejeli mbaya dhidi ya chama hiki kinachoongoza dola na members wengi wa JF wametumbukia kwenye kejeli hii ambayo mimi naona sio uungwana.
Mbona wao CCM hawakebehi vyama vingine? I mean mbona wao hawaiti chadema majina ya kukebehi na ya mzaha?
Nashauri Mods walambishe BAN wote watakaokuwa wanakidhalilisha chama hiki badala yake tujadiliane kwa staha. Hata kama mimi nitajisahau nitakiita chama cha magamba na mimi nilambishwe BAN tu.
Naomba kutoa hoja

TTOZI BWEKA;
Join Date : 3rd July 2011Posts : 51

Rep Power : 21

Mazao ya semina elekezi. Karibu sana jamvini japo una only 2 days!!!!!!!!!!!! Naona juhudi zako. Kuhusu chama cha magamba. Nadhani jibu analo mwenyekiti toka alivyotangaza kujivua gamba lakini akasahau nyoka ni nyoka hata akijivua gamba sumu ni ile ile.
 
Naunga mkono,
CCM haina mvuto tena, na hii ndio nafasi pekee tuliyonayo ya kufanya mapinduzi halisi ya kifkra ili yadhihilike katika sanduku la kura.
Ila mimi siungi mkono style inayotumiwa na wanachama wa chama chochote/wananchi katika kuishambulia ccm kwa matusi maneno ya kejeli katika mtandao unaoaminika ni wa watu makini.
Style hii inapaswa itumike katika jamii ambayo haina uwezo wa kuchambua mambo kwa undani, watu wasio na muda wa kusikiliza hoja.
lakini sio eneo kama hili linalodhaniwa ni la watu wenye uelewa mkubwa.
Nawaomba vijana wenzangu wenye nia nzuri na nchi hii tuwe na utamaduni wa kujibu hoja hata kama ni ya maji taka, tunatakiwa tuishambulie kwa hoja mzingo zenye kumezeka.
Mfano juzi niliona mjumbe amabye nadhani alikuwa mkereketwa wa ccm aliandika jambo la kuhoji umakini wa cdm, badala ya watu kujibu kwa hoja, nilishangaa kuona majibu kama vile 'kavue gamba kwanza' kamuulize nepi' sidhani kama tunakuwa warithi/tunapanda hekima zozote vichwani mwetu zakuwa waamuzi wazuri bila kuwaonyesha tunaowapinga kuwa tunawazidi hoja.
Siku moja nilisema sio vyema kuishi kwa kutambua makosa tu,bali tunatakiwa tujifunze kujenga mwelekeo pia.
Tujue kutoa njia mbadala na tujue kujibu hoja kwa hoja na sio kuwa watu wenye uelewa mkubwa wa makosa tu,bali pia tuweze kutoa njia mbadala.
Tazama mijadala mingi ya vijana utagundua vijana tuna uwezo huo kinzani na ni changamoto kubwa sana kwa sasa.
Naachia hapo nikiwaomba tuikosoe serikali sana na tujifunze kutoa njia mbadala, tuwe watu wenye kujua mbinu za ujenzi wa vyama vyetu kwa maeneno muafaka, mfano hili la kebehi na makajuliso tunajua wapi pa kuitumia na sio humu.
Nao ccm wajue tu hawana mvuto na siwaombei wafe, bali nawaombea waishi maisha marefu maana hawa watakuwa wakosoaji wetu wazuri sana hapo baadae wakiwa chama cha upinzani.
Nawakumbusha kuchukua hatua ya kuvua magamba kama walivyoahidi wenyewe vinginevyo:- hawataamini kitakachowatokea na posho zao mifukoni.
 
Nyakarungu nimekupata na uko sawa kwa comment zako ila ni vema ukajua profile za wanachama wengi wa JF. Wengi ni vijana wasomi walioko vyuoni na makazini na si kwamba hawajui kuchambua mambo ila naona wengi wana hasira na yanayotokea TZ na hapa ni kama wana pre-empty mind zao. Kinachotakiwa humu ni kuzingatia masharti ya JF ila kufundisha watu jinsi ya kukosoa na kukielezea CCM ni kuzuia uhuru wa kujieleza na kwa namna hii JF itakosa mvuto .
Hatuwezi kuita chungwa parachichi mkuu kwa hiyo lazima tuonyeshe kero zero kwa kutumia vema maneno yatakayo portray mtazamo wetu kwa hiki chama. Tunatakiwa tu tusitukane matusi no more.
 
Mambo ya majina sio tatizo, tatizo wananchi kukosa huduma za jamii, hapendezi wananchi kukosa umeme
 
JF imekuwa na members wengi wasioipenda CCM. Siku za karibuni zimeibuka kejeli mbaya dhidi ya chama hiki kinachoongoza dola na members wengi wa JF wametumbukia kwenye kejeli hii ambayo mimi naona sio uungwana.
Mbona wao CCM hawakebehi vyama vingine? I mean mbona wao hawaiti chadema majina ya kukebehi na ya mzaha?
Nashauri Mods walambishe BAN wote watakaokuwa wanakidhalilisha chama hiki badala yake tujadiliane kwa staha. Hata kama mimi nitajisahau nitakiita chama cha magamba na mimi nilambishwe BAN tu.
Naomba kutoa hoja

Kama na wewe ni baba huruma wa chama cha magamba na wewe kavue gamba maana ndicho kinachoendelea sasa hivi kwa chama cha magamba, chama dola na chama cha mafisadi.
 
Back
Top Bottom