Haipendezi hata kidogo

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,832
. . .haipendezi sana mume na mke mmepanda gari lenu asubuhi mnaenda ku kazi huku
mmenunaaa njia nzima! Bora mmoja ashuke akatafute daladala apate kucheka na vituko
vya wapiga debe! Hata mfungwa akisindikizwa na askari utawaona wanapiga stori na
kucheka njia nzima,nyie mnashindwa nini?! Nawatakia jumanne njema!
 
Imekuwa ni kawaida kwa wanandoa kutocheka wakiwa pamoja. Ukiona hivyo ujue pepo mbaya kaishapita kati yao. Ili kunusuru hii kabla ya kutoka nyumbani hata kama mmenuniana inabidi muongee yaishe!
 
. . .haipendezi sana mume na mke mmepanda gari lenu asubuhi mnaenda ku kazi huku
mmenunaaa njia nzima! Bora mmoja ashuke akatafute daladala apate kucheka na vituko
vya wapiga debe! Hata mfungwa akisindikizwa na askari utawaona wanapiga stori na
kucheka njia nzima,nyie mnashindwa nini?! Nawatakia jumanne njema!

Dawa ni kila mtu awe anakwenda na gari yake ili acheke vizuri? Kweli appetite tunatafuta barabarani kushiba tunashibia nyumbani! Jnne njema Nazjaz
 
Last edited by a moderator:
Hakuna jipya la kudiscuss naye kama lipo muda wa home unatosha barabarani no maongezi

Nazjaz umepotea wewe mpaka naumwa kukukosa
 
Ukiona mwanaume yuko kwenye gari na mwanamke na wanatabasamu, story kwa wingi n.k. ujue hiyo ni small house teh.
 
Ndoa hizi!!..kila siku yanakuja mapya!
Sasa mkinuniana kwenye gari huko home inakuwaje??
 
Ukiona hivyo wamepigwa chini NEC AU mmoja kachaguliwa mwengine kachezea jalamba.....

Ndoa ngumu sijui wazee wetu waliwezaje kukabiliana nazo laiti wazee wangu wangekuwa hai ningewauliza
 
newly-designed-or-developed-seat-belt-wife-mouth.gif
it works here!
 
kutoelewana huwa kunatokea sn wakatimwingine kukaa k100 kunasaidia kupunguza hasara zapande mbili. ila mwanaume jitahid kuwa wakwanza kurejesha mazungumzo tena anzia kwakuomba ile kitu! huku ukileta utan mwingi aman itarud
 
Back
Top Bottom