Hainiingii kichwani serikali kusema inakabiliwa na ukata!

Baba C

Senior Member
Mar 15, 2012
125
55
Waziri mkuu alitangaza bungeni serikali kukabiliwa na ukata wa hela!Amezitaka Wizara na taasisi mbalimbali kubana matumizi kwa chochote watakachopata(kama wakibahatika kupata)

  1. Zito aliwahi kusema serikali imeishiwa na Waziri wa fedha Mustafa Mkulo kumkatalia na kumwambia ni muongo! NAFIKIRI NI WAKATI MUAFAKA WA MKULO KUWAJIBIKA NA KUJIUZULU KATIKA HILI.
  2. Kila mfanyakazi iwe wa UMMA au sekta binafsi anakatwa kodi kulingana na mshahara wake."THE HIGHER THE SALARY THE HIGHER THE TAX"Ni hela nyingi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
  3. Kila mkulima na mfanyakazi analipa kodi katika kila bidhaa anayoinunua apende asipende. Ni hela Nyingi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
  4. TRA imekuwa ikisifika kwa makusanyo makubwa hivi karibuni. Zinakwenda wapi?
  5. Vipi kuhusu vyanzo vingine vya mapato kama madini mbalimbali,mbuga za wanyama,ardhi kubwa na yenye rutuba pamoja rasilimali zingine nyingi...............
  6. Wakati huo huo watu wenye kipato kidogo kama walimu,manesi,maaskari na nk wanakatwa kodi wakati kuna mijitu yenye kipato kikubwa na inakwepa huku huku walikindwa na kukumbatiwa na serikali.........?
  7. Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali imethitisha matumizi mabaya ya fedha katika halmashauri nyingi nchini.HELA ZA KUTOA RUSHWA KATIKA CHAGUZI MBALIMBALI ZINAPATIKANA,MAFISADI WANAKUMBATIWA!KWA KWELI SIELEWI!
  8. NATAMANI MSHAHARA WANGU USIKWATWE KODI TENA MAANA SIONI UMUHIMU WAKE
  9. TUACHE USHABIKI NA TUTANGULIZE UZALENDO.TUFANYE MABADILIKO YA DHATI.
 
hii ndo shida ya kuongozwa na wakeshao kwa waganga wa kienyeji!
 
nikiangalia ni kiasi gani nalipa kama payee inaniuma sana...

huenda safari za nje za mkuu wa kaya zimefilisi hazina.. wakakope huko anakoendaga.
 
jamani usiseme sasa hivi kodi serikali inazokusanya ni nyingi sana ila sasa matumiz ndio makubwa hivi unafikiri magari haya ya kifahari kuyweka tu barabarani ni sh ngapi yanatumia? je hao wa mjengoni wamewah kukopwa au ni sisi walalahoi ndo tunaokopwaga tu? hela wanayo ila ocs ni kuba kuliko za maendeleo
 
Back
Top Bottom