Hai kwachafuka; Viongozi wa CCM waendelea kula kichapo! Dr.feki anusurika kula kichapo

mao tse tung

Member
Mar 24, 2011
51
11
Ile hali ya wananchi kuendelea kupoteza uvumilivu inaendelea kusambaa.

Leo hii imetokea jimboni Hai jimbo la kiongozi wa upinzani pale mwenyekiti wa kijiji cha isuki kata ya masama kati walipojikuta wakila kichapo cha kutosha. sababu ya viongozi hawa kupewa kichapo ni pale chama cha mapinduzi kilipojimilikisha jengo ambalo ni ofisi ya kijiji na kuweka bendera ya CCM.

Katika mkutano huo mwananchi mmoja aliuliza ''umetuita kwenye kikao cha chama au cha serikali?" mwenyekiti alijibu ni kikao cha serikali, kisha akaulizwa tena sababu za yeye kuja na sare za CCM pamoja na kutundika bendera ya CCM. Hali ilibadilika ghafla kichapo kikatembea ambapo afisa mtendaji wa kijiji alibanwa koromeo na kujikuta akimwaga kojo na alipofanikiwa kuchomoka hajaonekana alipokimbilia.

Kwa sasa hali sii shwari kwani wananchi wanahofu ya kukamatwa na polisi kwani kunataarifa kwamba mwenyekiti wa kijiji alitoa taarifa polisi. Nilipojaribu kuhojiana na wananchi wachache walisema "sisi tulimtaka Norman Sigala huyo anae jiita dokta wakati ni dr. feki. na bado hapa mpaka mtu afe ndio watatujua vizuri. Huyu mkuu wa wilaya ana bahati, za mwizi ni arobain.

Kuhusu source msiniulize kwani nimezipata mwenyewe kutoka kwenye tukio
 
Duh! Ebwana eh kwa hali invyoenda sasa viongozi inabidi wajitathimini upya mambo yamebadilika watu hawataki blah blah! Ile dhana kwamba siasa ni kuongeaongea tu pumba, nonsense, uwongo, upuuzi zimepita. Viongozi inabidi wabadilike la sivyo itaendelea kuwacost, hasa hasa wale wa magamba walikuwa wanaongoza kwa mazoea. Zama hizi mbona mtachezea kichapo saana tu
 
Demokrasia inapobakwa,watu hulazimika kutumia nguvu.Siungi mkono matumizi ya nguvu,lakini tujitazame upya
 
Nitatoa ratiba ya viongozi wa ccm kupigwa mitama muda sio mrefu. Ratiba hiyo imepitishwa na Kivuitu wa Tz.
 
hali sasa imeshakuwa tete huku tuankoenda wananchi wameshachoka kuvumilia lakini wanasiasa wanasema wananchi wamekosa uvumilivu
 
bado mkuu wa kaya kukabwa koromeo kama huyo mwenyekiti wa kijiji,
ina maana rangi ya njano na kijani na bendera lao hazikubaliki tena??
 
Nashauri viongozi wote wa CCM wapewe 'semina elekezi' ya namna ya kukabiliana na 'vibano' maana mtachapwa viboko kama watoto wa shule mwaka huu.
 
mwaka huu watapigwa sana hao wana magamba na ikizingatia mtabiri wao aliyekuwa akiwasaidia ameisha tangulia mbele ya haki.Kweli watanzania wameamka sasa hawamtaki mkoloni mweusi aka chama cha magamba.
 
Demokrasia inapobakwa,watu hulazimika kutumia nguvu.Siungi mkono matumizi ya nguvu,lakini tujitazame upya

mzee hivi vichwa vilikubaliana na matumizi ya nguvu pale inapobidi
>>>>>>>>>Any people anywhere, being inclined and having the power, have the right to rise up, and shake off the existing government, and form a new one that suits them better. This is a most valuable - a most sacred right - a right, which we hope and believe, is to liberate the world.
Abraham Lincoln

Be peaceful, be courteous, obey the law, respect everyone; but if someone puts his hand on you, send him to the cemetery.
MALCOLM X

An individual who breaks a law that conscience tells him is unjust, and who willingly accepts the penalty of imprisonment in order to arouse the conscience of the community over its injustice, is in reality expressing the highest respect for the law.

Martine Luther king, Jr

NA WENGINE WENGI IN FACT NI KARIBU GREAT THINKER WOTE<<<<<<<<<<<<<<<<<

ukweli ni kwamba hakuna nchi ambayo imekomboka bila wananchi kutumia nguvu pale inapobidi kufanya hivyo, maana serikali/viongozi wanapoona hali inakuwa mbaya wanapashwa kuheshimu hisia za wananchi lakini wanapolazimisha uchafu na mwenendo mbaya ina maana wao (SERIKALI/ VIONGOZI) wametumia nguvu pia na mwananchi kujibu mapigo ni katika hali ya kuwekana sawa ndio maana
inakuwa nguvu ya umma , nguvu ya umma iko mara mbili kwa hoja au kwa physical sio muda wote diplomacy
anyway naheshimu maoni yake mkuu na unahaki zote ila nitamaliza kwa kusema
UNAFIKI NA USTAARABU WA KIZOBA/KIJINGA SIJUI TULIUTOA WAPI? NDIO UMETUFIKISHA HAPA TULIPO
 
Si vizuri jamani kuwapiga viongozi wenu....

Ujumbe wa kujivua gamba bado haujafika mashinani na inawezekana bado hawa watu wana chuki na CCM. Na hata kama ujumbe wa kujivua gamba umewafikia inawezekana au hawajua maana yake au hawaoni tofauti ya CCM wakiwa na gamba na baada ya kujivua gamba.

Hasira hizi zinasababishwa na msongo wa mawazo ya hali mbaya ya kiuchumi
 
cha msingi hapa ni hawa viongozi wetu wabadilike na wasome nyakati zikoje kwani sasa si ule utawala wa chama kimoja, kama hali ndio ilivyo kama ulivyotuhabarisha basi hiyo ni indicator ya watu kujua kuwa wanataka mabadiliko na si enzi za kuendeshwa kimazoea ya viongozi kudhani wao ndio wako juu ya kila kitu
 
Duh pole sana CCM na watu wako .Iko kazi badilikeni ndiyo mtajua nini maana ya maisha wanayo yataka watanzania wamechoka na ubabaishaji wenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom