Hafla imekwisha na sasa ni kikao kimeanza

de'levis

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
1,222
1,567
Hafla ya kupongezana juu ya kilichotokea jana huko Dodoma imekwisha na sasa kinachoendelea ni kikao cha hatua ya pili ya kukabiliana na mvutano uliopo bungeni miongoni mwa wabunge wenyewe na kuhakikisha baadhi ya wabunge wanadhibitiwa na hawapewi nafasi kusema kile kitakachoonekana kutibua na kuharibu hatua iliyofikiwa(ushindi wa jana) . Maagizo maalumu yametumwa Dodoma kwa spika wa bunge juu ya hatua za kuchukua kwa wabunge walioko katika kamati zinazotuhumiwa kupokea rushwa .

PUMA energy ni kampuni inayomilikiwa na kiongozi mmoja aliyeko serikalini (si kiongozi mdogo) akishirikiana na wenzake 3 wenye hisa katika kampuni hiyo. na si kweli kwamba Serikali ina hisa asilimia 50!!!.

Nitaishia hapa leo na nitasubiri iwapo spika makinda atayatekeleza maagizo yaliyokwenda kwake...
 
Siasa za Tz ni kizungumkututi! Yetu macho. Lkn kama kweli hoja zinazotetewa na Prof. Muhongo, manaibu Waziri wake na KM wake Bw. Maswi ni za kweli, basi juhudi zao ziungwe mkono ili mchwa wanaoitafuna nchi hii waadabishwe. Wasiwasi wangu, wataweza? Maana ni vigogo hasa na familia zao ndio wanaotuhumiwa!
 
Du kwenye hiyo PUMA ndo wamenimaliza maana kuna mchangiaji humu JF 'Mkandara' keshasema hiyo kampuni iliyoinunua BP ni ya kigogo humu nchini, Hivi haya sio makidamakida je/ mgawo wa Umeme ukirudi watatuambiaje hii Wizara?
 
Nimechoka ila tureview hizi propaganda isije ikawa ni za walionyang'anywa ulaji:hat:
 
Siasa za majitaka tu hapo. Kupakana matope na kukomoana na kulinda ulaji.
 
Hapa hata Upinzani utapitia changamoto nzito sana! lakini faida yake ni wanafiki kuwa uchi!!!
 
Tatizo sio hiyo Puma Energy kuwa ya kiongozi wa hapa tanzania, ila inauza mafuta bei nafuu kuliko hizo kampuni zingine,kwani sisi shida yetu c mafuta tuu??
 
Hafla ya kupongezana juu ya kilichotokea jana huko Dodoma imekwisha na sasa kinachoendelea ni kikao cha hatua ya pili ya kukabiliana na mvutano uliopo bungeni miongoni mwa wabunge wenyewe na kuhakikisha baadhi ya wabunge wanadhibitiwa na hawapewi nafasi kusema kile kitakachoonekana kutibua na kuharibu hatua iliyofikiwa(ushindi wa jana) . Maagizo maalumu yametumwa Dodoma kwa spika wa bunge juu ya hatua za kuchukua kwa wabunge walioko katika kamati zinazotuhumiwa kupokea rushwa .

PUMA energy ni kampuni inayomilikiwa na kiongozi mmoja aliyeko serikalini (si kiongozi mdogo) akishirikiana na wenzake 3 wenye hisa katika kampuni hiyo. na si kweli kwamba Serikali ina hisa asilimia 50!!!.

Nitaishia hapa leo na nitasubiri iwapo spika makinda atayatekeleza maagizo yaliyokwenda kwake...

Nakuheshimu kwa tread zako mkuu
 
Duh! Hizi tamthilia zetu zinavikorombwezo kibao, hivi ile tamthilia yetu ya Ulimboka imeishia wapi? Uzuri wa hizi tamthilia ni kuwa zimejaa mazingaombwe yaani mpaka watazamaji tumechanganyikiwa tunashindwa kujua starring ni nani na adui ni nani
 
Da yani watu wanapiga hela mpaka mtu unachanganyikiwa. Mi nafikiri hatuhitaji mawaziri, wabunge wala madiwani, ikibidi hata rais na haya mavyama. Tuwe na CEOs, usalama wa taifa imara, pccb na polisi imara. Hizi longolongo zote zitaisha. Hawa politicians hawa wanatufilisi tu.
 
Back
Top Bottom