hAdItHi nZuRiiiii....nLiYoIpA kiChWa::MJINI SI SHULE Tu!!!

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Unatoka kazini ukiwa
umechoka na kazi ngumu
za ofisi zisizoisha. Umeamua
kwenda karibu na kituo
cha daladala ili ujirudie zako
nyumbani. Nyumbani ni mbali, muda unazidi
kwenda na hakuna dalili ya
daladala kuja mapema.
Unaamua kutembea kidogo
ili daladala ikukutie njiani.
Ukiwa unatembea kwa uchovu unaotokana na
uzito wa begi la laptop
uliyoibeba na mawazo
chungu mzima kuhusu
familia na kazi, mara mbele
yako kidogo inasimama gari ndogo mpya kabisa
ikiwa tinted! Kioo kinashuka na
unamwona msichana
mrembo anachungulia na
kukusemesha “Mambo
kaka”, ukiwa bado
kwenye mshtuko mkubwa wa kusalimiwa na msichana
huyo mwenye tabasamu la
haja, unaitikia kwa
kujiumauma, “aah poa tu
dada”. “Unaelekea wapi
kwani?”Anakuuliza tena kwa sauti ile ile yenye
mvuto na inayosindikizwa
na tabasamu toka kwa
msichana anayeonekana
kutojua maana ya neon
‘shida’. Ukiwa umeanza kujiamini
kidogo unamwambia
unakoelekea. Anakuambia
yeye anaenda mbele ya
huko uendako na
angependa akusogeze. Kimoyo moyo
unajiongelesha “hili zali” na
kutojiuliza mara mbilimbili.
Unazunguka upande wa pili
wa gari na unaingia ndani.
Unapoingia ndani unakutana na halufu nzuri
ya perfume ya Beyonce
Pulse! Halufu yake na
mchanganyiko wa AC ya
ndani ya gari lake
inakupeleka paradise inayojengwa kwa muda
mfupi ndani ya mawazo
yako mwenyewe. Anakuangalia kwa upole
na kuisafisha siti
unayotakiwa kukaa na
kukukumbusha kufunga
mkanda. “Unaonekana
umechoka sana kaka, pole na kazi” Anakusemesha
huku macho yake yakiwa
mbele kutokana na
kuiondoa gari la kuanza
safari. Ukiwa bado
unautafakari urembo wake kama wa malaika unamjibu
“Asante”. Anakuambia
huna haja ya kukaa na begi
lako miguuni na unaamua
kuliweka kwenye siti za
nyuma ya gari. “Unaitwa nani” anakuuliza
kwa tabasamu lingine
linalokufanya ugundue
kumbe anabonyea shavuni
pia. Unashangaa ukijikuta
unaingiwa na woga tena, unamjibu kwa kumwambia
majina yako yote mawili
lakini macho yako yakiwa
yametazama katikati ya kiti
chake na chako ambako
kumewekwa simu mbili za gharama kabisa, iphone 4s
nyeupe na Samsung
GALAXY S II nyeusi. “Mimi naitwa Lynette”,
anajitambulisha kwako.
Unamwambia jina lake zuri
na mnacheka kwa pamoja.
Baada ya dakika kama
kumi na tano ya safari yenu mnajikuta mmezoeana
sana. Anakupa story zake
na wewe unampa zako na
vicheko vinatawala ndani
ya gari. Mnafika sehemu kuna
maduka kadhaa na
anakuambia kiu
kimemkaba sana na
ameshindwa kuvumilia.
“Samahani George naomba unichukulie maji makubwa
ya Kilimanjaro hapo mbele”.
Anakupa shilingi 2,000 na
unaonesha kufurahia
kutumwa maji na msichana
mrembo kama yeye. Unaenda dukani. Unapofika
unanunua maji kama
anavyotaka lakini
unajishauri ununue kitu
kingine kidogo tu kama
surprise kwake na kuonesha shukrani kwa
wema na uchangamfu
wake kwako. Unaamua
kununua chocolate za
shilingi 5,000. Unarudi pale
mlipoegesha gari lakini unashangaa hulioni! Baada
ya dakika kama kumi
unagundua kuwa
ameshaondoka na tayari
umetapeliwa!!!!
 
quite interesting mkuu.
Ntakuwa natembea na maji kwenye begi, ili kusiwe na haja ya kushuka.
Just kidding.

bampami,
Hili ni somo, na limetufikia haswa.
Si ajabu hata namba hakuisoma.
 
Last edited by a moderator:
Duh laptop ndo itakuwa imeota miguu hapo kama c kosei teah ameula wa chuya hapo na bdo buku5 kanunulia cju choklate dah. Kaz kweri kweri.
 
quite interesting mkuu.
Ntakuwa natembea na maji kwenye begi, ili kusiwe na haja ya kushuka.
Just kidding.

bampami,
Hili ni somo, na limetufikia haswa.
Si ajabu hata namba hakuisoma.

Nafikiri kwa wale wenzangu na mimi, ambao hawapata usafiri hii inawahusu sana, coz hutegemea daladala na lift toka kwa jamaa/marafiki zaö na hapo utapeli huu waweza kutokea pia.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom