hadithi hadithi...???

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Hapo zamani kuku na mwewe walikuwa marafiki. Siku moja kuku akaenda kuazima sindano ya kushona nguo kwa mwewe iliyokuwa ikitumiwa na ukoo mzima wa mwewe.
Kwa bahati mbaya ile sindano ikapotea. Mwewe alikasirika sana akataka alipwe sindano yake ya ukoo la sivyo atajilipiza kwa kuchukua vifaranga vya kuku na kupeleka kwenye ukoo wake hadi sindano itakapo patikana. Ndo maana hadi leo kuku anatafuta sindano kwa kufukua fukua kila sehemu ili kuokoa kizazi chake.
Hadithi yangu inaishia hapo. Mia
 
ha ha ha ha....dah kumbe ndio sababu ya kisa cha kuku kufukua chini.....aisee makes sense
 
Figganigga nakupa mji kale Arusha halafu tuletee nyingine bana zile za std 2.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom