Hadi lini?

MR NDEE

Member
Aug 2, 2011
54
21
Ninasema kwa yakini,Ya kweli ya mitaani
Mejitokeza machoni,Sononeko li moyoni
Hawa walio shakani,Lini tatoka tabuni
Mjizigo tumboni,Mateso yao moyoni

Starehe watupatia,Na wana watuzalia
Na ngumi twawapatia,Pekee wajililia
Ulemavu jipatia, Na ndoa wazililia
Mateso yao moyoni,Mijizigo matumboni

Maneno ya kuhadaa,Katu hawatokataa
Tena kwa yao ridhaa,Hapo kati utapata
Utamuona bidhaa,Mimba utaikataa
Mjizigo matumboni,Mateso yao moyoni

Na wale macho mekundu,Ni wale vibibi vizee
Wanao shikiwa mundu,Eti wachawi wazee
Tena na vijana watundu,Mezaliwa na wazee

Mijizigo matumboni,Mateso yao moyoni
 
Back
Top Bottom