HabariLeo Walamba matapish i- Wajuta kwa uzushi wao, waomba msamaha!

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
Jumapili iliyopita Gazeti 'kubwa' la habari leo waliandika habari iliyolenga kumchafua askofu msaidizi wa TAG ndugu Mhiche na Kanisa kwa ujumla, habari ilikua na heading "Askofu adaiwa kusambaratisha ndoa ya muumini'' ile habari ilikua imejaa uongo mwingi, nilikuja humu jamvini nikaelezea namna naifahamu hiyo story na nikaeleza kuwa kilichoandikwa na HabariLeo kilikua uongo mtupu.

Leo Gazeti limeandika katika ukurasa wake wa kwanza likimuomba radhi askofu na Kanisa kwa sababu 'eti' baada ya kufanya uchunguzi wa kina wamegundua zile shutuma zilikuwa uzushi.

Kitendo cha HabariLeo kuomba msahama ni cha kiuungwana lakini bado nina shida mbili.

1. Si kweli kwamba HabariLeo walijua kuwa hizo habari ni uzushi, Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba HabariLeo walijua kabisa kwamba zili shutuma 'eti kanisa lakubwa na kashfa ya ngono' ulikua ni uongo na bado wakaendelea kuzichapa, HILI NI KOSA KUBWA!

2.Ni jukumu la gazeti kupata ukweli wa story kabla ya kuchapisha gazetini, usumbufu uliosababishwa kwa askofu mhiche na kanisa la TAG hauwezi kufutika tu eti kwa habari leo kuandika kuomba msamaha leo wakati uzushi umeenea kwa wiki nzima, UELEDI (Professionalism) unailazimisha HabariLeo kuwa na uhakika na kila wanachoandika, habari ile ingeandikwa na magazeti ya udaku labda isingekuwa na damage kubwa namna ile. Kuchapa Habari afu 'kama wanavodai wao' kufanya uchunguzi badae ni KOSA KUBWA ZAIDI.

Najua Askofu Mhiche amesamehe, na hii ni kutokana na imani yake, lakini Uzembe kama huu sitegemei HabariLeo mtauacha upite kimya kimya, nasubiri kusikia hatua zilizochukuliwa kwa wale waliohusika kutoa habari ya uongo kwa kiasi hiki, habari ambayo hata angepewa mtoto wa form two kufanyia uchunguzi angebaini kwamba kulikua hakuna chembe ya ukweli
 
HabariLeo mimi silisomi siku hizi! Yaani utafikiri si gazeti la Serikali bali la Chama (Magamba)! Kuna wakati liliandika habari za Kanisa Katoliki Sumbawanga utafikiri wana chuki na Ukristo! Huyu JK wetu anaipeleka nchi pabaya bila kujijua!
 
HabariLeo mimi silisomi siku hizi! Yaani utafikiri si gazeti la Serikali bali la Chama (Magamba)! Kuna wakati liliandika habari za Kanisa Katoliki Sumbawanga utafikiri wana chuki na Ukristo! Huyu JK wetu anaipeleka nchi pabaya bila kujijua!

Sasa hii aibu wataificha wapi?
 
ulikua uzushi tu, sasa wanajuta

And no compromise in this issue, this is a war against crusaders. Huyu JK mwache tu aendelee kutalii lakini hizi chokochoko za kuwavunjia heshima maaskofu dawa yake inachemka.
 
Back
Top Bottom