Habari zisizokuwa rasim Pesa ya Mpya ya BOT Imeibiwa Airport!!

Hii ni mwendelezo wa deal chafu.Kama ni kweli this time somebody has to step down.Tumechoka na michezo ya kuigiza inayotuumiza!
 
Ziko mtaani zinatakatishwa. Kuna watu wanaziuza kwa dola, wapo tayari kutoa 1994 wakati dola kwa tsh ni 1960-70??? Usiniulize nimepata wapi taarifa hizi maana bado nazifanyia kazi.
 
Ziko mtaani zinatakatishwa. Kuna watu wanaziuza kwa dola, wapo tayari kutoa 1994 wakati dola kwa tsh ni 1960-70??? Usiniulize nimepata wapi taarifa hizi maana bado nazifanyia kazi.

:hungry::hungry:
 
Wazee sasa kama tunaanza kudanganyana wenyewe kwa wenyewe wanajamvi sio poa..... hebu mkuu leta details zaidi kuhusu hii tetesi sababu apart from hapa jamvini sijaisikia pengine..... Je hizi fedha ziliibiwa lini?
 
Kuna ukweli kuwa pesa mpya ya BOT imeibiwa Airport je kuna mwenye ukweli huu??

aisee mbona unatuchanganya, kwanza unasema kuna ukweli, kisha unasema mwenye ukweli alete. Ok, toa chanzo au fafanua kudogo.
 
Ziko mtaani zinatakatishwa. Kuna watu wanaziuza kwa dola, wapo tayari kutoa 1994 wakati dola kwa tsh ni 1960-70??? Usiniulize nimepata wapi taarifa hizi maana bado nazifanyia kazi.

maane, hiyo eksichenji reti umeipata wapi?
 
Jamani hizi siyo tetesi ni za kweli nimeshazina zaidi ya x2 ila hazijawekwa official kwa kutamkwa na wenyewe kama tulivyozoea linafichwa sana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa uzembe wao na kulinda maslahi ya serikali iliyoko madarakani ila nilivyozipata mimi kwenye wikiliki ya minazini ni kuwa ni billioni kumi tu wenye habari zaidi kwa uhakika hasa walioko maeneo ya JKN. Watujuze jamvini jamani

Kumbuka kuwa kama ni kweli za BoT matumizi yake yatakuwa magumu kidogo kutokana kuwa na Namba za pesa hizo maana watakuwa na uwezo mkubwa kuzitrack kwenye mzunguko wa kawaida lakini kama kuna ufisadi hapo watanyamaza hatatangaza na zitaingia kwenye mzunguko kama kawaida then Tanzania nakupenda kwa moyo wote.


Hapo kwenye red pamenistua sana yaani billion kumi tunaziona kitu kidogo!!!! Kweli ufisadi wa EPA, DOWANS, KAGODA, MAJENGO PACHA YA BOT umetuharibu kiasi kwamba shilingi billion kumi tunaziona ni kitu kidogo!!!!! ni billion kumi tu!!! Ufisadi ni ufisadi tu haijalishi ni wa shilling ngapi.
 
Nijuavyo mimi kuhusu usafirishaji wa fedha,
1.Fedha mpya zilishakuja kwa meli, makontena kwa makontena, sinateremshwa usiku, zinasafirishwa usiku, ulinzi usipime!.
2. By the time, fedha zinatangazwa, zilishafika long time, there is no way zikaibiwa njiani.
3. Nimetokea kushuhudia clearance fulani ya contena la fedha mpya za BOT pale bandarini, hiyo shughuli yake, siamini zitaibiwaje.
Hata hivyo.
4. Niwewahi kusafiri njia moja na malozi makubwa matatu ya fedha, yakizipeleka Dodoma kwa wabunge kabla bunge halijavunjwa.
5. Gari hizo tatu ni za heavy metal, fire proof na bullet proof.
6. Zimetanguliwa mbele na Sweep car ya kingo'ra kuyaomba magari yapishe njia.
7. Nyuma ya gari ya kingora, kuna security car ya vioo vyeusi bullet proof, ndani wamekaa makomandoo wakiwa stand by na AK-47.
8. Ndipo hufuata hayo malori matatu yakifuatana huyu yakienda kwa mwendo kasi na nyuma husindikizwa kwa security car nyingine ya jamaa wa AK-47
9. Lengo ya hayo yote ni kuhakikisha usalama wa fedha, ila nilichoshuhudia, kwa vile BOT haikuwahi kukumbwa na tukio lolote la wizi wa fedha,
wahusika wote wa zoezi zima la usafirishaji wa fedha, wako relaxed wakati wate, hivyo kwa technics ndogo tuu kama za kwenye action movies, hizo fedha on transit zinaweza kuibiwa kwa urahisi kuliko hata ule wizi wa kwenye sinema.
10. Pamoja na uwezekano yote haya, na mimi binafsi nilivyokatisha katisha corridors za BOT kwenye yale maandalizi ya lile tangazo la BOT kuhusu noti mpya, naamini ningesikia, tuu, lakini kwa vile sikusikia chochote, siamini kama kuna kitu kama hiki, ila all and all, nothing is imposible under the sun, you never know!.
Pasco

Mkuu kama ulivyoambiwa hapo juu vyombo vya habari tayari vilishatangaza huo wizi na mpaka sasa hakuna aliyekanusha. Kama watu wanakanusha mpaka taarifa za kweli za wikileaks ndio sembuse washindwe kukanusha hii?

Wizi hauongelewi kwenye corridors hata siku moja.
 
Back
Top Bottom