Habari zisizokuwa rasim Pesa ya Mpya ya BOT Imeibiwa Airport!!

Ninavyojua mini ni kwamba fedha inapoingia nchini from kiwanda haiwezi tumika kwa namna yoyote labda tu (only and only if) kwa msaada wa wajanja BOT. Maana inapingia nchini inapita katika mikono zaidi ya mitano ili ipate go ahead na wote wana special and secret signs. Sasa sijui mm nnachojua ndivyo ilivyo au nliongopewa ila nasisitiza Ujambazi huo wa kimafia haukubaliki. Swala la kuibwa airport inawezekana maana kuna siku pale Flamingo canteen watu waliwekwa mtu kati mchana kwupe soon after lunch hours zikaondoka 30 miln.
 
NI KWELI KUNA ELA ZIMEIBIWA Tsh bil 10 ila wamesema HAWAJUI ZIMEPOTEAJE hii ilitangazwa radioni wiki iliyopita Lakini wameficha ukweli jinsi izo ela zilivyopotea kimazingira
 
HIvi hii nchi kabakia kuuwawa rais tu na mafisadi, haiwezekani kabisa 10bill ziibiwe katika mazingira ya kibabaishaji namna hiyo kama kuna ukweli. Ngiojeni muda mfupi ujao utasikia kiongozi fulani lakini wauwaji hawajulikani. Kupingana na ufisadi ni kugumu kuliko hata kukemea pepo wachafu 10mill!!!!!!!!
 
Yeah, nikweli chief, Ililripotiwa na vyombo vya habari kuwa Bil 10 zimepotea ktk mazingira yanayoashiria kuwa yameibiwa Airport wakati zikiingizwa kutokea Uswis. Pia hivi karibuni Kontena lililojaa Antiretroviral Drugs I.e ARVs zilizotolewa kama msaada kutoka marekani nalo limepotea ktk mazingira kama hayo. Na kwa kuwa mpaka hii leo hawajakanusha, tunaamini kuwa ni kweli vitu hivi vimetokea.
 
Kama kweli naowamba wataalam wa kuandamana kuitetea nchi zingine kama palestina na kwingine, muingie hapa na kuitisha maandamano nchi nzima,kama kweli hiii ni hatari sana
 
Mhhh ikibainika kama ni kweli jamani mbona ni hatari..... hakuna atakayekubali that stupidity!!! TUMECHOSHWA!!
 
Mh!!! Hizo zinaitwa kazi za ndani.
Kagoda na meremeta wamerudi kwa style nyingine maana wameona watu mnachonga sana.
 
Huwezi kuiba 10 and remain unnoticed!! hizo ni pesa nyingi na ni mzigo mkubwa wa lori zima..kama ni kweli basi walizipeleka ktk election tu then wanaripoti theft transit insuarance icover
Jinsi wanavyozipokea kwa makeke utaibaje..na ukiteka lile gari la BOT halifunguki na ni fire proof
 
Ujanja ni kughairi mpango wa kutumia noti mpya, tuone watazitumia wapi!
 
Kuna ukweli kuwa pesa mpya ya BOT imeibiwa Airport je kuna mwenye ukweli huu??

Kwani tatizo liko wapi mbona hata mimi jana nimeibiwa pesa ya zamani Tshs 2000. Au ulitaka umaanishe mitambo ya kutengenezea pesa mpya
 
Wakuu mbona mnaonekana mna taarifa,lakini hamtaki kutujuza vizuri?
Siunajua govana ninani??ukitaka habari za huakika Kama uko dar BOT Hipo sokoine drive nekitengo cha habari kuna afisa uhusiano pale atakupa deep news.
 
Huwezi kuiba 10 and remain unnoticed!! hizo ni pesa nyingi na ni mzigo mkubwa wa lori zima..kama ni kweli basi walizipeleka ktk election tu then wanaripoti theft transit insuarance icover
Jinsi wanavyozipokea kwa makeke utaibaje..na ukiteka lile gari la BOT halifunguki na ni fire proof
Ndo maana nasema kuna something behind sio hilo wanalosema ni wizi au ujambazi wameiba kweupe kabisaaa na hawataki isomeke kwa walipa kodi..
 
Nijuavyo mimi kuhusu usafirishaji wa fedha,
1.Fedha mpya zilishakuja kwa meli, makontena kwa makontena, sinateremshwa usiku, zinasafirishwa usiku, ulinzi usipime!.
2. By the time, fedha zinatangazwa, zilishafika long time, there is no way zikaibiwa njiani.
3. Nimetokea kushuhudia clearance fulani ya contena la fedha mpya za BOT pale bandarini, hiyo shughuli yake, siamini zitaibiwaje.
Hata hivyo.
4. Niwewahi kusafiri njia moja na malozi makubwa matatu ya fedha, yakizipeleka Dodoma kwa wabunge kabla bunge halijavunjwa.
5. Gari hizo tatu ni za heavy metal, fire proof na bullet proof.
6. Zimetanguliwa mbele na Sweep car ya kingo'ra kuyaomba magari yapishe njia.
7. Nyuma ya gari ya kingora, kuna security car ya vioo vyeusi bullet proof, ndani wamekaa makomandoo wakiwa stand by na AK-47.
8. Ndipo hufuata hayo malori matatu yakifuatana huyu yakienda kwa mwendo kasi na nyuma husindikizwa kwa security car nyingine ya jamaa wa AK-47
9. Lengo ya hayo yote ni kuhakikisha usalama wa fedha, ila nilichoshuhudia, kwa vile BOT haikuwahi kukumbwa na tukio lolote la wizi wa fedha,
wahusika wote wa zoezi zima la usafirishaji wa fedha, wako relaxed wakati wate, hivyo kwa technics ndogo tuu kama za kwenye action movies, hizo fedha on transit zinaweza kuibiwa kwa urahisi kuliko hata ule wizi wa kwenye sinema.
10. Pamoja na uwezekano yote haya, na mimi binafsi nilivyokatisha katisha corridors za BOT kwenye yale maandalizi ya lile tangazo la BOT kuhusu noti mpya, naamini ningesikia, tuu, lakini kwa vile sikusikia chochote, siamini kama kuna kitu kama hiki, ila all and all, nothing is imposible under the sun, you never know!.
Pasco
 
Kama taarifa hii itatokea kuwa ya kweli itatakiwa isomeke hivi: "Pesa mpya zilizokuwa zikiingizwa nchini zimechukuliwa kinyemela".
Kwa kuwa haingii akilini kwamba fedha ambazo hulindwa kwa ulinzi mkali vile kutoka benki kuu kwenda mikoani halafu kutoka kiwandani kwenda BOT kwenyewe zoezi liwe hoi kiasi hicho, nasisitiza haiwezekani.

Pia kama ni kuibiwa kwa mbinu bado kuna hitaji ushirika wa kila aliyehusika na somo hili kwa sababu wataalamu wa noti watakapotueleza kwamba yale maboksi ambayo tunayafahamu ambamo huhifadhiwa pesa huwa na na uwezo wa kutunza kiasi gani cha pesa mpaka ifike mtu afanikishe zoezi la kutoweka na 10bn si bure baraka za waheshimiwa ni lazima ziwepo.

Hakuna bahati mbaya hapo kila kila kitu kilipangwa kabla na hata washirika wote askari, maofisa wa benki na hata wadau wa airport wana ufahamu mpango huu na wana mgao.

Kweli bongo tambarare.
 
Labda mkuu angesema hizi tetesi kazipata wapi na ni jinsi gani anaamini hiyo source yake...
 
Back
Top Bottom