Habari za kale na Ally Saleh: Zanzibar yataka Nyerere mwengine

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
1610
2009​
Na Ally Saleh

Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kuwa kipenzi kikubwa sana cha wananchi wa Zanzibar. Na hilo ni kwa sababu nyingi ambazo kwa ukweli au dhana walizihusisha nae. Kama ningeruhusiwa kuwasemea Wazanzibari nigethubutu kusema kuwa Nyerere hakuliliwa sana wakati alipofariki kama vile ambavyo watu hawakutaka kumfurahia wakati wa uhai wake.

Lakini hii haina maana kabisa kuwa Nyerere hakuwa na heshima mbele ya Wazanzibari. Ukweli ni kuwa heshima yake ilikuwa ni ya hali ya juu kwa sababu wengi walimuona kuwa ni mtu mwenye uwezo sana wa kujenga hoja na ambaye daima hakuogopa kusema fikra zake wakati akiwa kwenye siasa na nje ya siasa.

Wanajua pia mchango wake katika suala zima la kuunganisha watu wa Zanzibar kupigania uhuru wao. Yeye ni chanzo kikuu kilichopelekea kuundwa au tuseme kuunganisha nguvu za Shirazi Association na African Association na kuzaliwa Afro Shirazi.

Binafsi wakati mmoja nilishangaa mwaka 1985 nilipopata maagizo kuwa Mwalimu ametaka kupata maelezo kutoka kwangu kuhusiana na taarifa niliokuwa nimeitoa kwenye Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC. Taarifa hiyo ni kuwa Wazanzibari walikuwa wanapendelea Rais wa Zanzibar Ali Hassan Mwinyi abakie kuwa Rais wa Zanzibar na asiende kushika wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Wakati huo ilikuwa tayari minon'gono ilikuwepo kuwa Mwinyi anaandaliwa kuwa Rais wa Muungano na ilhali alikuwa kipenzi cha Wazanzibari kwa hatua zake ambazo zilikuwa zimeanza kuifungua Zanzibar kibiashara na kiuwekezaji, lakini muhimu zaidi kwa Wazanzibari ilikuwa ni kurudishiwa uhuru wa maoni na haki za binaadamu.

Hivi kwa Wazanzibari ndivyo alivyokuwa Mwalimu kuwa hakuweza kuacha kitu chochote kile bila ya kukiulizia na kama si kukiulizia basi kukisema na zaidi ya hapo hata kukikemea. Na mifano ya hiyo iko mingi sana ingawa mara mbili tatu aliwaangusha Wazanzibari kwa baadhi ya mambo kuyaachia na kutishia hata uhai na usalama wa Zanzibar .

Nyerere hakuwa mkali au tuseme alikuwa mzito wa kumgomba au kumkosoa Rais Abeid Karume na wengine tunaamini ni kwa sababu kwa wakati ule alikuwa anataka Zanzibar ibakie katika Muungano wa Tanzania kwa gharama yoyote ile.

Maana Nyerere hakutoa sauti yake wakati wananchi walipokuwa wakichukuliwa usiku usiku na kupotea, wala Karume alipokuwa akiwamaliza viongozi wenzake na wala Karume aliposimamia zoezi la ndoa za lazima hasa dhidi ya Waasia wa Kizanzibari.

Lakini pia Nyerere alikuwa kimya kwa sera nzuri za Zanzibar kama elimu bila malipo, afya kwa wote, maji kwa wote na hata suala la kupewa ardhi wananchi, pamoja na makosa yake, hakuwa akiziunga mkono na kuzipa nguvu stahiki. Nyerere hakuonekana kusaidia kuhimiza mafanikio hayo na tuseme mpaka anaondoka la Zanzibar lilikuwa la Zanzibar na la Tanganyika la Tanganyika.

Tulimuona Nyerere aliyebadilika baada ya kuundwa kwa CCM na pengine ndio maana hakuwa na sauti wakati Afro Shirazi Party ilipokuwa hewani, ila baada ya kuja kwa CCM Nyerere alisogea karibu zaidi kukemea matukio ya Zanzibar na kwa hilo ndilo ambalo Wazanzibari watamkumbuka Nyerere.

Wengi tunakumbuka Nyerere alipokuwa mtu wa mwanzo kabisa kusema kuwa njia bora kabisa ya Zanzibar kukabili uwili wake wa siasa, maana siasa za Zanzibar ni uwili wa CUF/CCM ni kuundwa kwa Serikali ya pamoja, lakini wakati huo Dk. Salmin Amour alikataa kabisa wazo hilo .

Pengine kwa wakati ule sauti ya Nyerere haikuwa kubwa kwa sababu mabaki ya Afro Shirazi Party yalikuwa bado yana nguvu na kwa hakika wengine kati yao walikuwa na uchungu wa Nyerere kuingilia kuizuia Zanzibar isiwe na uhuru wa kuwa na ushirikiano wa kimataifa kupitia Jumuia ya Kiislamu (OIC).

Na hatujasahau mbele ya Nyerere mabaki ya Afro Shirazi yaliposimama kidete kumkataa Salim Ahmed kuwa Rais wa Zanzibar na mawazo kama hayo ya kuwa Mpemba na Muarabu hatawali Zanzibar kwa hakika mpaka leo yapo na yanapepea.

Kwa kupinga wito wa Mwalimu kufanya serikali ya pamoja Zanzibar ilikosa fursa muhimu sana ya kutandika msingi mzuri wa siasa za ushindani kwa kuendekeza mawazo kuwa kwa mujibu wa siasa za Zanzibar hasa kwa jicho la kihistoria basi vyama vya CUF na CCM haviwezi kuwa na serikali ya pamoja – ilhali vyama kinzani zaidi duniani tumeona vimeweza kufanya hivyo na mfano wa karibu ni huko Zimbabwe.

Naamini kama Nyerere angekuwapo basi asingekubali kabisa kuundwa kwa makundi ya vijana yaliyopewa jina la Janjaweed ambayo kila kipindi cha uchaguzi hupewa satwa kubwa kufanya kila watakalo katika kuviza demokrasia na kujenga mazingira ya nguvu ya kukipa ushindi Chama cha Mapinduzi Zanzibar. Na pia asingeridhi kabisa kwa vyombo vya dola kuonekana wazi wazi kulalia kwa upande wa chama tawala.

Nyerere katu asingekubali kabisa kuwa CCM Zanzibar iko tayari kufanya lolote lile lakini lazima ushindi wa uchaguzi ubakie na zaidi CCM Tanzania Bara ikinyamaza kimya na kubariki matendo hayo, yawe ni ya kupandikiza wapiga kura na kufanya ghilba mbali mbali.

Angekuwepo Mwalimu asingefurahi kabisa kuona Wapinzani wanafikia mpaka kufanya matumizi ya nguvu kama vile uripuaji wa baruti, ususiaji wa vikao vya Baraza la Wawakilishi na kukataa kushirikiana na Serikali.

Mwalimu angekuwepo angekasirika sana kuona nchi hii sasa inagawanyika kwa ugomvi wa rasilmali kama vile suala la mafuta, mgawano wa michango ya wafadhili na hata namna ambavyo uchumi wa Zanzibar unavyokabwa koo kwa taasisi kama Mamlaka ya Kodi (TRA) isivyokuwa na huruma kabisa kwa visiwa hivyo.

Naamini kuwa Mwalimu angekuja Zanzibar mara nyingi kadri ambavyo ingewezekana lakini asingekubali suala la Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi liwe kidonda kwa chama chake na hata Serikali za Zanzibar na Tanzania na kuhakikisha kuwa misingi ya demokrasia iliyowekwa ya kuwa kila raia anaweza kupiga kura apate fursa hiyo na sio kuvizwa kwa visingizio vya kukosa cheti cha kuzaliwa au ruhusa ya Sheha.

Kwa fikra zangu naamini kuwa Zanzibar ina vitu kidogo sana vya kumuonyesha Mwalimu na yeye kuweza kuridhika kuwa visiwa alivyoviwacha vimesonga mbele kidemokrasia na kuhakikisha haki, usawa na umoja. Katika sheria hilo limefanikiwa lakini katika uhalisia au ukweli wa mambo hilo liko mbali sana .

Mwalimu hangesita kuikemea Halmashauri Kuu ya CCM, moyo na injini ya chama hicho kwa kubariki ya dhulumati ya kisiasa na kiraia inayoendela Zanzibar. Naamini angekuwa zamani ameshakutana na Rais Kikwete na Rais Karume kuwauliza mbona hawachukui uongozi?

Kama nilivyokuwa nimesema mwanzo kuwa Nyerere hakuwa kipenzi kikubwa cha Wazanzibari. Lakini sasa hivi wanamuhitajia sana maana wanaona wametupwa na Watanzania wenzao kuanzia taasisi za haki za binaadamu na hata wasomi wakubwa wakubwa.

Wanamkumbuka Nyerere kwa sababu jumuia ya kimataifa inaburura miguu kwa sababu wapiga kura hawaandikishwi kwa kisingizio au maelezo ni kwa ajili ya sheria. Si Watanzania wenzao – wasomi na taasisi za haki za binaadamu na wala si jumuia ya kimataifa inayohoji – hivi kweli sheria ambayo inatenga idadi kubwa ya watu kutoweza kupiga kura ina uhalali gani na uchaguzi unaofanywa chini ya msingi huo unaweza kuwa na uhalali gani?

Nyerere asinge nyamza. Angesema, akateta, akahoji mpaka akajua mwisho. Kama wangeweza kumpelekea salamu hizo hii leo kaburini kwake wangempelekea ujumbe wa wazi kabisa: Anaweza kumleta Nyerere mwengine aje awasemee? Asaa pengine atasikilizwa kwa kuwa amemleta yeye.

Lakini sote tunajua haliwezekani. Na ndio maana kumbukumbu ya miaka kumi tokea kufa kwa Mwalimu Nyerere haina maana yoyote ile kwa wengi wa Wazanzibari – hasa wanaoona hivi hivi kuwa nchini mwao wenyewe haki ya kupiga kura haiwezi kupatikana na kwa hivyo kuchagua na kuchaguliwa ni dhana tu kwao lakini haina mashiko.

Chanzo: Mwananchi

Hii ni habari ya Zamani; lakini kwa sababu ya habari zinazoendelea nchini kwetu Zanzibar na Bara; nimeona niitafute niiweke

kama Mchango wa Maoni ya Ali Saleh Miaka iliyopita, anavyoona yeye kuhusu Zanzibar na Muungano.
 
Mmmhh, binadamu walivyo na kumbukumbu fupi subiri uletewe majina mbalimbali 'wanavyomuona', hadi ushangae!
 
Mwalimu angekuwepo angekasirika sana kuona nchi hii sasa inagawanyika kwa ugomvi wa rasilmali kama vile suala la mafuta, mgawano wa michango ya wafadhili na hata namna ambavyo uchumi wa Zanzibar unavyokabwa koo kwa taasisi kama Mamlaka ya Kodi (TRA) isivyokuwa na huruma kabisa kwa visiwa hivyo.
Chanzo: Mwananchi
Ni kweli kabisa habari hii ni ya zamani lakini inawakilisha sana mawazo ya Wazanzibar. Ikumbukwe kuwa Ally Salehe kwa ushirika na Farouk Karimu ndio walioua ligi ya muungano. Iwe kwa mazuri au mbaya ukweli unabaki kuwa huo.

Kwa sasa hivi Ally ni mjumbe wa tume ya kurekebisha katiBa na hivyo mawazo yake bado hayabadilika.
Ally anaushawishi mkubwa sana wa siasa za visiwani na ni 'mwanachama' mtiifu wa CUF. Kama umesoma between the lines amejaribu kuonyesha madhila ya wenye damu za uarab vs wazawa.

Kilichonisukuma niandike ni mtazamo wa Ally kuhusu TRA. Yeye anasema TRA haina huruma na Zanzibar kwa vile inakusanya mapato. Hebu tuangalie kwa uchache sana pesa inazokusanya TRA zimamsaidiaje Mzanzibar

1. Mishahara ya wafanyakazi wa muungano inalipwa na kodi kutoka hazina Dar es Salaam wala si hazina SMZ
2. Mishahara ya wafanyakazi wa SMZ imekuwa na inaendelea kulipwa kutoka hazina Dar es Salaam
3. Wanafunzi wa elimu ya juu kutoka Zanzibar wanalipwa mikopo pamoja na unafuu wa masomo kama Mtanganyika
4.Viongozi wa SMZ wastaafu wanapata mafao kutoka hazina na si hazina SMZ

5. Kubwa zaidi ni kuwa, bidhaa zinazoteremshwa Zanzibar zinaletwa kwenye soko la bara. Endapo Tanzania bara itaacha kukusanya kodi basi TRA haitakuwa na mapato. Hata mimi nitapitishia Zbar ili mizigo iingie bara. Kodi nitakayolipa itabaki Zanzibar na si TRA. Kwa mantiki hiyo ni uzembe naujinga wa hali ya juu kuacha Zanzibar ikusanye mapato kwa gharama za soko la bara. Hapa ni falsafa ya Changu ni changu chako ni chetu.

Ushauri: Ili Zanzibar ifaidi matunda ya kazi za wananchi wake ni wakati sasa ijitoe katika muungano.
Jambo hilo limeungwa mkono na watu wengi wa bara ambao ndio wabeba mzigo.
Tunaomba Wazanzibar wanaoishi Dar es salaam, Tanga, Morogo waandae maandamo kutaka muungano ufe nasi tutawaunga mkono na hakika nitabeba bango langu 'LET ZANZIBAR GO! PACK AND GO ASAP
 
huyu bwana ni mwandishi mzuri ila taarifa zake nyingi hazina utafiti wa kina ni maoni yake binafsi. kwa kipindi nilicho mfahamu mimi huyu ndugu ni agenti wa awtu wanaotaka kuvunja muungano.sijawahi kuona ametoa taarifa yenye muelekeo wa kuupenda muungano hata mara moja.kwa mtazamo wangu yeye alitakiwa aone kuwa wanaofaidika na muungano ni wazanzibar kuliko watu wa bara. na ukweli ni kwamba ukiachilia mbali kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, wanaouhitaji muungano zaidi ni wao kuliko sisi.
 
Ni kweli kabisa habari hii ni ya zamani lakini inawakilisha sana mawazo ya Wazanzibar. Ikumbukwe kuwa Ally Salehe kwa ushirika na Farouk Karimu ndio walioua ligi ya muungano. Iwe kwa mazuri au mbaya ukweli unabaki kuwa huo.

Kwa sasa hivi Ally ni mjumbe wa tume ya kurekebisha katiBa na hivyo mawazo yake bado hayabadilika.
Ally anaushawishi mkubwa sana wa siasa za visiwani na ni 'mwanachama' mtiifu wa CUF. Kama umesoma between the lines amejaribu kuonyesha madhila ya wenye damu za uarab vs wazawa.

Kilichonisukuma niandike ni mtazamo wa Ally kuhusu TRA. Yeye anasema TRA haina huruma na Zanzibar kwa vile inakusanya mapato. Hebu tuangalie kwa uchache sana pesa inazokusanya TRA zimamsaidiaje Mzanzibar

1. Mishahara ya wafanyakazi wa muungano inalipwa na kodi kutoka hazina Dar es Salaam wala si hazina SMZ
2. Mishahara ya wafanyakazi wa SMZ imekuwa na inaendelea kulipwa kutoka hazina Dar es Salaam
3. Wanafunzi wa elimu ya juu kutoka Zanzibar wanalipwa mikopo pamoja na unafuu wa masomo kama Mtanganyika
4.Viongozi wa SMZ wastaafu wanapata mafao kutoka hazina na si hazina SMZ

5. Kubwa zaidi ni kuwa, bidhaa zinazoteremshwa Zanzibar zinaletwa kwenye soko la bara. Endapo Tanzania bara itaacha kukusanya kodi basi TRA haitakuwa na mapato. Hata mimi nitapitishia Zbar ili mizigo iingie bara. Kodi nitakayolipa itabaki Zanzibar na si TRA. Kwa mantiki hiyo ni uzembe naujinga wa hali ya juu kuacha Zanzibar ikusanye mapato kwa gharama za soko la bara. Hapa ni falsafa ya Changu ni changu chako ni chetu.

Ushauri: Ili Zanzibar ifaidi matunda ya kazi za wananchi wake ni wakati sasa ijitoe katika muungano.
Jambo hilo limeungwa mkono na watu wengi wa bara ambao ndio wabeba mzigo.
Tunaomba Wazanzibar wanaoishi Dar es salaam, Tanga, Morogo waandae maandamo kutaka muungano ufe nasi tutawaunga mkono na hakika nitabeba bango langu 'LET ZANZIBAR GO! PACK AND GO ASAP

Kwanini msijitoe nyinyi? muungano ni wa nchi mbili. Unataka wenzakao wakale marungu ya FFU? anza wewe, huku kwenu, wao wageni tu.
 
Kwanini msijitoe nyinyi? muungano ni wa nchi mbili. Unataka wenzakao wakale marungu ya FFU? anza wewe, huku kwenu, wao wageni tu.
Nchi zipi wakati Zanzibar wanasema ni koloni letu. Hivi anyepaswa kutoka katika koloni na mkoloni nani anapaswa kuwa na jitihada! Endapo hamjitoi basi mkae kimya!
 
Kwanini msijitoe nyinyi? muungano ni wa nchi mbili. Unataka wenzakao wakale marungu ya FFU? anza wewe, huku kwenu, wao wageni tu.

zomba, kwani ni nani anayesema anaonewa kwenye huu muungano? Tanganyika au Zanzibar? Nani ameenda UN kuupinga muungano? Anayedhulumiwa na kuonewa si ndio aanze zake. Imefika wakati muafajka sasa kuliko kuendelea kupiga kelele, jamani nendeni zenu. Tanganyika kwa ukubwa na raslimali zake kamwe hatutakosa chochote kwa kuondoka Zenj...mwenye macho haambiwi ona!
 
Last edited by a moderator:
Tuache kupiga piga kelele tunapoteza muda. Actions speak louder than words.
 
Nchi zipi wakati Zanzibar wanasema ni koloni letu. Hivi anyepaswa kutoka katika koloni na mkoloni nani anapaswa kuwa na jitihada! Endapo hamjitoi basi mkae kimya!

MImi naona ni kinyume chake. Ikiwa mlolongo wa huduma ulizozitaja unapelekwa Zanzibar wakati wao wamekaa, huoni kuwa wao ndio waliotutawala? hatuna nchi, wenzetu wanayo, hata Tanganyika yetu wameimeza. Leo wao wamekuwa koloni? Fikra za kinyumenyume hizo.
 
Naamini kama Nyerere angekuwapo basi asingekubali kabisa kuundwa kwa makundi ya vijana yaliyopewa jina la Janjaweed ambayo kila kipindi cha uchaguzi hupewa satwa kubwa kufanya kila watakalo katika kuviza demokrasia na kujenga mazingira ya nguvu ya kukipa ushindi Chama cha Mapinduzi Zanzibar.
Ningefurahi kama Ally Saleh ataandika pia kuhusu "kuundwa kwa makundi ya vijana yenye jina la UAMSHO".
 
zomba, kwani ni nani anayesema anaonewa kwenye huu muungano? Tanganyika au Zanzibar? Nani ameenda UN kuupinga muungano? Anayedhulumiwa na kuonewa si ndio aanze zake. Imefika wakati muafajka sasa kuliko kuendelea kupiga kelele, jamani nendeni zenu. Tanganyika kwa ukubwa na raslimali zake kamwe hatutakosa chochote kwa kuondoka Zenj...mwenye macho haambiwi ona!

Mkuu Ndahani kwa taarifa yako Zombi ni Mzenji
 
Kuna kile chama Chenu Cha UAMSHO ambacho Nape anakiita cha MAJAMBAZI kitusaidie

CHADEMA msimamo wao upi katika hili suala maanake nimewasikia Uamsho na kauli za kichadema "mpaka kieleweke" - Sheikh Farid, Uamsho Zanzibar.
 
CHADEMA msimamo wao upi katika hili suala maanake nimewasikia Uamsho na kauli za kichadema "mpaka kieleweke" - Sheikh Farid, Uamsho Zanzibar.

Mhe. Zomba,

Kwa Sheikh Farid kusema "mpaka kieleweke" kunaonyesha tu kwamba anajua lugha yetu ya kitaifa ya Kiswahili. Hakuonyeshi yeye ni MwanaChadema mwenzetu, ingawa kama ni raia ana haki na uhuru wa kuomba kuwa mwanaCDM.

Sikuwa namfahamu huyu Sheikh mpaka alipojitokeza akiongoza hiki Kikundi cha Uamsho, labda kwa vile sio miongoni mwa Viongozi wa CDM Zanzibar. Hata hivyo tuna vigezo vya raia mwanachama kuchaguliwa kuwa kiongozi CHADEMA.
 
"Mpaka kieleweke" - Sheikh Farid, Uamsho Zanzibar.

Hata yule mwana chadema wa Zanzibar aliyekuwa pamoja na Tundu Lussu wakihojiwa katika kipindi cha pima joto cha ITV wiki iliyopita alikiri kuwa ni mfuatiliaji mzuri wa Mikutano ya Uamsho na kila apatapo fursa huwa anahudhuria.
 
Back
Top Bottom