Mshama wa SIKONGE?....
Nsesi,
Sitaki kuendeleza malumbano. Ni ukweli mtupu kwamba Prof. alimuunga mkono Dr. Mwakyembe 2005. Lakini pia ni ukweli mtupu kwamba prof. sio mjinga hakutumbukiza kichwa kichwa kwenye siasa za Kyela kama ambavyo hakufanya kwenye siasa za Mbeya. Pia ni ukweli mtupu kwamba Prof. Mwandosya ni kingmaker wa siasa za mkoa wa Mbeya.
Pia ni ukwelui mtupu kwamba Kyela inategemea baadhi ya mambo toka Rungwe wakati ilitakiwa kuwa kinyume. Hali ya hewa ya Kyela ni nzuri zaidi lakini hata mboga za majani zinaletwa toka Rungwe.
Hapo mjini penyewe, biashara zimeshikwa na wageni wakati sisi wenyeji tunapiga domo. Hayo ndio mambo ya kushughulikia na sio kuelezea mapato ya halmashauri. Hayo mapato si yanaletwa na watu wanaochapa kazi wakiwemo wengi kutoka nje ya Kyela?
Unaweza kuukataa ukweli lakini ndio hivyo. Kyela tuko nyuma sana mkuu. Mimi naijua Kyela kuliko unavyodhani na inanisikitisha sana kuona huo umaskini wa kutisha huko vijijini wakati resources zipo kibao. Ninawaelewa vijana wa Kyela hapo mjini, ni maneno tu na majungu mengi ya kisiasa badala ya kuchangamkia kazi. Afadhali hata dada zetu angalau wameanza kuamka na kujifunza toka kwa wenzao wa Rungwe na kuanza kufanya vibiashara vyao.
Concern yangu Kyela ni maendeleo na wala sio mwanasiasa mmoja mmoja. Sio rafiki wa mwanasiasa yeyote lakini pia si adui wa mwanasiasa yeyote. Kwangu mimi Kyela ni kubwa kuliko mimi au kuliko mtu mwingine yeyote. Yeyote ambaye yuko tayari kukemea ujinga huo, mimi nitamuunga mkono.
Raia Mwema,
...... Hivi mimi Mtanzania leo nikiandaa maandamano ya wahuni pale mjini na kuwapa pesa za soda kisha nikawaambia waseme ninachokitaka, mwandishi makini utachukulia hiyo kama wananchi wa Kyela wanaamini kwamba?
Mbona Raia Mwema ilikuja kwa nguvu zote na kupinga matatizo ya RAI, wakati na nyie mnaandika habari bila hata kufanya analysis? .............
ulivyoandika hapo juu ni wazi unapinga kuwa wananchi wa kyela walisema kilichoandikwa walisema.
kwa mujibu wa raia mwema source ya habari hiyo ni wananchi wa kyela. umejuaje kama ni uongo? umejuaje kama wahuni ndio walikusanywa na kusema kilichotakiwa kusemwa? we chanzo cha habari yako ni nani/nini?
unataka vichwani mwetu tujenge picha kuwa watu wa mwakyembe waliwaambia wahun waseme yaliyoandikwa. lakin for sure watu wasio wahuni wanaweza kutoa habari kama hizo kwa vyombo vya habari
au unataka kutuaminisha kuwa hamna watu wasio wahuni kyela wanaweza kutoa taarifa kama ile kwa vyombo vya habari?
mwakyembe anaweza kuwa na weaknesses nyingi sana. lakin usitake kutuaminisha kuwa ni wahuni tu ndio waliotoa habari kwa raia mwema (japo inawezekana)
kama ulivyosema somewhere - maendeleo ya watu kwanza
Mwakyembe hapa kyela hana pa kuishi na hivyo anaishi GUEST HOUSE.Mara Stiva mara Pataya.
Nadhani haya ndiyo muhimu kujadili kwa sasa,
Mvua kubwa yabomoa nyumba wilayani Kyela
MVUA inayoendelea kunyesha katika Wilaya za Rungwe, Ileje na Kyela mkoani Mbeya hivi sasa imesababisha zaidi ya kaya 40 kukosa makazi ya kuishi wilayani Kyela baada ya nyumba zao kuzama na maji.
Mbali ya kuzamisha makazi ya kaya hizo, mvua hiyo vile vile imebomoa jengo kubwa la Msikiti linalojengwa mjini Kyela na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni tisa.
Mvua hiyo ilianza kunyesha kwa nguvu katika wilaya hizo Machi 31, mwaka huu na maji yake kujaza mito ya Songwe na Kiwira wilayani humo ambapo ilifurika na kusababisha mafuriko yaliyozamisha nyumba za wakazi wa kata mbili za Katumba Songwe na Ngonga.
Kufuatia mvua hiyo kuzidi kunyesha kwa nguvu mfululizo, zaidi ya kaya 40 katika vijiji vya Katumba, Kabanga, Mpunguti pamoja na Ndwanga katika kata ya Katumba Songwe zimekosa makaazi na hivyo kupatiwa hifadhi katika Shule ya Sekondari ya kutwa Katumba Songwe baada ya makazi yao kujaa maji.
Chanzo Mtanzania Jumamosi Aprili 4, 2009
Mkuu haya maneno kweli au?.. mbona unatisha mkuu wangu, yaani kweli haya maswala yametokea nyumbani kwa Diwani!...Kuelezea kwamba nyumba ya wageni ya diwani wa mjini ilitumika kulawitia watoto hao, mtu anakimbilia hoja dhaifu eti Nsesi mkabila, hata katika uchafu kama huo tena ulioripotiwa kwenye magazeti hadi watuhumiwa kufikishwa mahakamani tunataka kupotosha umma kwa kisingizio cha ukabila, ajabu sana.
Nsesi,
Mkuu haya maneno kweli au?.. mbona unatisha mkuu wangu, yaani kweli haya maswala yametokea nyumbani kwa Diwani!...
Duh, jamani mwee nyie acheni ujinga hili swala zito sana kuliko huyo Mwakyembe mara 1000..Hata kama ni swala la Mhariri wa habari kuichapisha gazetini, lakini kama atakataa kuichapisha bado itauzika tena kwa bei kubwa kuliko mshahara wa mwezi -Kuwatahadharisha wananchi!
Nsesi,
wewe unaushabiki wa kitoto.
Sawa hao waandishi hawaandiki mambo uliyo yasema.Je unawatenga watu kutokana na kuwa Taarifa zao hazikutoka gazetini?Ujinga huo sasa.Wao sio wahariri wakuu ndugu yangu.
Swali liko pale pale.
Mwayembe kaifanyia nini Kyela?[/QUOTE]
Nijuavyo aliwajengea au ana mpango wa kujenga shule maana kwenye fundraising hata mie niliwachangieni tena si kitoto!
Au hiyo shule nayo ni hewa?
Mkuu wangu kulingana na habari hiyo, mwenye Guest na hao waliowaliwiti watoto wa shule ya msingi wote wana makosa!..Madai ni kwamba kuna wanafunzi walifanyiwa hivyo vitendo kwenye guest house ambayo mmiliki wake ndiye diwani wa Kyela mjini.
Sasa hapo mwenye kosa ni mmiliki wa guest au hao waliofanya kosa na kukamatwa?
Mtanzania,
Mkuu wangu kulingana na habari hiyo, mwenye Guest na hao waliowaliwiti watoto wa shule ya msingi wote wana makosa!..