Wananchi hao, wakiongozwa na viongozi wao wa jadi na wazee waliandaa maandamano makubwa mjini Kyela, Jumapili iliyopita, maandamano ambayo katika dakika zake za mwisho yalizuiwa kwa amri ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen. Hatua hiyo imeacha maswali mengi yasiyo na majibu.
Katika hili Rais Jakaya Kikwete anapaswa kuelewa kwamba anapolea uozo kama huo wa kudumaza demokrasia na kuwanyima wananchi haki yao ya msingi na kikatiba, anazidisha hasira ya wananchi dhidi yake yeye na wala si hao wasaidizi wake.
Wananchi wa Kyela wanaamini kwamba Rais wao ndiye chanzo cha matatizo yote ya kisiasa yanayowasibu wilayani humo pamoja na mbunge wao.[/COLOR][/font][/size]
Raia Mwema,
Hivi kumbe Kyela kuna viongozi wa jadi? Wamechaguliwa na nani? Najua kuna wazee lakini viongozi wa jadi tena inatoka wapi?
Pia kusema wananchi wa Kyela wanaamini kwamba: utafikiri hata kuna kura ya maoni yoyote umefanya?
Hivi mimi Mtanzania leo nikiandaa maandamano ya wahuni pale mjini na kuwapa pesa za soda kisha nikawaambia waseme ninachokitaka, mwandishi makini utachukulia hiyo kama wananchi wa Kyela wanaamini kwamba?
Mbona Raia Mwema ilikuja kwa nguvu zote na kupinga matatizo ya RAI, wakati na nyie mnaandika habari bila hata kufanya analysis?
Matatizo ya Kyela sio JK wala sio prof. Mwandosya. Matatizo ya Kyela ni ubinafsi wa watu wawili ambao baada ya kushindana mwaka 2005, mpaka leo wameshindwa kabisa kuweka tofauti zao pembeni na kazi zao ni kulalamika kila siku. Wanatumia vijana wasio na kazi na wazee wenye njaa ili kuchochea maugomvi yasiyoisha. Badala ya kutumia resources hiyo ya wananchi ili kusaidia kusukuma maendeleo ya wilaya, viongozi wetu ni majungu tupu usiku na mchana na kuendelea kuwachanganya wananchi.
Kama maandamano yalizuiwa, mbona wafuasi wa mbunge nao walizuia hao waandishi wa Kyela wasiende kwenye mkutano huo. Mimi naona kama ni kitu kile kile cha kutumia mabavu na kutaka kuwalazimisha wananchi wafuate upande mmoja. Kama wananchi wanataka kuandamana, wache waandamane ili mradi hawavunji sheria. Kama kuna mkutano wacha waandishi waje na waandike wanachokijua. Sisi wananchi tuna uwezo wa kuchambua pumba na mchele.