Habari Njema kwa Tanzania toka IBM Company!!

wende

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
714
65
IBM yafungua ofisi Tanzania
na Irene Mark

KAMPUNI ya IBM imefungua tawi lake jijini Dar es Salaam ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake barani Afrika na Dunia nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa IBM hapa nchini David Sawe, alisema uzinduzi huo ni sehemu ya mpango wa kusambaza huduma za kampuni hiyo duniani.
Alisema licha ya IBM kuwepo Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka 50 sasa imefungua ofisi zake nchini ili kuwafikia wateja wake kipindi hiki cha kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.
“Tunazo sababu nyingi za kufungua ofisi Tanzania, tunaamini ipo fursa ya kupata soko la uhakika, imara, sawia na Teknolojia ya Mawasiliano (TEHAMA)… pia kuna uchumi na siasa isiyoyumba.
“Sababu hiyo na nyingine nyingi zimetulazimu kufungua ofisi ya IBM hapa hivi sasa, katika miaka ya hivi karibuni tumejenga uwezo wa kibiashara hapa nchini,” alisema Sawe na kuongeza kwamba wameanzisha makundi ya kusambaza huduma za kibiashara kwenye sekta ya utalii, elimu na TEHAMA.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa IBM Afrika Mashariki, Tony Mwai, alisema hadi sasa zipo ofisi 20 za kampuni hiyo kwenye nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Misri, Afrika Kusini, Senegal na Tunisia.
Nyingine ni Ghana, Morocco, Nigeria, Algeria na kwamba mpango wa IBM ni kuwa na ofisi 40 barani Afrika ifikapo mwaka 2015 huku ikijivunia kuongeza ajira kwa nchi husika.

Yap, hii ni habari njema, naona wanaitangaza sana kwenye google ads na semina kama sikosei watakayofanya movenpick
 
mhhhhh Hivi ni ofisi gani za serikali ziantumia IBM server. ?
 
Wengine hiyo IBM ndo tunaisikia leo tujuzen inahusika na jambo gan hasa.. Na upatikanaji wake ukovipi?
 
DUh such a cool move kwa sisi wadau wa IT i just love that!! tusubiri tuone whatcha gonna do for us!
 
Wengine hiyo IBM ndo tunaisikia leo tujuzen inahusika na jambo gan hasa.. Na upatikanaji wake ukovipi?

International business machine, ni kampuni kogwe manufacturers wa computer and its accessory. Nafkri orgin yake ni ya wa marekani.
 
Marekani wajanja sana hii ni janja ya kututeka kiteknolojia tutumie server zao watusome kila kitu hadi kitanda anacholalia mkulu wa kaya halafu siku wakitaka kitu kwetu mkileta longolongo ni kichapo ka ghadafi.shauri yetu na umaskini wetu.
 
nafasi za ajira wanaICT lkn duuuu...... lkn hawa IBM wawe waangalifu sana na biashara yao maana hapa ma HR wakibongo watajaza ndugu na kujuana kwenye ajira na matokeo yake kazi mbovu mpk ofisi itakufa
 
Wengine hiyo IBM ndo tunaisikia leo tujuzen inahusika na jambo gan hasa.. Na upatikanaji wake ukovipi?

IBM kwa kirefu International Business Machine ni kampuni ya Kimarekani inayotengeneza na kuuza vifaa vya kompyuta na softwares. Bado sijui ofisi zake Tanzania ziko wapi lakini makao makuu yapo New York Marekani
 
Marekani wajanja sana hii ni janja ya kututeka kiteknolojia tutumie server zao watusome kila kitu hadi kitanda anacholalia mkulu wa kaya halafu siku wakitaka kitu kwetu mkileta longolongo ni kichapo ka ghadafi.shauri yetu na umaskini wetu.

unachanga siasa na teknolojia mkuu.

Hawaji kuiteka teknolojia hata wasipokuja Kwa Tanzania server zinazotumika ni IBM na HP na zote za kimarekani. Kama kuna kitu wakitaka ufanya kibatya wanaweza kufanya from remote.

Kujua MKuu analala wapi kwao ni suala dogo hata kwa Google map/earth na intellengcy ndogo wakiamua wanajua . It has nothing to do with IBM

Sio kwamba IBM kufungua ofisi yao ndio wanaanza ufanya biashara Tanzania. Wapo siku nyingi wanawatumia wahindi kula dili. Bora waje wenyewe.

So nadhani hapa umeenda nje kabisa ya mada.

Nawasilisha
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Waje, angalau tupunguze idadi ya computer fake za kichina zilizojaa bongo, hata kwenye maofisi
 
Sure,sure,sure! Ila impact ya IBM kwa chinese fake products + cheaper inaweza kuwa ndogo sana.
 
Kitengo cha COMPUTER kilishauzwa siku nyingi sana na ni Wachina walikinunua na sasa wanaita LENOVO.

Wao wamebaki na hayo ma SERVER na Super Computer zaidi.......

Hizi PC na Laptop ni LENOVO kwa sasa.
 
Waje, angalau tupunguze idadi ya computer fake za kichina zilizojaa bongo, hata kwenye maofisi

IBM fake wapi jamani acheni uzushi. Supply chain ya afrika ukinunua IBM lazima itatoka china tu. Supply chain ya Afrika ukinunua HPor IBM lazima itakuwa ni ya china. Ukiona umenunua IBM au HP east africa imeandikwa imekuwa manufactured Eoroe ujue hiyo ndo fake.

Kitengo cha COMPUTER kilishauzwa siku nyingi sana na ni Wachina walikinunua na sasa wanaita LENOVO.

Wao wamebaki na hayo ma SERVER na Super Computer zaidi.......

Hizi PC na Laptop ni LENOVO kwa sasa.

Hata hizo server mi nimeshaziona most parts zinatengenewa China. Mi nashangaa nchi yetu hata kiwnada cha sindano au vifungo hatuna lakini kuna watu wanaita bidhaa za wenzao fake.
 
IBM yafungua ofisi Tanzania
na Irene Mark

KAMPUNI ya IBM imefungua tawi lake jijini Dar es Salaam ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zake barani Afrika na Dunia nzima.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa IBM hapa nchini David Sawe, alisema uzinduzi huo ni sehemu ya mpango wa kusambaza huduma za kampuni hiyo duniani.
Alisema licha ya IBM kuwepo Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka 50 sasa imefungua ofisi zake nchini ili kuwafikia wateja wake kipindi hiki cha kusherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.
“Tunazo sababu nyingi za kufungua ofisi Tanzania, tunaamini ipo fursa ya kupata soko la uhakika, imara, sawia na Teknolojia ya Mawasiliano (TEHAMA)… pia kuna uchumi na siasa isiyoyumba.
“Sababu hiyo na nyingine nyingi zimetulazimu kufungua ofisi ya IBM hapa hivi sasa, katika miaka ya hivi karibuni tumejenga uwezo wa kibiashara hapa nchini,” alisema Sawe na kuongeza kwamba wameanzisha makundi ya kusambaza huduma za kibiashara kwenye sekta ya utalii, elimu na TEHAMA.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa IBM Afrika Mashariki, Tony Mwai, alisema hadi sasa zipo ofisi 20 za kampuni hiyo kwenye nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Misri, Afrika Kusini, Senegal na Tunisia.
Nyingine ni Ghana, Morocco, Nigeria, Algeria na kwamba mpango wa IBM ni kuwa na ofisi 40 barani Afrika ifikapo mwaka 2015 huku ikijivunia kuongeza ajira kwa nchi husika.

Umesomeka mkuu nilikuwepo kwenye seminar yao jana pale Moven Pick ,tuwape nafasi
 
Back
Top Bottom