kvelia
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 246
- 44
Kada wa CCM Arumeru atimkia CHADEMA
MAMBO ndani yaChama Cha Mapinduzi (CCM) yameendelea kuwa tete baada ya mmoja kati yawalioshiriki kinyanganyiro cha kuomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo laArumeru Mashariki kwa tiketi ya chama hicho, Anthony Musami, kutimkia Chama chaDemokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mgombea huyoambaye ni mkuu wa Shule ya Sekondari ya Leguruki inayomilikiwa na Jumuiya yaWazazi wa CCM alijiunga na CHADEMA juzi, ambapo alichukua fomu za kuombakuteuliwa kugombea ubunge kupitia CHADEMA.
Musamiakiongea na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alikiri kujiunga naCHADEMA na kuongeza kuwa atazungumza na waandishi wa habari leo (Jumapili)kuelezea sababu za kujitoa kwenye chama hicho tawala.
Kada huyo waCCM aliweza kurejesha fomu hizo ambapo alifuata taratibu kwa kujaza nahivyo kuwahi kuzirejesha jana ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho yakuzirejesha.
Katibu waCHADEMA wilayani Arumeru, Totinan Ndonde, aliwaonyesha waandishi wa habari fomuza mgombea huyo ambaye alisema kuwa kama chamawalimpokea na wanaamini atafuata na kukubaliana na taratibu za CHADEMA, ikiwamokuheshimu maamuzi ya vikao halali vya chama.
Kwa upandewake, Katibu wa CCM wilayani Arumeru, Edson Lihweuli, alipopigiwa simu yake yakiganjani na kuulizwa endapo chama chake kina taarifa za kukimbiwa na kadahuyo, katibu huyo alikata simu mara moja na alipopigiwa tena simu hiyo iliitabila kupokewa.
Musami alikuwamiongoni mwa wagombea sita walioshiriki kinyanganyiro cha kura za maoni ndaniya CCM na kuambulia kura 22 kati ya kura 1,134 zilizopigwa.
Mgombea huyoalishika nafasi ya tano kwenye uchaguzi huo ambao mtoto wa aliyekuwa mbunge wajimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari, Sioi Sumari, aliongoza kwa kupata kura361 akifuatiwa na William Sarakikya aliyepata kura 259, Elirehema Kaayakura 205, Elishilia Kaaya 176 na Rishankira Urio aliyeambulia kura 11.
Hata hivyokura hizo za maoni ndani ya CCM zilipigiwa kelele za kuwapo kwa vitendo vyarushwa, hali iliyosababisha mmoja wa wana CCM aliyekuwa amechukua fomu yakuomba kuteuliwa ambaye ni Rais wa Mtandao wa Maendeleo ya Vijana nchini (YDN),Elipokea Urio, kujitoa kwenye kinyanganyiro hicho akipinga vitendo hivyo vyarushwa.
Aidha,mchakato huo wa kupata mteule wa kupeperusha bendera ya CCM umesababishamvutano mkali ndani ya Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (UV CCM) kiasi chakutolewa kwa tamko la kumzuia mjumbe wa Baraza la UVCCM mkoani Arusha, KenedyMpumilwa, kujihusisha na kampeni kwenye jimbo hilo.
Mpumilwa nimmoja kati ya viongozi wa chama hicho waliojitokeza hadharani kupinga vikalimatokeo ya uchaguzi huo kwa madai kuwa yalitokana na ushawishi wa rushwa,kwamba mmoja wa wagombea hao kwa kushirikiana na wapambe wake waligawa fedhakwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu uliompitisha mgombea, hivyo akautakauongozi wa chama kuyabatilisha.
Hata hivyomwishoni mwa wiki Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, akiongea na waandishi wa habari jijini Arusha alielezea kushangazwa nawale wanaolalamikia kuwapo kwa vitendo vya rushwa kwenye kinyanganyiro hicho,kwa madai kuwa havikuwapo na akawataka wakubaliane na matokeo.
Alisema kuwa rushwa inayodaiwa kutolewa haikuwapo, kwani kiongozi wa kimila wa ukoo wa Sumari alitaka kuandaa chakula kwa ajili ya kutoa sadaka ya shukurani kutokana na msiba wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah, lakini Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) walimfuata wakamshauri sadaka hiyo akaitoe kanisani.
SOURSE: TANZANIA DAIMA