Habari Njema kama ilivyoandikwa na Kompanero Mwanamapinduzi

Unabii huu wa campanero utatimia pale tu waalimu wote wa Tanzania na wengine watakaosimamia masanduku ya kuhesabia kura mwezi October watakaposimama kidedea kuzuia wizi wa kura unaopangwa na chama cha mafisadi ili kupoka matakwa ya waliowengi nchini.
Hao waalimu ndo muda muafaka wa kufanya kweli, badala ya kudanganya na vijisent halafu baadae waje kuitisha migomo ya isiyo na mbele wala nyuma!
 
Hongera Kompanero mawazo yanajenga 2010 nadhani Dr Slaa atafanya mabadiriko ..
kama kauli inavyosema sauti ya watu ni sauti ya mungu..naaamini mwenyezi mungu atalisimamia hili.
 
Basi na kila atakayesoma ujumbe huu na amfikishie mwenzake ili nchi yote ikapate kusikia juu ya unabii huu, na wala asitokee hata mtu mmoja wa kupaza sauti ya kwamba hakusikia. Siku yaja, mafisadi na wazandiki watakapotaka kutumia utaratibu wao ule ule wa kujipatia ushindi kwa ulaghai, basi na iwe kwetu nafasi ya kuwakana mchana kweupe kwa kuwa hawayatendi wala hawayaishi wanayonena, nao wamejifanyia nchi hii kivuno chao, wala wasiwakumbuke wapiga kura wao.
 
Wakuu, Dr Slaa atapita kama kutakuwepo na careful strategy atakayo onyesha katika kampeni. Ni muda wa kuwaonyesha watanzania wa kawaida nini atafanya akiingia magogoni. Kazi yakuwaelewesha watanzania wa kawaida ni ngumu ati; lakini tunajitahidi wakuu. Nimedhamiria kuwa "changes must come to TZ 2010, i must be part of it"

Go Dr. Slaa go.:biggrin:
 
Mwaka wa tano wa kutawala kwake Rais Jakaya Kikwete,
Amani Karume alipokuwa Rais wa Zanzibar, na Ali Karume,
ndugu yake, Balozi wa Nchi, na Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania,
wakati wa Uspika wa Samuel Sitta na Anna Makinda, neno la kura
likamfikia Kompanero, mwana wa Kamaradi, jijini.
Akafika nchi yote iliyo karibu na maziwa makuu,
akihamasisha uchaguzi uletao ondoleo la ufisadi,
kama ilivyoandikwa katika juzuu la Mwanaharakati Mwanakijiji:

Sauti ya mtu aliaye vijijini,
Itengenezeni njia ya Dakta,
Yanyoosheni mapito yake.
Kila shimo litafukiwa,
Na kila kifusi kitashushwa,
Palipopotoka patakuwa pamesawazishwa,
Na wote wenye macho watayaona mabadiliko ya kweli.



View attachment 12365
 
Ingekuwa busara kama hizi fulanas zingesambazwa matawi yote ya Chadema nchi nzima na kuwagawia wananchi bure kipaumbele kikiwa kwa wanachama wa Chadema; kwani waccm wanaweza kuzihujumu!!
 
"Iandike njozi ukaifanye wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia"
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom