rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 454
Mkuu Mashauri, hili linawezekana kabisa hata nchini kwetu kama hao (mafisadi) walio madarakani wangeweka maslahi ya Tanzania na Watanzania mbele badala ya kununuliwa kwa kupewa shares chache katika makampuni hayo na hivyo kuwaachia wachukuaji wachukue 96%/97% na kutuachia sisi kiduchu tu na mashimo chungu nzima na huku wamechafua vyanzo vingi vya maji katika maeneo yenye rasilimali.
Ni kweli kabisa BAK. Hawa mafisadi wangeweka mbele maslahi ya taifa lao hiyo inawezekana kabisa na nchi yetu ingepeata maendeleo kwa kasi. Mbaya zaidi ni kuwa hata hizo share wanazopewa kwenye hayo makampuni pesa zao wanawekewa nje ya nchi na mwisho wa siku wanakufa na kuyaacha hayo matrilioni yakiendeleza nchi za wazungu. Mbaya sana hii. Mkapa aliuza madini yetu na Kikwete anaendelea kuyauza na gesi asilia pia, Mwinyi aliuza mbuga za wanyama ili hali wanafahau fika kuwa hata wakistaafu wanatunzwa na serikali mpaka kufa kwao, sijuwi wanataka hizo pesa zaidi za nini! Inashangaza sana hawa viongozi wetu wa kiafrika.