Habari kutoka kwa Dr. Kairuki hospital

Pole sana Mkuu!! Kwa kweli Dr alikiuka maadili ya kazi yake!!

On the other hand, wasichana wengi siku hizi hupenda kuzaa kwa operation, ati ili wasiharibu elasticity ya k*** zao, yaani waendelee kuwa vigori hata kama atazaa watoto! Hii inaweza imechangia kwa maDr wasio na maadili sawasawa kupenda operation hata kama hakuna indication (sababu). Afterall, operation ya aina yoyote ile inaingiza pesa nyingi kuliko matibabu ya aina nyingine!!

Hata hivyo ni kazi ya Dr kumwelewesha patient pros and cons za kila aina ya matibabu.

Mkikukmbuka, huko nyuma (na huenda mpaka leo) mgonjwa bila kuchomwa sindano alikuwa anaona hajatibiwa!

Mkikumbuka zaidi, huko nyuma ilikuwa fashion kwa mwanamke, hasa msomi, kutonyonyesha watoto, ati washaribu shape za vifua vyao!! But slowly after sustained health education, sasa wanawake wanaona pride kuwanyonyesha watoto wao, hata mbele za watu!!

Kwa hiyo ninachotaka kusema ni kuwa a good Dr ni yule anaye toa elimu ya kipi kinafaa kwa wagonjwa wake, siyo yule anayeheshimu matakwa ya wagonjwa wake hata hayo matakwa hayafai, ati kwa kuogopa kumkasirisha patient!!

Drs kwenye private hospitals are very unethical, ingawa Drs wa namna hii pia hupatikana kwenye public hospitals.

Cha kushangaza, utakuta Dr wa public hospital anakuwa na two different faces. Akiwa kwenye public hospital anakuwa ethical, lakini jioni akienda kwenye kubangaiza anavua ethics!!!
 
Pole, hiyo ndio legacy ya Dr Kairuki kama ulikuwa hujui!

Don't try that at Home. Mara mia ukaenda Muhimbili fast track, lakini sio hapo Kairuki, panasifika kwa operesheni za uzazi za kulazimisha.
 
wanandugu majuzi nimempeleka ndugu yangu kwenye hii hospital ya dk kairuki,..wengi walinishauri hosp ya karibu tukaamua kumpeleka hapo
tulipofika binti alikuwa na mimba ya miezi 7 akaongea na dk jinzi ya kuendelea
na clinic na jinsi gani ya kujifungia hakika dk alitukatisha tamaa sijui alikuwa na stress na mkewe ama lah,..alipotujibu mimba ya ngapi akamabiwa ya kwanza ...aisee yaani ukija hii lazima tuitie kisu mimba ya kwanza nyingi ni kisu siku hizi tukamwacha akama dk 5 tukihisi anatania ..akasema else utapata shida kwenye kujifungua m sikudanganyi...

Mmmmh nkasema kama ndio hivi ma ndugu tusonge mbele akaenda aghakhan hospit ndipo alipo mpaka sasa....
Imenishtua kidogo,..madk hata kama mnania operation msiwambie hivi wagonjwa mtawakimbiza jamani

kuna kipindi wanalazimisha kufanya op ili iwe sehemu ya mazoezi yao. Cha msingi ni mzazi kukataa op mpaka itakapolazimu, lakini akileta usisita du, anashindwa kusukuma kwa nguvu/bidii, anaremba, basi lazima apigwe kisu tumboni kitu ambacho sio kizuri
 
Kuna kahospitali kengine kako upanga kanaitwa Tumaini nako kwa kupenda visu weee acha tu.

Visu vinaongezeka kwa kuwa prevalence ya dada zetu warembo ambao ni wafupi kupenda kuolewa na kina kaka warefu imeongezeka sana. Fuatilia.
 
kujifungua mtoto wa kwanza Muhimbili ni better choice, tafuta hela ya kwenda fast track.
hata mie kuna daktali aliniambia niende Mikocheni kwa Kairuki na tukaambiwa tujiandae kwa kisu, sisi hatukuwa tayari kwa majibu hayo tukaenda fast track ya Muhimbili wakafanya vipimo wakatuambia tarehe na my wife wangu alijifungua salama kabisa bila kisu.
Ndiyo hivyo kule Mikocheni ukitumia kisu kumzalisha mtu unalipwa zaidi!!!!

Ivi Fast track ya MNH ni pesa ngapi, nimekuwa nikiitafakari kumpeleka my waifu wangu huko!!
asante
 

Don't
try that at Home. Mara mia ukaenda Muhimbili fast track, lakini sio
hapo Kairuki, panasifika kwa operesheni za uzazi za
kulazimisha.
Private nyingi mimba ya kwanza kisu! Wanataka ukianza kuumwa tu ujifungue faster.
 
haaaa basi ni mchezo wao mi nimepata jibu kama hilo hospitali inaitwaukombozi kinondoni
doc kanishauri eti wanikate ajili njia haijazoea mikiki mikiki kabla hata hajanipima .asee alinishangaza sana
nimeamua kwenda kujifungulia kilimanjaro kwetu kama ni ya kisu ntajua hapo na si kulazimishiwa kisu khaaaaaa yaani ta kumpigia staki tena


hawa wanataka kufanya biashara yao ya operesheni kwa lazima hivi kupata shida wakati wa kujifungua si ni kitu asili???? hebu tujuzeni labda kuna la ziada kwakweli yaani alieniagiza kwenye hospital ile ha
Wanandugu majuzi nimempeleka ndugu yangu kwenye hii hospital ya dk kairuki,..wengi walinishauri hosp ya karibu tukaamua kumpeleka hapo
tulipofika binti alikuwa na mimba ya miezi 7 akaongea na dk jinzi ya kuendelea
na clinic na jinsi gani ya kujifungia hakika dk alitukatisha tamaa sijui alikuwa na stress na mkewe ama lah,..alipotujibu mimba ya ngapi akamabiwa ya kwanza ...aisee yaani ukija hii lazima tuitie kisu mimba ya kwanza nyingi ni kisu siku hizi tukamwacha akama dk 5 tukihisi anatania ..akasema else utapata shida kwenye kujifungua m sikudanganyi...

mmmmh nkasema kama ndio hivi ma ndugu tusonge mbele akaenda aghakhan hospit ndipo alipo mpaka sasa....
Imenishtua kidogo,..madk hata kama mnania operation msiwambie hivi wagonjwa mtawakimbiza jamani
 
kwa kuwa jf na madaktari ni familia moja
bila shaka watatuambia ni kwa nini wanaamua
kufanya hivyo mkuu.
 
kujifungua mtoto wa kwanza Muhimbili ni better choice, tafuta hela ya kwenda fast track.
hata mie kuna daktali aliniambia niende Mikocheni kwa Kairuki na tukaambiwa tujiandae kwa kisu, sisi hatukuwa tayari kwa majibu hayo tukaenda fast track ya Muhimbili wakafanya vipimo wakatuambia tarehe na my wife wangu alijifungua salama kabisa bila kisu.
Ndiyo hivyo kule Mikocheni ukitumia kisu kumzalisha mtu unalipwa zaidi!!!!
lakini mkuu kuna watu zaidi ya wanne na wote walianza clinic mwezi wa tano wa mimba tena private/fast track kwa professor mmoja pale, ukweli ni kuwa mwishoni ilikuwa ni operations!

Naomba tu tuliongelee hili kwa makini

 
Eeeeeeeeebanaeee hii kitu ni cha kawaida ktk hospitali nyingi binafsi.Na hii ni kwa sababu upasuaji huongeza kipato kwao,malipo ya upasuaji ni makubwa kuliko kujifungua kawaida.
Mimi nilimpeleka mke wangu Madafu(hii ni hospitali ya wazazi) iliyoko Ukonga nilipomfikisha pale usiku akiwa na uchungu wakasema nimuache hapo mpaka kesho yake asubuhi nije kuangalia.Kweli mapema asubuhi nikawa pale nikakutana na msimamizi mkuu wa wodi ya wazazi akaniambia mke wangu mtoto hana nguvu kabisa na lazima afanyiwe operation haraka ndani ya nusu saa,basi mimi nilikataa alichoniambia yule dr ni kuwa nihesabu mtoto sina tena.
Basi niliaga nikalipa pesa yao pale nikachukuwa Tax kuelekea Amana Hospital Nilipofika pale wakampima na kuniambia hana tatizo lolote nisubiri nje,baada ya masaa kama matatu nikapigiwa simu na mke wangu kuwa amejifungua salama na mtoto ni mzima kabisa bila shida yoyote.
Mtoto sasa ana umli wa miaka 3 na hakupata matatizo yoyote mpaka leo.Chonde tuwe makini na hospitali zetu hizi binafsi la sivyo tufwile....:A S-coffee:
 
MADAKTARI NJAA!

Sijui kuna bodi yoyote ambayo inashughulika na kupata habari za kiintelijensia za mahospitali yetu haya...!, maana kuna vituko vya ajabu.

How come unamwambia mgonjwa kwamba ...wewe ni wa kisu tu..??..ndo maadili ya uganga hayo?...Ama kweli hakuna taaluma siku hizi...inayopendwa ni ajira tu not anything else!

Je ana umri gani huyo mzazi mtarajiwa?

Hata hivyo ingawa huenda kitakwimu ni kweli,lakini lugha aliyotumia,is unethical..
 
Ila... Kwa upande wa huduma,generally Kairuki is the best! Kwa sisi tunaotumia insurance kwa matibabu,tunapata huduma vema kuliko tunapoenda hospitali nyingine hasa za serikali...I
 
Back
Top Bottom