Habari kutoka kwa Dr. Kairuki hospital

Naomba kuchangia hoja hii ya Dr Kairuki…..
Nakubaliana na waliotangulia kuchangia kwamba suala la madaktari kufuata maadili ya kazi yao ni jambo la muhimu kabisa….na ni kweli katika zama hizi za utandawazi na liberalization maadili yamepungua sana katika fani ya utabibu kama ilivyo kwenye fani nyingine. Tofauti na zamani, watu wanaokwenda kusomea fani za uganga siku hizi hawaendi kwa wito bali ni kupata qualifications ili wapate ajira….
Such bad aples wapo sehemu mbalimbali kwa Kairuki, Aga Khan, hata Hospitali za Uingereza na Marekani (angalia latest incident iliyotokea huko Uingereza http://www.guardian.co.uk/society/2010/feb/25/mid-staffordshire-nhs-trust na http://www.dailymail.co.uk/health/article-490583/Killed-hospital-just-didnt-care--widow-recounts-husbands-final-days.html
That said, lazima ku appreciate kazi kubwa wanayofanya madaktari wengi walio wazuri Tanzania na kwingineko….. Mazuri mengi wanayofanya hayaingii kwenye headlines, isipokuwa few negative isolated incidents. Kwa mtazamo wangu madaktari wetu wa Tanzania haswa wanastahili pongezi kwa sacrifice kubwa, kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na mishahara midogo…kumbuka daktari wa Tanzania mmoja anawajibu wa kutibu watanzania 25,000 (angalia http://www.africapedia.com/wiki/index.php?page=DOCTOR-%20PATIENT%20RATIO%20IN%20AFRICA Tanzania ni nchi ya pili kutoka mwisho katika nchi za Afrika zenye madaktari wachache kulinganisha na population. Kwa hali hii, mara nyingine tunapojikuta tunakutana na madaktari ambao wanafanya kazi kwa uchovu kutokana na kuwa overwhelmed na majukumu iwe kwa Kairuki, au Muhimbili au Hindumandal…mara nyingine lazima kutambua changamoto wanazokumbana nazo…badala ya kuwalaani, tuwaonee huruma…..na kutafuta jinsi ya kuwasaidia….Ukiangaia kwa sura hiyo then utatambua kwamba mjadala tunaotakiwa kuuzungumzia…tufanye nini kuongeza idadi ya madaktari nchini kwetu, tufanye nini maslahi ya wataalam hawa wazalendo walioamua kubaki nchini kuhudumia watanzania wenzao yaboreshwe…..
Nirejee kwenye hoja ya Edo aliyesema legacy ya Dr Kairuki ni kufanya upasuaji
Niweke wazi mapema, mke wangu ametibiwa na Dr Kairuki kwa muda mrefu…na kwakweli bila Dr Kairuki watoto wetu (3) tulionao tusingekuwa nao…ametusaidia sana. Kuna mamia ya watu wenye simulizi kama mimi jinsi walivyofaidika na utaalam wa huyu Daktari mzalendo na hospitali yake… Hivyo kwangu mimi tofauti na Edo legacy ya Dr Kairuki ni outcome ya kazi yake kwa patients wake…ambao wengi leo hii wana watoto na baadhi ya watoto hao ni madaktari, wanasheria, etc na wengine pengine ni wachangiaji wa mijadala kwenye jamii forum……
Pamoja na yote, mapungufu yaliyosemwa hayapaswi kupita hivi hivi, wewe kama ni mteja wao nashauri ukawaambia watu wao wa utawala warekebishe matatizo hayo…ili zahama iliyokupata isimtokee mtu mwingine…
 
aah, lisemwalo lipo kama halipo laja... Tatizo madaktari wa siku hizi hawana ethics za udaktari au kama si hivyo ni njaa tu zinawasumbua ukizingatia mishahara yenyewe ndo kama ile tena.... dah, afadhali kutumia miti shamba ya babu zetu.
 
mpumbavu hutoa maneno ya kipumbavu, bali mwenye hekima huangalia sana aendako!!!
Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake, bali kila mpumbavu ataka kugombana

Fahari ya vijana ni nguvu zao na uzuri wa mzee ni kichwa chenye mvi.
 
Doh! pole Ahgakhan is the worst!!!!! I lost my wife in front of my eyes!!!!!!!
Try regency, it worked very well with my family. My wife had five (not all are for the babies) successful c-sections at this hospital. But it need close follow for huzy and wify!
 
Hii ni matokeo ya kuchanganya biashara na huduma. With Oparation, its more money.
Lakini pia baadhi ya wadada zetu wa kisasa, wanaprefer kisu ili 1.Wazijifungue kwa uchungu. 2. Wamaitain ubinti! na wengine hufikia hatua hata ya kutomnyonyesha maziwa ya mama ili kumaitain saa sita kamili!.

Madaktari wengi wanafanya kazi nzuri, tusiichafue kwa hawa wachache wanaofanya madudu.
 
Pamoja na yote, mapungufu yaliyosemwa hayapaswi kupita hivi hivi, wewe kama ni mteja wao nashauri ukawaambia watu wao wa utawala warekebishe matatizo hayo…ili zahama iliyokupata isimtokee mtu mwingine…

Well said Pareto, Kwa muda mrefu hii imekuwa miongoni mwa Hospitali ambazo zimekuwa zikionesha juhudi za dhati katika kutoa huduma kwa ufanisi wa hali ya juu. Nimeguswa na story yako, lakini sisi kama customers wao, we have to provide feedback kwa uongozi bwana. Hii ni pamoja na kushare concerns kama hizi kwa utawala wao. You should inform management yao juu ya huyo daktari..

Binafsi nimekuwa mteja wa hospitali hii for years and I have always been enjoying the best health care services vissioned by its founder, kairuki.

Kuondoka kimya pasipo kuchukua hatua inayoweza kuwasaidia ku-improve won't be fair to both parties I.e. Kwa watu wao wa utawala na to you and me as consumers of their services.


 
Hospital nyingi za private zipo kibiashara zaidi na operation ndiyo inayolipa zaidi. Kwani hata Aghakani si hivyo hivyo tu?? Je nani anakumbuka hospital ya Dr. Andrew hapo Mbuyuni Ada Estate enzi hizo? Massana hospital Mbezi kwa Dr. Lema usiombe, nafikiri ndiyo anashikilia usukani kwa sasa baada ya Dr. marehemu Mod alikuwa na hosp hapo Ilala(Sikimbuki vizuri sana). Kwa mantiki hii, ni vema kuanzia sasa kama hujaanza basi jitahidi uwe na family doctor tu, japo kwa ushauri genuine!!
 
Mimi mke wangu alijifungua salama salmini hapo hapo Kairuki bila kisu wala nini nadhani we should not rely on doctor's but God other wise we will keep on running from one hospital to another. Every hospital has its positive and negative sides.
 
Doh! pole Ahgakhan is the worst!!!!! I lost my wife in front of my eyes!!!!!!!

Pole sana mkuu. Mungu akuongeze katika maisha yako.

Duh kumbe miye namlilia mtoto wangu mchanga kufa kwa uzembe wengine mke kabisa
 
Lakini wana JF habari nilizo nazo ni kuwa kina dada wengi wanaomba kisu ili njia yake ya kawaida isipanuke sana. Huo ndio ujumbe niliopata baada ya kuona wadada wengi hususan wanaojifungua mtoto wa kwanza. Chunguza utaniambia.
 
Kuna rafiki yangu aliambiwa mimba yake mtoto amefia tumboni wakamlaza ili wamtie kisu kutoa kiumbe but mumewe akakataa akaenda Muhimbili wakagundua mtoto yu hai na leo hii ana zaidi ya miaka sita healthly
 
Eeeeeeeee........banaeee hii kitu ni cha kawaida ktk hospitali nyingi binafsi.Na hii ni kwa sababu upasuaji huongeza kipato kwao,malipo ya upasuaji ni makubwa kuliko kujifungua kawaida.
Mimi nilimpeleka mke wangu Madafu(hii ni hospitali ya wazazi) iliyoko Ukonga nilipomfikisha pale usiku akiwa na uchungu wakasema nimuache hapo mpaka kesho yake asubuhi nije kuangalia.Kweli mapema asubuhi nikawa pale nikakutana na msimamizi mkuu wa wodi ya wazazi akaniambia mke wangu mtoto hana nguvu kabisa na lazima afanyiwe operation haraka ndani ya nusu saa,basi mimi nilikataa alichoniambia yule dr ni kuwa nihesabu mtoto sina tena.
Basi niliaga nikalipa pesa yao pale nikachukuwa Tax kuelekea Amana Hospital Nilipofika pale wakampima na kuniambia hana tatizo lolote nisubiri nje,baada ya masaa kama matatu nikapigiwa simu na mke wangu kuwa amejifungua salama na mtoto ni mzima kabisa bila shida yoyote.
Mtoto sasa ana umri wa miaka 3 na hakupata matatizo yoyote mpaka leo.
Chonde Chonde tuwe makini na hospitali zetu hizi binafsi la sivyo tufwile....:A S-coffee:
 
Muhimbili fast track is the best. Mimi watoto wangu wote enzi hizoo walizaliwa pale salama kabisa.
 
Wanandugu majuzi nimempeleka ndugu yangu kwenye hii hospital ya dk kairuki,..wengi walinishauri hosp ya karibu tukaamua kumpeleka hapo
tulipofika binti alikuwa na mimba ya miezi 7 akaongea na dk jinzi ya kuendelea
na clinic na jinsi gani ya kujifungia hakika dk alitukatisha tamaa sijui alikuwa na stress na mkewe ama lah,..alipotujibu mimba ya ngapi akamabiwa ya kwanza ...aisee yaani ukija hii lazima tuitie kisu mimba ya kwanza nyingi ni kisu siku hizi tukamwacha akama dk 5 tukihisi anatania ..akasema else utapata shida kwenye kujifungua m sikudanganyi...

mmmmh nkasema kama ndio hivi ma ndugu tusonge mbele akaenda aghakhan hospit ndipo alipo mpaka sasa....
Imenishtua kidogo,..madk hata kama mnania operation msiwambie hivi wagonjwa mtawakimbiza jamani

Alimuuliza hivyo
baada ya kumpima? Lakini hata hivyo lugha aliyoitumia ni unethical, yaani haikuzingatia maadili.
 
Kuna kahospitali kengine kako upanga kanaitwa Tumaini nako kwa kupenda visu weee acha tu.
 
Back
Top Bottom