Ha..hahaa mathematiks bwana raha sana kama ulifeli poleee!!

siku hizi ma binti wa shule wanaita hesabu BABA MKWE kwa jinsi wanavyoiogopa
 
nimezipenda zote 2.
Safi sana tukielimishana hv,hasa ss tulio kimbia pure!
 
Maisha yametawaliwa na hesabu. Kujua hesabu kuna raha yake.
 
nashukuru,ingawa sikuwa mzuri wa hesabu darasani,lakini sikuwahi feli hesabu..form four niligonga ka D kangu safi na six kwenye BAM nikagonga ka S,mambo yakawa mswano!Kuna washkaji zangu wengine walikuwa na div one kali,lakini wakafeli hesabu na kujikuta wako kwenye div 3,noma kweli hasa pale kufaulu hesabu inapokuwa kigezo cha kuwa admitted kwenye kozi unayoipenda chuo kikuu.
 
ivi zile hesabu za x na y huwa zna application gan ktk maisha mkuu?
Unamaanisha algebra? Kimsingi kila hesabu zina application na kila kitu kilichotengenezwa na mwanadamu kiwe kimesimama au kinatembea, hesabu nyingi tu zimetumika. kwa mfano hebu angalia chupa ya bia. Unataka kutengeneza chupa ya bia inayoweza kubeba 0.5ltr za bia na kubaki nafasi ndogo kama 0.005ltr kwa ajili ya gas. Sasa je kitako kiwe na kipenyo cha urefu gani? hali kadharika urefu wa chupa hadi mabegani na ule wa shingo pamoja na kipenyo cha mdomo wa chupa
 
> 1 x 9 + 2 = 11
> 12 x 9 + 3 = 111
> 123 x 9 + 4 = 1111
> 1234 x 9 + 5 = 11111
> 12345 x 9 + 6 = 111111
> 123456 x 9 + 7 = 1111111
> 1234567 x 9 + 8 = 11111111
> 12345678 x 9 + 9 = 111111111
> 123456789 x 9 +10= 1111111111

Safi sana hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom