Ha ha ha wazee wa mjini noma!

EMEDNEY

Member
Sep 20, 2012
72
38
[h=5]Mwanasheria mmoja alienda porini kuwinda, akampiga swala risasi lakini swala akakimbia na kuingia katika kibanda cha mzee mmoja...
Mwanasheria: "Mzee kuna swala wangu kaingia kibandani kwako namuomba...."
Mzee: "Kama yuko kwangu huyo wangu..."

M/Sheria: "We mzee mi mwanasheria maarufu ntakupeleka mahakamani utalipa swala na fidia..."
Mzee: "Hakuna haja ya hilo, huku kwetu tunasheria inaitwa mateke makumi kumi.... Tunapigana mateke kumi kumi mpaka mmoja akubali kushindwa...."

Mwanasheria kuona kale kazee kalivyo akakubali akijua zamu yake ikija atakapiga mpaka kakubali..... Mzee akaanza teke la kwanza katikati ya miguu ya mwanasheria, teke la pili kamfumua pua, teke la tatu, la nne mpaka la kumi akamalizia kwenye nyeti za jamaa....

Mwanasheria akaamka kwa uchungu na hasira ili nae amtwange babu mateke....

Kabla hajafanya chochote, Babu akawahi....
'Aaaah, we chukua tu swala wako nimeshindwa mimi!!!!"

[/h]
 
Mi ningekachapa ngumi na mateke ya kutosha halafu na swala nasepa naye,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom