Ha! ha! ha! Hivi ndo Russia ilivyowaachia pirates

hivi sivyo tunavyotakiwa kuishi mkuu, every person on earth deserves a second chance, hata kama ni muuaji, jambazi, pirate etc, he still needs a chance to repent and come to his God, change his ways brabrabraaa. wahalifu si pirates peke yao, kama wewe ni mtakatifu uwe wa kwanza kurusha jiwe. je, haujawahi kula rushwa hapa tz? bila shaka siongei na fisadi, ila kama ni mmoja wao basi fisadis za tz ni wabaya kuliko hata pirates. those people live in a failed state and sometimes they are driven by warlords, ambao kama wakikataa kufanya hivyo wanaweza kuuawa. pia mazingira ya somalia yanawaweka watu kuwa katika roho ya aina hiyo, if they would have been given a chance to live in a peaceful country like tz, unafikiri wangeopt kufanya wayafanyayo? hata hivyo, many of you in this JF are pirates before God, kama Mungu angelihesabu maovu yetu nani angesimama? na Mungu hafurahii kifo cha mtu mwenye dhambi, hivyo si sahihi kabisa kuwaua hivyo. wenzao wa EU na NATO wamekuwa na agreement na selikali ya Kenya, so when they capture them wanawapeleka kwenye mahakama za kenya kutokana na mutual agreement za nchi walivyokubaliana. kama Mungu angekuwa anawaua enyi wanaume mnaoharibu vitoto vya secondary hata shule havimalizi, je mngesimama? kama Mungu angeamua kuharibu/kuua enyi sugermami mlio jaa dar es salaam wamama watu wazima mnawavulia watoto wadogo kama si laana hiyo ni nini? je, mngesimama mbele za Mungu kweli? si neema tu ya Mungu tunaishi wakuuu?

hata hivyo, siiamini hii thread iliyoanzisha, kwasababu kama wangefanya hivyo, jumuiya ya kimataifa ingeshawashambulia sana Russia....

Swadakta mkulu na maelezo yako nadhwifu.

Tatizo la pirates ukilitazama na ukachimba source yake, unaeza ikuta ipo hukohuko kwa wazungu. Sasa kidogo inanitatiza kuona mtu mweusi akishangilia kuona mtu mweusi mwenzake akiuawa kwa kifo cha kikatili kabisa na hii mijitu mweupe isiyo na chembe za huruma.

Siungi mkono kwa asilimia 100, na vivohivo sipingi kwa asilimia 100 suala la uharamia kwene meli. Watu wanasahau kuwa Somalia haina serikali, its a anarchy state, na kuna tuhuma kwamba dola za kigeni wameifanya ile pwani kuwa sehemu ya kutupa taka za sumu, pamoja na uvuvi haramu.
 
Wanafanya mambo ya Uharamia sio kwa sababu wanapenda ila kwa sababu njaa na Nchi yao ina matatizo ya Kisiasa hakuna Serikali huko Somalia shida tupu wanauwana wao kwa wao Tangu Aondoke Dikteta Siad Bare nchi imekuwa kwenye matatizo na hao hao wakubwa wa Dunia Amerika, Rusia,china, Ufaransa na Uingereza wamelifumbia macho kwa sababu kule Somalia hakuna Kitu chochote laiti somalia kungekuwa na Mafuta ungewaona hao watu weupe wangekuja upesi kutatuwa Matatizo na wala kusingekuewepo na vita vya wenyewe kwa wenyewe hayo ndio matatizo ya Mataifa ya kimagharibi wanakwenda mahali palipo na maslahi yao wao wenyewe mimi mpaka leo inanishangaza Umoja wa nchi huru za Afrika umeshindwa mpaka hii leo kutatuwa Tatizo la Somalia?hivi wamelifumbia macho hilo tatizo la Somalia hao viongozi wa Nchi huru za kiafrika kwanini? wanavyofanya hao pirates wa Kisomali ni sawa tu kwa sababu ya njaa waache wafanye na hao Warusi kuwauwa hao vijana na sio ndio kumaliza tatizo la hao pirates, wakae wazungu na Viongozi wetu wa Nchi za Kiafrika watafute Ufumbuzi wa Nchi ya Somalia kuwepo na Serikali huru inayotambuliwa na wanachi wake kisha waone kama kutakuwepo tena na matatizo ya hao pirates Mwenyeezi mungu ndio atakae wasaidia ndugu zetu wa Somalia kupatikana kwa Ufumbuzi wao inshallah.
 
SIdhani kama kuwatosa wale baharia 12 ndio suluhisho la kudumu bali itakuwa ni kichocheo zaidi cha uharamia; na kwa taarifa yetu hao jamaa jana tu wameteka meli nyengine ya Ugiriki (Elen P).

Source: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2010/05/100512_somalia_ugiriki_maharamia.shtml

090603020250_somalipirates386.jpg
Picha kwa Hisani ya BBC Swahili
 
High risk high return, let them know that nothing comes without a cost. If they know pirating will risk their lives they'll probably try fishing
 
Mimi siungi mkono maharamia ila kama kweli Urusi wamefanya kitendo hicho cha kuwaacha katikati ya Bahari bila vifaa si kitendo kizuri kabisaa. Ni kitendo cha uharamia pia.
 
Maharamia walikutana na Maharamia wenzao! wasio na chembe ya utu kwa mtu asiye wa taifa lao.
 
this is too unfair, walitakiwa wawakamate wawapeleke mbele ya vyombo vya dola, na sio kuuwaacha kinyama hivyo. you know, kila mwanadamu hata kama ni jambazi,katili etc, ni kiumbe wa Mungu na Mungu bado anampenda, na anastahili haki zote. siamini kwamba Russia nchi iliyokomaa ktk sheria za kimataifa ingefanya kitu kama hicho. lazima watakuwa waliwaacha na hata kadarubini kamoja ili wasijekujikuta badala ya kwenda somalia, wanaelekea china ambako watatembea kwa miaka miwili na hako kaboat. si unajua mtu akiachwa katikati ya bahari hajui wapi kusini, wapi kaskazini etc.

Sawa kabisa hao majambazi ni viumbe wa Mungu, na warusi wamefanya vema kumwachia Mungu viumbe wake awatunze, kuna tatizo hapo? Kwani kuna anayemzuia huyo Mungu asiwaokoe hao viumbe wake walioachwa baharini wajiendee kivyao?
 
ii ndio inavyotakiwa hawa pirates hata wakikamatwa kwao ni kwamba wameenda ulaya still is ok to them, ila kwa hili they surely re think their strategies
 
hapa ndio nachanganyikiwa na taratibu za kisheria! wapelekwe mahakamani wakati pirates wenyewe wameshajitolea kufa maana wanajua fika hiyo ni do-or-die game,sasa wewe unatoa wapi huruma? kwavile ni mwafrika mwenzangu ndio nitetee upuuzi? go to hell you pirates!!!! hivi hamuoni huruma kwa hao wanaolipa hizo ransom za hadi 3 Millions USD? Hii kazi sasa inawavutia zaidi vijana wa kisomali kwa hicho mnachokiita 'haki za binadamu au mkondo wa sheria'.
 
Back
Top Bottom